Utamaduni wa 'gukuna' chini Rwanda ambapo sehemu nyeti hurefushwa
Huwezi kusikiliza tena

Utamaduni wa 'gukuna' nchini Rwanda ambapo sehemu nyeti hurefushwa miongoni mwa wanawake

Wakati nchi nyingi za afrika hufanya mila ya ukeketaji wa wanawake,nchini Rwanda hali ni tofauti,sehemu nyeti haikatwi badala yake hurefushwa hadi kufikia urefu wa kidole cha katikati.

Mila hiyo inafahamika kama 'gukuna' hufanywa na shangazi wa mtoto wa kike au mamake mwenyewe.

Lengo hasa ni kuongeza ashki wakati wa tendo la ndoa.Mila hii imeanza kutoweka kwa vijana wa kizazi kipya hasa sehemu za mijini,Lakini inaonekana kushamiri kwa wanawake ambao hawakuitekeleza wakiwa watoto.