Paka shume na mbwa koko wanalaumiwa kwa kuharibu baianuwai na kutokomeza baadhi ya viumbe

Feral cat Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paka shume wanaweza kuua baadhi ya wa mwituni

Wanasayansi wanapigia chapuo kutengwa ama kutokomezwa kabisa kwa kwa paka shume, mbwa koko, panya, mbuzi na nguruwe katika baadhi ya maeneo ili kulinda viumbe vilivyo hatarini kutoweka.

Endapo wanyama hao wataondoshwa kwenye zaidi ya visiwa 100 kunaweza kulinda viumbe waliyomo hatarini kutoweka, wanashauri timu ya wanasayansi wa kimataifa.

Visiwa mbali mbali duniani vimepoteza zaidi ya asilimia 75 ya ndege, wanyama wa nchi kavu na majini katika ndani ya miaka 500 iliyopita.

Upotevu huo kwa kiasi kikubwa umechangiwa na wanyama ambao walipelekwa na binaadamukatika maeneo hayo, mathalan paka na mbwa.

Wanyama hao wa kufugwa majumbani sababu hawana asili ya maeneo hayo, huwa tishio kubwa kwa viumbe vyenye asili ya maeneo hayo.

"Kuwatokomeza wanyama wawindaji katika visiwa ni moja ya njia kubwa ya kuondosha hatari ya viumbe wa visiwani kutokutokomea na kulinda baianuwai," amesema Dkt Nick Holmes, kutoka kwenye kundi la wanasayansi la Island Conservation.

Utafiti wao umebainisha visiwa 107 ambavyo iwapo wanyama wawindaji wakiondoshwa kutasaidia kutunza asilimia 9.4 ya viumbe vilivyo kwenye hatari ya kutoweka duniani.

Haki miliki ya picha Andy Schofield (rspb-images.com)
Image caption Ndege hawa, Tristan albatross, wanaopatikana kwenye visiwa vya Gough Island pia wamo kwenye tishio la kutoweka
Haki miliki ya picha Jonathan Hall (rspb-images.com)

Stuart Butchart, mwanansayansi mkuu wa Birdlife International, amesema iwapo hatua hizo zitachukuliwa itasaidia pakubwa kuwalinda "viumbe wa kipekee ambao wamekuwa kwa upekee na katika mazingira yao binafsi ambao hupatikana katika visiwa vya mbali kabisa."

Tayari baadhi ya visiwa vimeshaanza kutekeleza mangamizi hayo. Programu kubwa zaidi ya kutokomeza panya hivi karibuni ilitangazwa kufanikiwa katika visiwa vya South Georgia. Some culls have already taken place on islands. Visiwa hivyo ambavyo ni milki ya Uingereza kusini mwa bahari ya Atlantiki kwa mara ya kwanza katika miaka 200 havina panya kabisa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mbuzi pori nchini Australia wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuharibu mazingira.

"Utafiti huu unaonesha namna gani ni muhimu kuondosha wanyama wavamizi ili kuzuia kutomea zaidi kwa viumbe asilia na vilivyo kwenye hatari. Kinachohitajika sasa ni utashi wa kisiasa na fedha ili kutekeleza miradi hii ili kuvirejeshea visiwa hivi sura yake asili ya kimazingira inayovutia," amesema Jonathan Hall ambaye ni Mkuu wa milki zote za Uingereza zilizopo maeneo ya mbali.

Mada zinazohusiana