Unaweza kuwazuwia wazazi kuwashirikisha watu picha zako mtandaoni?

Baba akichukua picha ya selfie na mtoto mchanga anayelia Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption "Kushirikisha picha" -ni raha isiyo hatari au kuingiliwa kwa maisha ya mtu

Upende usipende, wazazi wameingia kwenye mitandao ya habari ya jamii , na yaelekea hawataacha kuitumia.

Ni njia nzuri ya mawasiliano- na mara nyingi inachekesha unapomuona mzazi wako akijaribu kujipiga selfies au akitumia ishara ya hisia fulani kujibu ujumbe.

Lakini kama watashirikisha umma picha zao kwenye mtandao bila idhini yako - na bila kufahamu maisha yako ya kibinafsi yako vipi - watakuwa wamevuka mpaka?

Na kama unataka ikitaka ziondolewe unawezaje kuwashawishi wazitoe mtandaoni ?

"Sharenting" -ikimaanisha mtindo wa wazazi kushirikisha jamii habari na picha za watoto wao mtandaoni - ni jambo lililovuma kwenye taarifa za habari baada ya Gwyneth Paltrow kutuma picha yake na binti yake mwenye umri wa miaka 14- Apple Martin wakiteleza kwenye barafu.

Zaidi ya watu 150,000 walibonyeza ishara ya kuipenda picha, lakini Apple hakufurahia hilo aliandika kwenye ukurasa wake wa kibinafsi wa Instagram: "Mama tulilijadili hili. usitume kitu chochote bila ruhusa yangu."

Paltrow alijibu: "Huwezi hata kuona uso wako!"

Wengi miongoni mwa wafuasi wa Paltrow , walidai kuwa kama mama yake ana kila haki ya kushirikisha jamii picha za binti yake - lakini wengine wakasema watoto wanahaki ya kuwa na maisha yao ya kibinafsi pia.

Kwanini watu huudhika wazazi wao wanaposhirikisha umma picha zao?

La kushangaza , watoto hata hawaruhusiwi kusajiliwa na huduma nyingi za mitandao ya kijamii hadi wanapotimiza umri wa miaka 13 - hii ikimaanisha kuwa watoto wanaofuata sheria hushituka sana wanapojipata wako mtandaoni.

Konrad Iturbe, mwenye umri wa miaka 19 mtengenezaji wa programu ya kompyuta ya software kutoka Uhispania amasema alikuwa na "mshituko mkubwa alipokuwa na umri wa miaka 14" alipogundua kuwa wazazi wake wamekuwa wakituma picha zake mtandaoni.

Haki miliki ya picha Konrad Iturbe
Image caption Konrad: "Ilikuwa ni zamani , picha zilipotea, lakini sasa kila kitu kiko mtandaoni na kitakuwa huko daima"

"Mama yangu alikuwa kwenye Instagram kabla hata sijamiliki simu -kwa hiyo sikufahamu b kuwa picha zangu zilikuwa zinachapishwa " aliiambia BBC.

"Kusema ukweli sipendi picha zangu ziwekwe mtandaoni kwa njia yoyote - situmi picha zangu kwenye ukurasa wangu wa Instagram - kwa hiyo nilipomfuatilia mama yangu na kuona picha zangu kwenye utambulisho wake, nilimwambia nilimwambia ' aziondoe, sikukupatia ruhusa '."

"Sikutaka umma ushirikishwe picha zangu za ujana , ni jambo la siri sana," alisema, akiongeza kuwa pia alihofia juu ya "kutambuliwa kwa sura yake " na hivyo kuwawezesha watu "kuanza kumtafuta atakapokuwa mtu mzima ".

Sonia Bokhari, mwenye umri wa miaka 14 raia wa Marekani pia alikumbwa na hali kama hiyo alipojiunga na mitandao ya Twitter na Facebook.

Katika simulizi yake kwenye Jarida la Fast Compay alisema: "Nilipoona picha ambazo mama yangu amekuwa akituma kwenye Facebook kwa miaka , nilijihisi kuaibika sana na nikahisi nimesalitiwa sana.

"Pale kwa kila mtu kuangalia kwenye akaunti yake ya Facebook ya umma,kilikuwa ni kipindi cha aibu cha utoto wangu : barua niliyoandika nikiwa na umri wa miaka mitano, picha zangu nikilia nilipokuwa mchanga , na hata picha nilizopigwa tulipokuwa mapumzikoni nikiwa na miaka 12 na 13 ambazo sikuzifahamu ."

