Uhamiaji wa Afrika: Mambo matano tuliojifunza

Mwanaume mmoja akisukuma mizigo katika uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi, Kenya. Haki miliki ya picha AFP

Zaidi ya mtu mmoja kati ya watu watatu barani Afrika ameishawahi kufikiria uwezekano wa kuhama, kulingana na watafiti wa taasisi ya Afrobarometer.

Utafiti wao katika mataifa mengi ya Afrika pia umebaini kuwa vijana na wasomi ndio wenye uwezekano mkubwa wa kutaka kuzihama nchi zao.

Kwa wale ambao huhama , hawahamii tu katika Mataifa ya ulaya au Marekani ambako wengi huenda, lakini pia huhamia katika mataifa mengine ya Afrika.

Yafuatayo ni mambo matano tuliyofahamu kutokana na ripoti:

Kwa nini watu wanataka kuhama?

" Kutafuta ajira " na " kuukimbia umaskini na ugumu wa uchumi " zilikuwa ndio sababu kubwa za kutaka kuhama katika nchi karibu zote 34 zilizofanyiwa utafiti kwa kiwango cha 44% na 29%.

Kuwa na wanafamilia au wapendwa nje ya nchi inaweza kuwa sababu pia ya kufanya uhamuzi wa kuhama.

Afrobarometer ilibaini kuwa mmoja kati ya watu watano hutegemea walau 'kiasi kidogo' cha pesa zinazotumwa kutoka nchi nyingine. Robo ya watu waliofanyiwa utafiti wanasema mtu mmoja katika familia amekuwa akiishi katika nchi nyingine katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Wanataka kwenda wapi?

Wengi hawataki kwenda Ulaya au Marekani , ila katika mataifa ya Afrika.

Watu wanaosema wanaangalia uwezekano wa kuhama wengi wao wangependa kuishi katika kanda zao kwa kiwango cha (29%) au katika mataifa mengine ya Afrika kwa kiwango cha (7%).

Haki miliki ya picha Getty Images

Lakini watafiti walibaini baadhi ya tofauti za kushangaza.

Watu wa kusini mwa Afrika walionyesha utashi mkubwa wa kukaa katika kanda yao kwa kiwango ya (58%), huku hisia hizi zilikuwa tofauti sana katika kanda ya Afrika magharibi ambapo ni asilimia (8%) pekee waliokuwa na utashi wa kuendelea kubaki katika kanda yao.

kwa wale wanaosema wanataka kuhama bara na kuelekea Ulaya walikuwa ni (27%) na Marekani walikuwa ni (22%).

Ni nani mwenye uwezekano mkubwa wa kuondoka ?

Takriban nusu yote ya vijana na raia wenye kisomo cha juu walisema waliwahi kufikiria kuihama nchi yao walau "kidogo ".

" Fikra za kuhamia nchi ya ng'ambo zimekuwa za kawaida miongoni mwa watu wenye maisha mazuri na maskini ", kulingana na ripoti ya Afrobarometer.

Wanaume ni zaidi (40%) kuliko wanawake (33%) wanasema wanaangalia uwezekano wa kuhama , na watafiti walibaini kuwa haja ya kuhama ilikuwa ya kiwango cha juu miongoni mwa watu wanaoishi katika maeneo ya mijini (44%) kuliko maeneo ya vijijini (32%).

Ni nchi gani watu wanataka kuzihama zaidi?

Moja ya mambo yaliyojitokeza zaidi katika utafiti ni kwamba 37% - zaidi mtu mmoja kati ya Waafrika watatu - wamewahi kufikiria kuhamia ng'ambo . Ni chini ya nusu tu ya wale waliosema hili ni jambo ambalo waliwahi kulifikiria ''sana'' .

Inapokuja katika suala la kuhama , 7% ya watu wa Zimbabwe na Lesotho wanasema wanajiandaa sasa kuondoka, ikilinganishwa na wastani wa Afrika wa 3%.

Nchi ambazo zaidi ya nusu ya raia wake wanafikiria uwezakano wa kuondoka walau "kidogo" ni Cape Verde (57%), Sierra Leone (57%), Gambia (56%), Togo (54%), na São Tomé na Príncipe (54%).

Lakini hii haitoi picha kamili . Sudan Kusini, ambayo haimo katika utafiti wa Afrobarometer, imeshuhudia watu wake milioni 2.2 wakikimbilia katika nchi jirani tangu vilipoibuka vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013.

Nchi ya Eritrea pia haikuhusishwa na utafiti ambapo Umoja wa mataifa unasema wakimbizi 2,500 huvuka mpaka kuingia Ethiopia kila mwezi.

Ni vikwazo gani vya kusafiri vinavyowakabili watu?

Uhuru wa kutembea kwenye mipaka ya kimataifa miongoni mwa nchi za kanda vinafikia kwa kiwango cha 56% kulingana na majibu ya watu waliozungumza na utafiti wa Afrobarometer.

Lakini takriban idadi sawa na hiyo ilisame inakuwa vigumu kuvuka mipaka kufanya kazi au biashara katika nchi nyingine.

Katika miaka ya hivi karibu nchi za Namibia, Mauritius, Ghana, Rwanda, Benin na Kenya zimelegeza masharti ya wasafiri kutoka mataifa mengine ya Afrika , na sasa zinatoa visa unapowasili au huwaruhusu kutembelea nchi hizi kwa siku 90 ukiwa na paspoti tu.

Haki miliki ya picha Getty Images

Lakini raia wa nchi za Afrika bado wanahitaji kuwa na visa kusafiri katika zaidi ya nusu ya mataifa ya bara la Afrika , zikilinda mipaka iliyochorwa na wakoloni wa Ulaya zaidi ya karne iliyopita.

"Mtu kama mimi, licha ya ukubwa wa Jumuiya yetu, ninahitaji visa 38 kutembea katika nchi za Afrika," alilalamika bilionea wa Nigeria Aliko Dangote katika mahojiano mwaka 2016.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii