Changamoto zinazomkabili Zidane Real Madrid

Zinedine Zidani Haki miliki ya picha Getty Images

Miezi 10 tu baada ya kuiambia Real Madrid kwamba: ''Ningependa kuendelea kubaki, lakini kwa sababu hamutaki kunisikiliza ni heri kuondoka.'' Amesema Zinedine Zidane. Zidane amerudi katika kiti moto cha Santiago Bernabeu

Aliondoka baada ya kushinda mataji matatu ya ligi ya vilabu bingwa Ulaya mfululizo na sasa anarudi katika klabu ambayo haina mwelekeo-klabu ambayo haina chochote cha kushindania msimu huu isipokuwa kufuzu katika kombe la vilabu bingwa msimu ujao.

Zidane aliondoka siku 300 na kitu zilizopita akitangaza kuwa baada ya miaka miwili na nusu juu ya uongozi wa timu hiyo ,huo ndio uliokuwa wakati mzuri kwa kila mtu.

Atakuwa kocha wa tatu wa klabu hiyo msimu huu baada ya Julen Lopetegui, ambaye alisimamia timu hiyo hadi 29 Oktoba na Santiago Solari ambaye baada ya wiki moja kila kitu kilikuwa kikiporomoka.

Katika kile kinachoonekana kuwa siku sita mbaya zaidi katika historia, klabu hiyo iliondolewa katika kombe la Copa del Rey na Barcelona wakilazwa 3-0 nyumbani .

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Habari ya Zidani kurejea Real madrid haijamfurahisha Gareth Bale ambaye hapatani za Zidani

Na baadaye kupoteza nafasi iliokuwa imesalia ya kushinda ligi ya La Liga baada ya kupoteza 1-0 dhidi ya Barcelona mbali na kucharazwa 4-1 na klabu ya Ajax katika kömbe la vilabu bingwa wakiwa nyumbani .

Ushindi wa 4-1 dhidi ya klabu ya Real Valladolid siku ya Jumapili haukuweza kutosha kumsaidia Solari na tayari kulikuwa na mpango wa kumuajiri mrithi wake hata kabla ya mech hiyo kuanza.

Zidane aliondoka kwa sababu alihoji kwamba timu hiyo ni lazima iendelee kushinda na kwa hilo kufanyika inahitaji mabadiliko.

Aliendelea : Mimi ni mshindi sipendi kupoteza.Iwapo hakutakuwa na uhakika kama ambavyo ningependelea na kwamba hatutaendelea kushinda sio vyema kuendelea na kuharibu.

Rais wa klabu hiyo Florentino Perez alimuahidi raia huyo wa Ufaransa mahitaji yake yote ili kumvutia ili arudi.

Wazo kwamba alirudi bila hakikisho lolote haliwezekani.

Hatua ambayo ni habari mbaya kwa mchezaji Gareth Bale .Raia huyo wa Wales na Zidane hawapatani .Wakati Bale alipohitaji msaada kwa kuwa watu walidai kwamba mchezo wake umeshuka ,Zidane hakutoa tamko lolote.

Uhusiano wao uliharibika msimu wa 2017-18 ulipokamilika ,huku Bale akiuambia ulimwengu kwamba anafikiria kuhusu hatma yeke mwisho wa fainali ya kömbe la vilabu bingwa msimu uliopita.

Zidane hataki kushirikiana na Bale lakini haitakuwa rahisi kumuondoa katika klabu hiyo. Akikaribia umri wa miaka 30 ni klabu gani itakayolipa zaidi ya Yuro milioni 75 na mshahara wa yuro milioni 12 anazopokea kwa sasa?.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy alijaribu kumrudisha mchezaji huyo katika klabu hiyo kupitia mkopo wa mwaka mmoja na mshahara wa chini wa kila wiki , pendekezo ambalo halikufika kwa Real Madrid huku akijua ni jibu lipi lingetolewa.Kiwango cha mchezo wa Bale kimeshuka.

Anahitaji mtu wa kumpatia motisha ili kuweza kuiinua kiwango cha mchezo wake, lakini Zidane sio mtu wa aina hiyo, lakini iwapo hakuna mtu atakayemnunua , raia huyo wa Ufaransa atalazimika kunoa majembe yake ya ukufunzi ili kushirikiana na mchezaji ambaye ana uwezo wa kushinda mechi licha ya tofauti zao.

Hatua hiyo itakuwa habari nzuri kwa Eden Hazard na habari mbaya kwa upande wa Chelsea .

Hazard ameonyesha hamu ya kutaka kuichezea Real Madrid mbali na kucheza chini ya ukufunzi wa Zidane.