Si wote wanaojali wazazi wao kushirikisha picha zao kwa umma ", hata hivyo. Charlotte Christy, mwenye umri wa miaka 23 anayesomea London, anasema binafsi anadhani ni ''jambo la kawaida'.'

Haki miliki ya picha Charlotte Christy
Image caption Charlotte, kutoka Marekani, anasema mama yake anashirikisha umma picha zake sasa

Alikuwa na umri wa miaka 13 mama yake alianza kuweka picha zake kwenye Facebook. "Salikuwa nanishirikisha pia na ziliweza kuangaliwa na yeyote .Nilidhani lilikua ni jambo la aibu , lakini halikuniudhi kiasi cha kumwambia aziondoshe."

"Ninadhabi tunaishi katika jamii ambapo kila mtu anataka picha yake kuwa kupendeza - lakini kama mama yangu atatuma picha yangu ambayo haipendezi haiwezi kunikera."

Wazazi kushirikisha umma picha za watoto wao linawezakuwa jambo hatari?

Kwa Sarah (sio jina lake halisi), mwenye umri umri wa miaka 29- mwenye taaluma ya afya kutoka Hong Kong,jambo linalotia hofu zaidi ni athari za maisha yako binafsi.

"Nilipokuw na umri wa miaka 21, mama yangu alinishirikisha picha zake kwenye Facebook, na nikaona kwamba alikuwa anaweka picha zangu - kuanzia nilipokuwa mtoto mchanga hadi nilipokuwa na miaka ishirini na zaidi ," aliiambia BBC.

"Ukurasa wake ulikuwa unaweza kutazamwa na kila mtu, kwa hiyo nilihisi usalama wangu uko hatarini. Sikutaka picha zangu nikiwa mchanga zionwe na kila mtu, na nilifahamu kuwa kutokana na Google, unaweza kutafuta jina la mtu kwa kutumia picha yake. Na kwake kuendelea kutuma picha zangu zaidi mtandaoni, makampuni ya teknolojia yana data zangu zaidi juu ya sura yangu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wataalamu wanasema kwa wazazi kushirikisha umma picha za watoto wao wanawatia katika hatari ya unyanyasaji wa mtandaoni

kuna umuhimu wa wazazi kuzingatia ruhusa ya watoto wao wanapotuma picha zao mitandaoni?

Prof Siibak anasema wazazi wengi wanahisi kuwa , kama mtu mzima, wanawajibika kwa hali bora ya waotot wao ,na hawahitaji ruhusa ya mtoto ilimtradi wanaamini kuwa picha hazina madhara

Hata hivyo , anasema kuwa wazazi wanapaswa'' kabisa'' kuzingatia hofu za taarifa za kibinafsi za watoto wao kama kitu muhimu zaidi.

" Kuwa na mazungumzo rahisi yanayowahusisha watoto juu ya aina za picha wanazopenda, au kama ni sawa kuziweka mtandaoni , husaidia kujenga uhusiano mzuri kati ya mzazi na mtoto."

Mara nyingi wazazi huweka taratibu kali za matumizi ya mtandao kwa watoto wao ili kulinda taarifa zao binafsi, lakini "taratibu hizo zinaonekana kuwahusu watoto tu na zi watu wazima katika familia ".

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Prof Siibak anasema kujadili kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii yanaweza kujenga imani

Ni vipi unaweza kuwashawishi wazazi wako kubadili namna wanavyotumia mitandao ya kijamii?

Ni vigumu - hasa kwasababu hakuna njia za kawaida au za kisheria za kuwazuwia kutuma taarifa mtandaoni. mara kwa mara njia ya kutumia ni ya ushawishi au kuafikiana.

Konrad anapendekeza njia iliyo bora ni kuwaomba wazazi kwa unyenyekevu ambazo wanaweza kuzielewa.

"Ninaweza kusema ni vipi ungejihisi babu yangu angetuma picha za mambo yanayokuaibisha kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti?. Enzi zenu, picha zilikwa zinapotea , lakini sasa kila kitu kiko mtandaoni na hakiwezi kutoka daima."

"Ni njia yao ya kukuonyesha ni kwa kiasi gani wamewakosa na kuwakumbuka watoto wao [wanapokuwa hawaishi pamoja] - hiyo ndio sababu kuu niliamua kutomkataza kabisa mama yangu kutuma picha zangu."

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii