Ukubwa wa vazi la wana anga lawa kikwazo cha kutimiza ndoto za wanasayansi wa kike

Wana anga wanawake Haki miliki ya picha NASA
Image caption Christina Koch (kushoto) atavaa vazi alilolivaa Anne McClain (kulia) atakapofanya safari ya anga siku ya Ijumaa

Mipango ya wana anga wanawake katika historia kufika kwenye anga la juu imezimwa baada ya kukosekana kwa vazi rasmi la pili, Shirika la anga za juu nchini Marekani NASA limeeleza

Christina Koch na Anne McClain walikuwa wakitarajiwa kutoka nje ya kwa ajili ya kupachika betri.

Lakini ikagundulika kuwa wote wawili walitakiwa kuwa na mavazi rasmi ya wana anga ambapo ni vazi moja pekee lililokuwa tayari kwa matumizi.

Hoteli ya kwanza katika anga za juu

Ujumbe kutoka anga za juu?

Sasa Koch atafanya kazi hiyo na mwana anga mwenzie wa kiume Nick Hague.

Atavaa mavazi ya ukubwa wa kati yaliyotumiwa na McClain alipofika kwenye anga la juu juma lililopita.

McClain ana uzoefu wa kutembea angani na mavazi ya saizi kubwa na ya kati lakini aligundua kuwa saizi ya kati inamtosha vizuri zaidi.Shirika la anga za juu Nasa limeeleza.

Anatarajiwa kufika tena kwenye anga la juu , tarehe 8 mwezi Aprili, akiwa na mwana anga wa kiume, David Saint-Jacques.

Mavazi hayo yana tatizo gani?

Shirika la NASA lina aina mbili za mavazi ya size ya kati.Lakini kuliandaa vazi jingine huchukua saa kadhaa hivyo Nasa iliona kumbadilisha mwana anga mwingine

Brandi Dean, Msemaji wa kituo cha anga Johnson Space mjini Houston, ameeleza kuwa ukubwa wa vazi hubadilika pale mwana anga anapokua angani tayari.

mahitaji ya ukubwa wa nguo huweza kubadilika wanapokua kwenye muhimili , kutokana na mabadiliko ya hali ya mvutano.Alinukuliwa na shirika la AFP.