Real Madrid inaweza kumbadilisha Bale na kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, mchezaji wanayemlenga mwisho wa msimu huu, lakini Spurs haiwezi kulipa mshahara wa Bale.

Na kwa sasa hayuko tayari kuupunguza mshahara huo. Huku macho ya Real yakiwalenga kwa muda mrefu wachezaji kama Neymar na Kylian Mbappe, hatua ya PSG kukataa kuwauza wachezaji hao , pamoja na ari ya Zidane kumleta Hazard nihini Uhispania inaweza kuwa mojawapo ya changamoto zinazomkumba kocha huyo mpya.

Mbappe na Neymar wameifungia PSG magoli 49 msimu huu.

Nahodha Sergio Ramos hakushiriki katika mechi ya kufuzu kwa robo fainali dhidi ya Ajax , na baada ya mechi hiyo alijihusisha sana sawa na wachezaji wengine wa Real Madrid usiku huo.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kwa mtu ambaye amekiri kufanya makosa ya makusudi ili apewe kadi katika mkondo wa kwanza ili aweze kushiriki katika mech ya robo fainali ambayo hawakutinga, ilimuonyesha beki huyo kama shujaa wa majanga yalioikumba Real Madrid baada ya mechi hiyo kukamilika.

Hiki ndicho kilichofanyika

Ni kawaida kwa rais wa klabu hiyo Perez kutembelea chumba cha kubadilisha nguo cha wachezaji baada ya mechi za nyumbani kukamilika.

Duru zinaarifu kuwa kilichofuatia kilikuwa matusi dhidi ya wachezaji hao akiwashutumu kwa kukosa kuwa na utaalamu akiwalaumu kwa kile ambacho klabu hiyo inakumbana nacho.

Mchezaji wa pekee aliyejibu alikuwa Ramos .Kile kilichotokea ni matamshi ambayo yaliwashangaza wengi.

Ramos alidaiwa kumwambia rais wa klabu hiyo kwamba iwapo angetaka kutoa lawama zozote kwa hali ya klabu hiyo basi ingekuwa vyema iwapo rais huyo angetazama kioo.

Ramos alikiri kwamba klabu hiyo ilikuwa imeathirika na kwamba badala ya Perez kumtibu mgonjwa ameamua kumuua kabisa.

Perez alijibu kwa kumwambia Ramos kwamba atamuondoa katika klabu hiyo, akijibiwa kwa kuambiwa kwamba 'nipe pesa niondoke'.

Hiyo si mara ya kwanza kwa wawili hao kurushiana cheche za maneno huku ikikumbukwa kwamba Ramos alikuwa anasubiri mkataba wake na hakuna kilichokuwa kikifanyika.

Perez alikuwa ameripotiwa akiwaelezea wakufunzi wengine kwamba atamuondoa Ramos kwa kutompatia kile alichokuwa akihitaji katika mkataba mpya.

Na klabu ya Manchester United ilipokaribia kumsaini , wawili hao walikubali kwamba wanahjitajiana na kandarasi mpya ikawekwa.

Na tangu cheche hizo za maneno kati ya rais na nahodha wake ni mzozo ambao Real Madrid wamemtaka Zidane kuutatua.

Je Perez na wachezaji wanafaa kulaumiwa sawa kwa sawa?

Kwa klabu ambayo inatarajiwa kusajili wachezaji bora duniani, mchezaji wa mwisho bora aliyesajiliwa ni James Rodriguez 2014.

Haki miliki ya picha Getty Images

Itakuwa vyema kuona ni mwelekeo gani Zidane ataipeleka klabu hiyo uwanjani na hata katika soko la uhamisho kwa sababu wachezaji alio nao pia wanafaa kulaumiwa.

Iwapo Perez ni msema kweli basi Zidane atakuwa na uhuru wa kununua wachezaji anaowataka mbali na kuyaondoa majina makubwa.

Isco alionyesha mchezo mzuri chini ya uongozi wa Zidane , lakini klabu hiyo iliunga mkono uamuzi wa Solari dhidi ya mchezaji huyo kufuatia maswala ya nidhamu .

Usimamizi wake wa klabu hiyo umemfanya kuungwa mkono na wachezaji pamoja na kwamba atakuwa na fedha za kuwanunua wachezaji -itamsaidia kuandaa kikosi anachohitaji.

Hatahivyo Real Madrid inahisi kwamba haiwezi kufikia mishahara kama ile ya Manchester City na PSG .

Hatahivyo kandarasi za Adidas na Fly emirates zitawahakikishia yuro milioni 125 kwa mwaka mbali na marekebisho ya ujenzi wa uwanja wa Bernabeu utakaosaidia kuleta yuro milioni 150 kwa mwaka.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii