Jamii ya India ambayo watoto wakubwa wa kike hulazimishwa kuwa makahaba

Katika jimbo hili wazazi huwalazimisha watoto wao kuingia katika ukahaba

Familia nyingi za India huependelea kujipatia watoto wavulana.

Lakini wakati Heena alipozaliwa wazazi wake walisherehekea. Lakini sio kwa sababu nzuri

Heena ni miongoni mwa jamii za mashambani za Bacchara.

Kwa karne kadhaa, watu wa jamii hiyo wanawalazimisha wasichana wao wakubwa walio na umri kati ya 10 hadi 12 kushiriki katika ukahaba.

Na wanapokaribia umri mkubwa dada zao wadogo wanarithi na kuchukua kazi hiyo.

Utamaduni huo umepitishwa kutoka kizazi kimoja hadi chengine kama utamaduni uliokubalika, na wanaume katika familia hizo hawaruhusiwi kutumia fedha zinazoletwa na wasichana hao.

Katika visa vingine baba ama ndugu hutumika kuwatafutia wanaume.

Hata harusi pia hufanywa tofauti katika jamii hizi.

Katika jamii hiyo familia ya bibi harusi ndio inayoitisha fedha nyingi za mahari kitu ambacho ni kinyume nchini humo.

Heena aliandaliwa kutekeleza majukumu yake tangu alipozaliwa kabla ya kuruhusiwa kuwa kahaba.

Nilikuwa na umri wa miaka 15 wakati waliponilazimisha kujiingiza katika kazi hiyo, nililazimika kuwacha mafunzo yangu na kufuata mkondo huo kama walivyofanya mamangu na bibi yangu, aliambia BBC.

Kila siku aliwashughulikia wateja kadhaa kutoka wale wa mashambani hadi matajiri.

Wakati nilipokuwa umri wa miaka 19 niligundua kwamba ninachofanya ni makosa makubwa na kwamba nilikasirika sana.

Je niliamua nini? Je fanilia yangu ingeishi vipi iwapo sina fedha?

Mamangu aliniingiza ndani ya danguro nikiwa na umri wa miaka 14 nikidhania kwamba alikuwa akinipatia kazi.

Jamii ya Bacchara huwa masikini nchini India na huamini wanawake wao kuimarisha hali ya kiuchumi ya familia.

Kulingana na Akasha Chouhan, mshirikishi wa shirika lisilo la kiserikali, thuluthi moja ya wanawake ambao hufanya kazi ya ukahaba ni watoto wadogo.

Jamii ya Bacchara ni ya ufugaji , iliopo katika wilaya tatu za jimbo la Pradesh, katikati ya taifa hilo.

Wengi huishi mashambani ama maeneo yaliopo karibu na barabara maeneo ambayo malori ya mizigo husimama.

Wasichana hao wadogo , wanaojuliakana kama Khilawadis ama wale wanaocheza, huonekana wamekongamana katika makundi madogo madogo peke yao wakisubiri wateja wao.

Kuna maduka madogomadogo barabarani ambapo maajenti wako wapo.

Wao hufanya makubaliano na madereva hao wa malori ambao hulipa kati ya $ 1.45 na US $ 2.80 kwa biashara hiyo kukamilika.

Kulingana na wakaazi , bei nzuri hulipwa mabikira ambayo hugharimu $ 72.

Mtu huyo huyo ambaye anakufanya kahaba na anayeishi katika makaazi jirani ni mume ya mtu na baba ya watoto kadhaa.

Wakati wa mchana kati ya wanaume wanne hadi watano hunitembelea. Usiku sisi hutembelea hoteli ama maeneo yaliopo karibu.

Kila mara tunakuwa na hatari ya kuambukizwa, Heena anaelezea.

Ripoti iliochapishwa na gazti la kitaifa nchini humo , The Hindu 2000 ilisema kuwa sampuli za damu 5,500 ya watu wa jamii hiyo zilifichua kuwa takriban asilimia 15 walikuwa na virusi vya ukimwi.

Baadhi ya wasichana wadogo huishia kupata watoto kutokana na kazi yao ya ukahaba. Heena alipata mtoto aliyemfanya kufanya bidii zaidi.

Kwa mfanyiabishara wa ngono pia inamaanisha kwamba haruhusiwi kuona mtu kutoka kwa jamii unayotoka.

Na hatimaye Heena alifanya juhudi kuondoka katika mfumo wa jamii hiyo kupitia usaidizi wa shirika moja lisilo la kiserikali.

Mumewe wangu alinibaka kila siku: Chanzo cha ndoa za kulazimishwa. Wasichana wanaokubaliana na utamaduni kama huo ndio watakaokuelezea tatizo wanalokumbana nalo.

Kuna vyanzo vingi vya utamaduni huu lakini hakuna vilivyothibitishwa. Sababu mojawapo ni ufukara na ugumu wa kabila hilo kupata fedha.

Lakini sheria inasema nini

Kupendwa kwa watoto wa kiume nchini India kumezua hali ya kutokuwa na usawa kati ya idadi ya wanaume na ile ya wanawake. Lakini tatizo hilo hapa ni kinyume.

Jamii hiyo ina takriban wanachama 33,000 ambao kati yao asilimia 65 ni wanawake, kulingana na Akasha Chouhan.

Sababu moja ya idadi kubwa ya wanawake ni usafirishaji wa wasichana kutoka maeneo mengine hadi katika eneo hilo.

Tumewaokoa wasichana 50 katika maeneo haya katika miezi ya hivi karibuni, alisema majon Kumar Singh afisa wa polisi. Tunampata mtoto wa miaka miwili ambaye tunamuhifadhi.

Kumar Singh anasema kuwa wao huwavamia watoto hao na kuwakamata lakini utamaduni huo ambao upo ndani ya jamii hiyo unaweza kuangamiwa iwapo kutakuwa na hamasa ya kutosha kuhusu tatizo hilo.

Madhya Pradesh , jimbo ambalo jamii hiyo inaishai , hivi majuzi ilipitisha sheria ambayo ilimpiga faini mtu yeyote anayembaka mtoto wa miaka 12 na hukumu ya kifo.

Pia iliongeza muda wa kwenda jela kwa watu wazima wanaoshiriki ngono na wasichana wasiozidi umri wa miaka 18, ikiwa ndio umri wa kutoa idhini nchini India.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii