Utata wa kubusu pete ya Papa sivyo ulivyochukuliwa

Pope Francis akipokea pete ya dhahabu kama ishara ya uongozi wake Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Pete ya Papa ya mvuvi ni ya kipekee kwa kila mkuu wa kanisa katoliki , na huharibiwa anapofariki

Ni vipi unapaswa kumsalimia Papa? Kwa karne nyingi , ulikuwa ni utamaduni wa Kikatoliki kubusu miguu ya papa. Siku hizi, wengi wa wakatoliki huchagua kuinama na kubusu pete ya Papa.

Wakatoliki wasiotaka mabadiliko , ambao mara nyingi wamekuwa wakimshutumu Papa Francis kwa kutofuata mafundisho na asili ya kikatoliki , sasa wanashuku ameondoa utaratibu wa kuibusu pete yake.

Wanasema hayo wakionyesha video iliyochukuliwa Jumatatu katika mji wa Italia wa Loreto, ambapo Papa anaonekana akiukwepesha mkono wake wakristo wa kikatoliki waliokuwa wakijaribu kuibusu pete yake.

Lakini picha kamili ilikuwa ni tofauti

Tendo la Papa katika video ni sehemu ya video ndefu.

Picha za Televisheni rasmi za Vatcan zinaonyesha Papa Francis akiwa amesimama alipokuwa anaupokea msururu wa tu kwa dakika 13 na kuwapokea watawa takriban 113 wakiwemo watawa wa kike na wakuu wa parokia , mmoja mmoja au wakiwa wawili.

Hakuna yeyote aliyeonekana kutoa mwongozo juu ya namna ya kumsalimia Papa. Katika kipindi cha dakika 10 za kwanza, watu 14 walimsalimia kwa mkono Francis na bila kuinama kuibusu pete yake.

Katika kipindi hiki ,watu 41 waliinama kwenye mkono wa Papa Francis , kwa kuonyesha ishara ya kubusu pete yake na wengine hata kuibusu.

Papa hakupinga.

Tisa waliinama na kuibusu pete yake, na kumkumbatia.

Baada ya dakika 10 za mwanzo, mwenendo wa Papa ukabadilika . Mstari wa salamu ilionekana kusonga kwa kasi.

Katika kipindi cha dakika 53-kipindi cha pili, Papa Francis alianza kutupa mkono wake mbali na watu 19 waliokuwa wakijaribu kumuinamia na kuibusu pete yake . Mtu mmoja ambaye alikuwa na bahati mbaya alijipata akibusu mkono wake baada ya Papa kukwepesha ghafla mkono wake.

Na hii ndio sehemu ya video iliyosambazwa kwenye mtandaoni.

Huenda ikawa kwamba Papa alikuwa na haraka ya kumaliza shughuli ya kuwasalimia waumini - na hicho ndicho hasa kinachoonekana , baadaye, alitumia muda zaidi kuwasalimia watu wengi wakiwa kwenye viti vya walemavu, mbele ya kanisa .

Huenda Papa Francis asifurahie kitendo cha watu kuibusu pete yake, lakini si sahihi kusema kuwa aliwakataa wale wote waliojaribu kuibusu pete yake.

Pete ya Upapa, inayovaliwa kwenye kidole cha pete cha mkono wa kulia, huenda ikawa ni ishara kubwa zaidi ya mamlaka ya Papa.

Papa anapofariki dunia mara moja huwa inaharibiwa ili kuonyesha mwisho wa uongozi wake.

Kuibusu pete ya Papa mara kwa mara huwa ni jambo linalotia hofu kwa wengi kwani kwa karne kadhaa ni jambo linalohusishwa na ishara ya kidini au kisiasa.

Haki miliki ya picha Bettmann / Getty
Image caption Mbele ya macho ya watu, aliyewahi kuwa rais wa Marekani John F Kennedy aliamua kutoibusu pete ya Papa Paul VI

Mnamo mwaka 1963, Rais wa Marekani John F Kennedy, aliyekuwa Mkatoliki, aliamua kwa makusudi kutoubusu mkono wa Papa Paul VI walipokutana Vatican – kwa hofu ya kutowapa nafasi wakosoaji wake waliosema rais mkatoliki analazimika wakati wote kuutii uongozi wa Roma.

Papa wa sasa anafahamu fika maana ya ishara ya kubusu pete yake.

Inawezekana kwamba angependa kutumia njia nyingine.

Katika ziara ya pamoja mjini Jerusalem Mei 2014, Francis alifanya juhudi kubwa kuubusu mkono wa kiongozi la Kanisa la Orthodox , Ecumenical Patriarch Bartholomew I, kama ishara ya maridhiniano baina ya makanisa ya kikristo.

Katika ziara hiyo hiyo , katika kumbukumbu ya Israel ya mauaji ya Holocaust , Francis alikaribishwa kusalimiana na manusura wa Holocaust.

Walishangazwa na kwamba ,Papa aliinamisha kichwa chake na kuibusu mikono yao - ishara ambayo ilikumbukwa miaka ya baadae.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii