Jo Cameron hahitaji kutumia dawa ya kuondoa maumivu, madaktari wasema hii si hali ya kawaida

Jo Cameron Haki miliki ya picha Jo Cameron
Image caption Jo Cameron hahisi maumivu

Jo Cameron aligundua kuwa ngozi yake inaungua mpaka anaponusa harufu ya kuungua kwa ngozi yake.Mara nyingi mikono yake huungua kwenye jiko la kuokea, lakini hahisi maumivu ya kumpa tahadhari kuwa yuko hatarini.

Yeye ni mtu wa pili duniani kuwa na hali hii ya mabadiliko ya kijenetiki ambayo hutokea kwa nadra sana.

Ina maanisha kuwa Jo Cameron huwa hahisi maumivu kabisa, hana wasiwasi wala huwa hapati hofu.

Hali ilikua hivyo mpaka alipotimiza miaka 65, ndipo alipogundua kuwa yuko tofauti-pale madaktari waliposhindwa kuamini kuwa hahitaji dawa za kuondoa maumivu baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa.

Kwa nini wasichana huchomwa moto matiti yao Afrika magharibi

Papa kutibu binadamu saratani na 'uzee'

Alipofanyiwa upasuaji kwenye mkono wake, madaktari walimtahadharisha kuwa ategemee kupata maumivu baada ya upasuaji.

lakini bi Cameron hakuhisi maumivu yeyote, Daktari wake wa dawa za usingizi Devjit Srivastava alimpeleka kwa wataalamu wa masuala ya maumbile na jenetiki katika chuo cha London na Oxford.

Baada ya vipimo, walibaini kuwa ana mabadiliko kwenye vinasaba vyake vinavyomfanya asihisi maumivu kama ilivyo kwa watu wengi.

'Hii si hali ya kawaida'

Jo aliiambia BBC kwa madakrari hawakumuamini alipowaambia hahitaji dawa ya kuondoa maumivu baada ya upasuaji.

Alisema:''Tulizungumza kabla ya kwenda kwenye chumba cha upasuaji na nikawahakikishia kuwa sitahitaji dawa za kuondoa maumivu.

''Alipogundua kuwa sikuwahi kumeza dawa za maumivu, alitazama historia yangu ya kitabibu na kugundua kuwa sikuwahi kutumia dawa za kuondoa maumivu.''

Ndio sababu hata akapelekwa kwa wataalamu nchini Uingereza.

Haki miliki ya picha Jo Cameron
Image caption Jo,akiwa na mume wake na mama yake.

Ilipobainika, Jo alijua kwamba kumbe hakuwa na'' afya njema'' sana kama ailivyokua akiamini.

Alisema:''Nikikumbuka huko nyuma, nikagundua sikuwahi kuhitaji dawa za kuondoa maumivu,lakini kama huzihitaji huwezi kuhoji kwa nini huhitaji.

''Wewe ni wewe ulivyo mpaka pale mtu mwingine atakapobaini vinginevyo.Nilikua mwenye furaha ambaye sikubaini kama kuna tofauti yoyote mwilini mwangu.''

Hakuwahi kupata maumivu hata wakati anajifungua, akikumbuka:''halikua jambo la kawaida, lakini sikuwa na maumivu. kwa kweli niliifurahia hali hii.''

Jeni zenye kuleta furaha

Madaktari waliamini kuwa Jo atakua na uwezo wa kupona haraka sana kuliko kawaida.Jeni zake pia zinamfanya asahau na asiwe mwenye hofu

''Inaitwa jeni zenye kuleta furaha au zinazosahau.Nimekuwa nikiwaudhi wengine kwa kuwa na furaha na mwenye kusahau maisha yangu yote-Nina sababu sasa,'' alieleza.

Jo alisema hivi karibuni alikua na uvimbe mdogo baada ya kujigonga akiwa kwenye gari, lakini hali hiyo ambayo wengi wangeiona mbaya sana, haimkumshtua hata kidogo.

''Sina adrenalini.Lazima uwe nayo ili iweze kukupa tahadhari kuhusu hali ulionayo, ni sehemu ya hali ya kuwa binaadamu,lakini siwezi kubadili hali hii.''

Dereva mwingine, alisema, ''Alikua akitetemeka kwelikweli'',lakini aliweza kutulia baadae.''Mimi hali hii hainitokei...si kuwa mimi ni mwerevu, ni kwamba hali ya hofu haijitokezi.''

Watafiti wanasema inawezekana kuna watu wengine kama Jo.

''Mmoja kati ya wagonjwa wawili baada ya upasuaji hupata maumivu kidogo au maumivu makali, pamoja na kuwepo kwa uboreshwaji wa dawa za kuondoa maumivu. alisema Dokta Srivastava.

Aliyoyapitia Jo yamo kwenye maandiko ya utafiti wa British Journal of Anaesthesia, ulioandikwa na Dokta Srivastava na Dokta James Cox

Mada zinazohusiana