Boeing yatangaza marekebisho ya hitilafu za ndege zake 737 Max

Kifusi cha ndege ya Ethiopian Airlines chapa 302 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kifusi cha ndege ya Ethiopian Airlines chapa 302

Kampuni ya Boeing imetangaza mabadiliko kwenye mfumo wake wa kuzuwia ajali unaohusishwa na ajali ajali mbili za ndege zake za 737 Max zilizosababisha vifokatika kipindi cha miezi mitano.

Lakini bado haijajulikana ni lini ndege hizo zilizozuwiwa kusafiri kote duniani mwezi huu zitaruhusiwa kupaa.

Wachunguzi wa ajali bado hawajaeleza sababu ya ajali hizo.

Kama sehemu ya kuboreshandege hizo , Boeing itaweka mfumo wa onyo kulingana na viwango ,ambao awali ulikua si wa lazima.

Ndege zake zilizopata ajali za makampuni ya Lion Air ya Indonesia na Ethiopian Airlines, hazikuwa na mfumo wowote wa kuashiria ajali, ambao lengo lake ni kuwaonya marubani wakati mtambo wa uongozaji wa safari ya ndege unapotoa taarifa kinyume na matarajio.

Boeing imesema makampuni hayatakuwa yakitozwa pesa za ziada kwa ajili ya kuweka mfumo huo wa usalama wa ndege.

Nini kitabadilishwa?

Mtengenezaji wa ndege pia amesema atafanyia mabadiliko programu ambao umehusishwa na ajali.

Mfumo wa MCAS , ulioundwa kuzuwia ndege kupoteza mwelekeo , huwa unatambua taarifa za kifaa cha kutambua ikiwa ndege mwinuko wa kasi ya kupindukia au la.

Lakini uchunguzi wa ajali ya ndege ya Lion Air iliyotokea mwaka jana ulionyesha kuwa mfumo huo ulikuwa haufanyika kazi ,na kulazimisha ndege kuelekea chini zaidi ya mara 20 kabla ya kuanguka ndani ya bahari na kuwauwa abiria 189 pamoja na wahudumu.

Shirika la safari za anga la Marekani (FAA) linasema ajali hiyo inafanana na ile ya Ethiopian Airlines iliyotokea tarehe 10 Machi.

Boeing imetengeneza programu ili kuzuwia mfumo wa MCAS ikiwa utapokea taarifa zenye mkanganyo kutoka kwenye kifaa cha utambuzi wa mfumo wa uongozaji wa ndege.

Katika taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari Boeing ilisema kuwa kubadilishwa kwa mfumo wa usalama wa ndege zake hakumaanishi kukiri kuwa mfumo uliokuwepo ulisababsiha ajali .

FAA yenyewe pia lilichunguzwa Jumatano

Katika kikao cha seneti kilichojadili usalama wa ndege, maseneta walimuhoji kaimu mkuu wa FAA Daniel Elwell juu ya namna wanavyowafuatilia wafanyakazi wa makampuni yanayotengeneza ndege katika mchakato wa kuzikagua , kuzipima na utoaji wa hati kwa makampuni yanayomiliki ndege.

Utaratibu huo ulielezewa na mmoja wa maseneta, Richard Blumenthal, kama unaoendeshwa na "watu wanaoongoza nyumba ya kuku".

Bwana Elwell alikanusha kuwa "wanajipatia vibali " akidai kwamba FAA "imeweka masharti makali ya mchakato wa ukaguzi " wa ndege . Alisema utaratibu huo unatumiwa kote ''duniani''

Bwana Elwell aliongeza kwamba kama FAA hawakuweza kuwapatia mamlaka hayo watengenezaji wa ndege ,na iwapo wangefany ahivyo italazimika kuwaajiri zaidi ya wafanyakakazi 10,000 , gharama ambayo itakuwa juu zaidi kwa dola bilioni 1.8

Image caption Waombolezaji wakihudhuria ibada ya waathiriwa wa ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines

FAA pia lilikosolewa kwa kuwa ya mwisho kuziwekea marufuku ndege za Boeing baada ya ajali ya Ethiopian Airline tarehe 10 Machi.

Calvin Scovel, ambaye ni mkaguzi mkuu wa idara ya uchukuzi , ambaye pia alifika mbele ya Kongresi , alisema : "Wasimamizi wengine wa usalama wa ndege kote duniani walichukua maamuzi kutokana na nafasi yao kama wasaimamizi , walihitaji kuzuwia hatari na walifanya hivyo kwa kupiga marufuku ndege ."

Hata hivyo bwana Elwell alisema FAA walitaka kusubiri hadi wapokee taarifa muhimu kabla ya kuchukua maamuzi.

Bwana Elwell alisema kuwa "aliamini " katika mfumo wa MCAS na marubani walipewa mafunzo ya kukabiliana na hali ambapo ndeg inaanguka ghafla.

Lakini alipoulizwa juu ya namna yeye angeweza kushughulikia ndege ambayo inashuka mara 21, katika kipindi cha dakika kadhaa kama ilivyotokea kwa ndege ya Lion Air ya Indonesia ilivyofanya kabla ya kuanguka mwezi oktoba, Bwana Elwell, ambaye ni rubani alisema : "Nitarejea kuzungumza nanyi baadae juu ya hilo."

Ratiba

Awali alipokuwa akitangaza mabadiliko ya mfumo wa uongozaji wa ndege katika chumba cha rubani Boeing ilisema mfumo wake mpya wa programu ya software utawasilishwa kwa Shirika la safari za anga la Marekani (FAA) kufikia mwisho wa wiki.

Lakini iliongeza kuwa ndege zitatakiwa kuweka programu hiyo , kutoa mrejesho juu ya utendaji wake na kuwapatia mafunzo marubani kabla ya mabadiliko hayo kuidhinishwa na ndege kufikia viwango vya kupaa tena.

Haki miliki ya picha Boeing
Image caption Hakuna ratiba ya ndege ya Boeing 737 Max ya kurejea angani

Wachunguzi bodi ya taifa ya Marekani ya usalama wa safari , mamlaka ya Ufaransa ya uchunguzi wa safari za ndege pamoja na wizara ya uchukuzi ya Ethiopia kwa pamoja wanatarajia kutoa ripoti ya awali juu ya ajali ya ndege ya Ethiopia wiki hii.

Afisa wa Boeing alisema : "Kufuatia tukio la kwanza nchini Indonesia tulifuata matokeo ya mamlaka huru zilizochunguza data, kama tunavyofanya kila mara kuboresha ambapo tunaweza kupata njia za kuboresha, tunafanya mabadiliko hayo ili kufanya maboresho."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii