Pentagon yaidhinisha dola bilioni 1 za ujenzi wa ukuta wa mpaka wa Marekani na Mexico

Picha ya uzio wa Marekani unaotenganisha mpaka baina ya Marekani na Mexico US and Mexico, viungani mwa mji wa Nogales, jimboni Arizona, Februari 9, 2019 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tayari upo uzio unaotenganisha mpaka baina ya Marekani na Mexico

Wizara ya ulinzi ya Marekani The Pentagon imeidhinisha kuhamishiwa kwa dola bilioni moja ($1bn) kwenye akaunti ya wahandisi wa jeshi kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa mpaka baina ya Marekani na Mexico.

Fedha hizo ni za kwanza kutolewa chini ya hali ya tahadhari ya kitaifa iliyotangazwa na rais Donald Trump ambazo hazikupitishwa na baraza la Kongresi na kujenga kizuwizi alichokiahidi wakati wa kampeni zake za uchaguzi.

Democrats wameipinga hatua hiyo.

Pesa hizo zitatumiwa kujenga uzio wa maili 57.

Rais Trump ameitaja hali katika mpaka wa kusini kama "mzozo " na akasisitiza mpaka kizuwizi halisi kinahitajika ili kuwazuwia wahalifu kuvuka mpaka na kuingia Marekani .Wakosoaji wake wanasema amebuni dharura ya mpaka.

Taarifa ya Pentagon imesema kaimu waziri wa ulinzi wa Marekani Patrick Shanahan alikwa "amemuagiza kamanda wa kikosi cha Marekani cha wahandisi kuanza kupanga na kutekeleza usaidizi wa dola bilioni 1 kwa wizara ya usalama wa ndani na udhibiti wa mipaka na forodha".

Taarifa hiyo ilielezea sheria ya serikali kuu kwamaba "inaipatia Wizara ya ulinzi mamlaka ya kujenga barabara na uzio na kuweka taa za barabarani kwa ajiliya kufunga mapito baina ya mipaka ya kimataifa na Marekani kama sehemu ya kusaidia kukabiliana dhidi ya shughuli za narcotic chini ya taasisi za usalama ".

Pamoja na ukuta huo wenye urefu wa futi 18 "uzio wa wapitanjia ", fedha hizo zitatumika katika ukarabati wa barabara na kuweka taa mpya.

Seneta wa Democratic alilalamika kuwa Pentagon haikuomba ruhusa ya kamati husika kabla ya kulifahamisha baraza la Kongresi kuhusu utoaji wa pesa hizo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption maelfu ya watu huvuka mpaka kila mwaka wakitafuta maisha mapya nchini Marekani

" Tunapinga vikali malengo ya kuhamishwa kwa fedha na pia utekelezaji wa wizara wa kuhamishwa kwa fedha bila kuomba idhini ya kamati za bunge za Kongresi za usalama Kongresi na ukiukaji wa vipengele vya ugawqaji wenyewe wa wizara ya ulinzi ," Waliandika katika barua kwa Bwana Shanahan, limeripoti shirika la CNN.

Bwana Trump alitangaza dharura tarehe 15 Februari baada ya Kongresi kukataa ombi lake la kuidhinishwa kwa dola bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa ukuta.

Kwa kutangaza hali ya tahadhari alipata uwezo wa kutolihusisha baraza la Kongresi na kujenga ukuta kwa pesa za jeshi.

Democrats walisema tangazo hilo si la kikatiba.

Bunge la Wawakilishi linalodhibitiwa na Democratic lilipitisha azimio la kupinga dharura hiyo mwezi uliopita, na wabunge 12 wa Republican baadae walijiunga na maseneta wa Democratic kuipitisha katika Seneti

Haki miliki ya picha AFP

Hata hivyo, Bwana Trump alitumia mamlaka aliyonayo kupiga kura ya veto dhidi ya maazimio hayo mapema mwezi huu.

Kwa sasa Kongresi itahitaji kuwa na theluthi mbili ya walio wengi katika mabunge yote kumpiku , jambo ambalo waandhishi wa habari wanasema huenda lisiwezekane.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii