Islamic State: Ni maeneo gani duniani ambayo vitendo vya wapiganaji wa IS vina nguvu?

Ufilipino imekuwa ikishambuliwa sana na IS katika miaka ya hivi karibuni Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ufilipino imekuwa ikishambuliwa sana na IS katika miaka ya hivi karibuni

Baada ya miezi kadhaa ya mapigano , kundi la wapiganaji wa Jihad IS hatimaye limepoteza eneo la Beghuz , kijiji kimoja mashariki mwa Syria ambacho kilikamilisha uwakilishi wa mwisho wa uongozi wa kundi hilo.

Huku hilo likiwa pigo kubwa , kupoteza kijiji hicho kilichopo karibu na mpaka wa Iraq hakumaanishi kuangamia kwa kundi hilo ambalo lina uwezo wa kutekeleza shambuio kali duniani.

Wapganaji wa IS na washirika wake wanaendelea kuwa na nguvu katika mataifa kadhaa wakidai kutekeleza mashambulio kila siku kupitia mtandao wa kundi hilo.

Data iliokusanywa na BBC Monitoring inaonyesha kwamba licha ya kupoteza himaya yake nchini Syria na Iraq mwisho wa 2017, IS linadaiwa kutekeleza mashambulio 3,670 duniani kila mwaka ikiwa ni sawa na mashambulio 11 kwa siku mbali na mashambulizi 502 mwanzoni mwa mwaka 2019 wakati kijiji cha Beghuz kilipokuwa kimezungukwa.

Kulikuwa na kilele cha mashambulio ya IS mnamo mwezi Septemba 2018.

Kilele hicho kilihusishwa na operesheni ilionzishwa mapema mwezi huo na kikosi cha Syria kinachooungwa mkono na Marekani SFD kwa lengo la kuteka ngome kuu za IS za Hajin na kasakazini mwa Baghuz.

Kundi hilo la Jihad hutekeleza mashambulio yake ili kulipiza kisasi mashambulio dhidi yake katika eneo lililozunguzwa ama kwengineko kule ili kuwafanya maadui zao kuondoa mafikra yao kwao na kupeleka kwengineko.

Ijapokuwa Iraq na Syria yanaendelea kupata mashambulio mengi ya IS, Afghanistan , Somalia, Ufilipino , Nigeria na Misri pia hushambuliwa mara kwa mara.

Katika ujumbe wa hivi karibuni, uongozi wa IS ulikejeli madai ya rais Donald Trump mnamo mwezi Disemba ya kulishinda kundi hilo huku kundi hilo likisisitiza kwamba bado vita hivyo havijaisha.

Hatahivyo uongo wa kundi hilo umekuwepo tangu 2017, baada ya kupoteza ngome yao kuu mji wa Mosul nchini Syria na Raqqa nchini Syria.

Baadaye , kundi hilo lilishindwa kujikuza kama linaloendelea na linaloweza kujikimu

Jinsi data ya IS zilivyokusanywa.

Data hiyo inatokana na kile ambacho kundi hilo limekuwa likidai kupitia mtandao wake wa Nashir News Agency katika programu yake ya kutuma ujumbe wa Telegram.

Tarehe hiyo inaonyesha siku ambayo IS inasema kuwa mashambulio hayo yalifanyika badala ya tarehe ambayo madai hayo yalichapishwa.

Data hiyo inashirikisha kila madai ya shambulio, bila kujali udogo wake ama athari zake.

Mashambulio mengi yanayodaiwa kufanywa na IS kupitia gazeti lake la kila wiki al-Naba bila kutoa taarifa tofauti hayakuwekwa katika data hiyo.

Ni muhimu kusema kuwa IS ni kama kundi jingine la Kijihad , na linapenda kuongeza chumvi viwango vya mashambulio yake na athari zake.

