Meli yatekwa na wahamiaji,vijana watatu wenye asili ya Guinea na Ivory Coast

Askari wa doria wa Malta wakiwa kwenye meli El Hiblu 1, inayoelezwa kutekwa nyara Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Vijana watatu huenda wakafungwa miaka 30 kwa kosa la kuiteka meli

Vijana wadogo ambao wanaelezwa kuwa wahamiaji haramu wameshtakiwa vsiwa vya Malta baada ya ''kuteka'' meli, tukio linaloelezwa kuwa ni la kigaidi chini ya sheria ya Malta.

Kwa majina ni Abdallah Bari,19 kutoka Guinea, wengine wawili wa umri wa miaka 15 na 16 kutoka Guinea na Ivory Coast.

Vijana wote watatu wamekana mashtaka dhidi yao.Watahukumiwa kifungo cha miaka 30 iwapo watakutwa na hatia.

Meli ya mafuta, Elhilbu 1, ilikua imebeba zaidi ya wahamiaji 100 ambao wote wanashikiliwa na mamlaka ya nchini humo.

Wahamiaji walikua wameokolewa na meli hiyo lakini baadae ikaripotiwa kuwa imevamiwa siku ya Jumatano baada ya kuhofiwa kuwa huenda ikarudi nchini Libya.

Wahamiaji hao walimshurutisha nahodha wa meli kuiongoza meli iende ulaya.

Nchi gani ina wahamiaji wengi?

Basi la shule latekwa na kuteketezwa Italia

Chombo kilichokuwa kikifanya doria kiliisimamisha meli hiyo kuingia maji ya Malta na kikosi maalumu kiliingia ndani ya meli na kuanza kuikagua meli hiyo, Vikosi vya jeshi la Malta vimeeleza katika taarifa yao.

Waziri Mkuu wa Malta Joseph Muscat amesema sheria zote za kimataifa zitafuatwa wakati polisi wakifanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Tukio hilo la karibuni limekuja wakati ambapo Umoja wa Ulaya unasema unamaliza doria za bahari ya mediterranea.EU imesema uamuzi wa kusitisha operesheni ya Sophia kuanzia September umekuja kutokana na ombi la Italia.

Operesheni hiyo ilikusudia kukamata wasafirishaji wa binaadamu na kuokoa wahamiaji wanaotaka kuingia ulaya kwa kutumia boti, maelefu ya maisha ya watu yameokolewa.

Hivi karibuni operesheni ilifanyika kunasa mitandao ya wasafirishaji binaadamu na kurekodiwa kuwepo kwa idadi ndogo ya watu wanaoingia ulaya, baada ya mkataba wa pamoja kati ya Umoja wa ulaya na Libya.

Waziri wa mambo ya ndani wa Italia, Matteo Salvin amelaumu operesheni Sophia kwa kuwapeleka wahamiaji waliookolewa kwenye pwani ya Italia.

Mapema juma hili, alielezea kitendo hicho kuwa ''uharamia wa kwanza kufanywa baharini na wahamiaji'',kwa mujibu wa shirika la habari la Marekani, AP.

Mada zinazohusiana