Tetesi za soka Jumamosi 30.03.2019:Rashford, Costa, Coutinho, Mourinho, Benitez

Rashford Haki miliki ya picha Michael Regan
Image caption Rashford kusalia Manchester United

Manchester United wamefanya mazungumzo na wawakilishi wa Marcus Rashford na wana matumaini mshambuliaji huyo wa England atatia saini mkataba wa miaka mitano na kuondoka na kitita cha £150,000 kwa wiki .(Mail)

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer anataka kumnyakua mshambuliaji wa Juventus Douglas Costa, 28,lakini atakumbana na upinzani wa Manchester City na Paris St-Germain ambao wana nia ya kumchukua mchezaji huyo raia wa Brazil.(Tuttosport, via Express)

Kiungo mchezeshaji wa zamani wa Liverpool Philippe Coutinho amewaambia wachezaji wenzake kuwa anafikiria kuiacha Barcelona katika kipindi hiki cha majira ya joto.Manchester United na Chelsea wanamtolea macho mchezaji huyo.(Express)

Bayern Munich ina mpango wa kumchukua Kocha wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho kuwa mbadala wa Niko Kovac.(Foot Mercato, via Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa Juventus,Douglas Costa

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino amekataa kutoa hakikisho kama atakuwa na kilabu hicho msimu ujao.(Telegraph)

Everton wamemwambia mlinzi Kurt Zouma, anayechezea kwa mkopo kilabu cha Goodison Park akitokea Chelsea, kuwa wanataka kumpa mkataba wa kudumu kuichezea timu hiyo.(Times )

Everton pia inataka kumsajili kwa mkopo kiungo wa kati Andre Gomes, 25 akitokea Barcelona, huku wakitarajiwa kutoa maamuzi kuhusu Phil Jagielka, 36 na Leighton Baines, 34. (Guardian)

Caster Semenya: U.Mataifa wakosoa 'udhalilishaji' wa sheria ya IAAF

Chelsea yampa Hudson-Odoi ushauri

Kocha wa Newcastle Rafael Benitez, anahusishwa na mpango wa kuhamia Super League ya Uchina, anasema alifanya mazungumzo ya awali na Mkurugenzi wa Newcastle Lee Charnley kuhusu kuongeza mkataba.(Sky Sports)

Arsenal imempa ofa mlinda mlango Petr Cech, 36, ya kuwa mwalimu atakapostaafu mwishoni mwa msimu, lakini kuna uwezekano akarejea Stamford Bridge. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jose Mourinho

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino ameonya kuwa uwanja wenye thamani ya pauni bilioni moja si kigezo cha kuwashawishi wachezaji wapya kujiunga na klabu hiyo au kuwafanya wachezaji wakatae kuondoka kwenye klabu.(London Evening Standard)

Winga wa PSV Hirving Lozano ana ndoto za kuhamia Manchester United.(Manchester Evening News)

Seamus Coleman ameweka wazi ndoto zake za kuwa Kocha siku za usoni.(Mail, via Liverpool Echo)

Mada zinazohusiana