IS imetangaza rasmi kwamba ina uwakilishi katika mataifa ya Iraq, Syria, Libya, Misri, Yemen, Saudia , Algeria, "Khorasan" (Jimbo la Afghanistan-Pakistan ), "the Caucasus", "mashariki mwa Asia" (lililopo Ufilipino), Somalia, na magharibi mwa SAfrika husuasana Nigeria.

Baadhi ya matawi haya , kama vile Algeria na Saudia, hayajathibitisha vitendo vyovyote vya IS katika maeneo hayo .

Kundi hilo hivi karibuni lilitoa ishara za kutaka kuanzisha vitendo vyake nchini Tunisia , taifa ambalo kundi hilo limeshindwa kuingia na kujistawisha kufuatia shambulio la 2015 la jumba la kumbukumbu na ufukwe wa kitalii.

IS pia ilitangaza kwa mara ya kwanza uwepo wake Burkina Fasso.

Tangazo hilo kuhusu Tunisia na Burkina faso linaonyesha kuwa katika propaganda , IS inaonyesha kuwa ajenda yake ya 'Kusalia na kupanuka'' inaendelea.

Kisichochangaza , ni kwamba ngome kuu za mashambulizi ya kundi hilo zinasalia kuwa Iraq na Syria ambapo ina raslimali zake kuu.

Kati ya takriban mashambulio 3,670 ya IS duniani mwaka 2018, mashambulio 1,767 yalifanyika nchini Iraq huku mashambulizi 1,1124 yakifanyika nchini Syria.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jeshi la Nigeria limekuwa likishambuliwa sana na IS katika miezi ya hivi karibuni

Lakini mwaka uliopita kuliripotiwa ongezeko la vitendo vya IS katika matawi mengine.

Ni kana kwamba kundi hilo lilitaka kufidia kwa kupoteza kwake nchini Iraq na Syria na kuwakumbusha watu kwamba lilifanya operesheni zake nje ya mashariki ya kati.

Mwaka 2018, IS lilidai mashambulio 316 nchini Afghanistan , 181 nchini Misri katika rasi ya sinai , 73 nchini Somalia, 44 nchini Nigeria, 41 nchini Yemen na 27 nchini Ufilipino.

Idadi ya mashambulio yaliosemekana kufanywa na Is katika eneo la mkoa wa magharibi mwa Afrika yameongezeka katika miezi ya hivi karibuni.

Jeshi ndio ambalo limekuwa likilengwa kwa sababu kundi hilo linatafuta silaha ili kuweza kupiga jeki uwezo wake.

IS limedai kutekeleza mashambulio 44 nchini Nigeria katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2019, likisawazisha idadi ya mashambulio lililotekeleza mwaka 2018.

Katika kanda ya video ya propaganda iliotolewa mwezi Januari, kundi hilo lililopo mkoa wa magharibi lilitoa wito kwa Waislamu kuelekea katika eneo hilo na kujiunga na tawi lake likiashiria kwamba liko tayari kupokea wapiganaji wa kigeni.

Mwezi Machi 22, IS magharibi mwa Afrika lilitangaza kuwa kwa mara ya kwanza lina uwakilishi Burkina Faso-taifa ambalo kundi pinzani la al-Qaeda lilitekeleza mashambulio kadhaa.

Pia kumekuwa na ongezeko la mashambulio yanayodaiwa kutekelezwa na Ufilipino.

IS inafanya operesheni zake katika taifa hilo kupitia washirika wake wengi wao wakiwa wamekuwa wakipigana ili kustawisha taifa la Kiislamu kusini kwa miongo kadhaa.

Lakini mashambulio yake dhidi ya jeshi hilo yametapakaa.

Mwaka uliopita lilidai ,mashambulio manne nchini Uingereza, ikiwemo shambulio la Manchester Arena , mashambulio ya Barcelona nchini Uhispania na lile la Las Vegas nchini Marekani.

Lakini baadhi ya mashambulio hayo yanadaiwa kuwa ya kuvizia kwa kuwa kundi hilo halikutoa ushahidi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii