Wanafunzi waliokamatwa Burundi waachiwa huru

Pierre Nkurunziza Haki miliki ya picha Twitter/Various
Image caption Si mara ya kwanza kwa wanafunzi kukamatwa kutokana na vitendo hivi

Burundi imewaachilia huru wanafunzi watatu wa kike ambao walikamatwa wakishutumiwa kuichafua kwa kuichorachora picha ya rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kwenye vitabu vyao vya shule.Waziri wa sheria Aimée Laurentine Kanyana ameeleza.

Kushikiliwa kwa wasichana hao takribani majuma mawili yaliyopita kwa shutuma za kumtusi rais kulizusha kampeni mitandaoni za kutaka wasichana hao waachiliwe kampeni iliyokua na jina #FreeOurGirls, watu wakituma picha kwenye mitandao ya Twitter.

Waziri amesema wasichana hao wenye miaka 15,16 na 17 wameachiwa huru kwa muda.

Kwa nini watu wanaweka michoro katika picha za rais huyu?

Rwanda yawataka raia wake walio karibu na mpaka wa Burundi kusitisha biashara na nchi hiyo

''Tunawataka wazazi kuboreha elimu ya watoto wao .Tunawakubusha watoto kuwa wanapaswa kuheshimu mamlaka,na kuwa umri wa kuwajibishwa ni miaka 15

Walikamatwa walipokuwa katika shule ya ECOFO iliyopo katika mkoa wa kaskazini wa Burundi wa Kirundo tarehe 12 mwezi Machi ,2019

Awali walishitakiwa wakiwa wanafunzi saba, lakini wanne wakaachiliwa huru.

Haki miliki ya picha Lewis Mudge
Image caption Mchoro unavyoonekana

Watatu hao walikua wanashikiliwa kwenye gereza la wanawake la mkoa wa Ngozi.

Mnamo mwaka 2016 shule mbali mbali mjini Bujumbura na mikoani watoto kadhaa walitiwa mbaroni wakihusishwa na matukio ya aina hiyo.

Shirika la kutetea watoto FENADEB lilikua msitari wa mbele kuwatetea watoto hao.

Mashirika ya kutetea haki za watoto nchini Burundi yameshauri uchunguzi wa kina ufanyikekabla ya kuwatia watoto hao hatiani ili kubaini ni kwa nini matukio kama hayo yanajitokeza.

Mada zinazohusiana