Afrika Kusini: Ramaphosa ashutumu mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni

Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini Haki miliki ya picha AFP

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Afrika Kusini ameitisha mkutano wa dharura na mabalozi kufuatia mashambulizi dhidi ya wageni mjini Durban.

Mapema Jumatatu watu watatu walifariki kufuatia maandamano yanayolenga maduka, mengi ambayo yanamilikiwa na wageni.

Takriban watu 50 walitafuta hifadhi katika kituo kimoja cha polisi wakati kundi moja la vijana wa Afrika wasio na kazi walipowashinikiza kutoka katika majumba yao usiku.

Wageni wanalengwa na watu ambapo wanawashtumu kuchukua kazi zao.

Amesema kuwa ghasia hizo, ambazo zimekuwa zikiwalenga raia wa Malawi na raia wengi wa Afrika katika jimbo la Kwazulu Natal ni swala la kujutia hususan katika mkesha wa siku ya mwezi wa uhuru ambapo taifa hilo linaadhimisha miaka 25 tangu uchaguzi wa kidemokrasia nchini humo.

Wiki iliopita , makumi ya raia walilazimika kutoka katika nyumba zao na waandamanaji waliojawa na hasira ambao pia waliwaibia maduka yao.

Ramaphosa ashutumu ghasia hizo

Wakati huohuo Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameshtumu ghasia za hivi karibuni za mashambulizi dhidi ya wageni na kutoa wito kwa taasisi za kiusalama kuwakamata wanaotekeleza vitendo hivyo.

Amesema kuwa ghasia hizo, ambazo zimekuwa zikiwalenga raia wa Malawi na raia wengi wa Afrika katika jimbo la Kwazulu Natal ni swala la kujutia hususan katika mkesha wa siku ya mwezi wa uhuru ambapo taifa hilo linaadhimisha miaka 25 tangu uchaguzi wa kidemokrasia nchini humo.

Wiki iliopita , makumi ya raia walilazimika kutoka katika nyumba zao na waandamanaji waliojawa na hasira ambao pia waliwaibia maduka yao.

Haki miliki ya picha AFP

''Leo uchumi wetu na faida za jamii yetu zinatokana biashara na uwekezaji kutoka kwa washirika wetu katika bara Afrika na wengi wanaishi hapa nchini Afrika Kusini ambapo wanachamngia pakubwa maenedeleo ya taifa hili. Maendeleo ya Afrika yanatokana na ongezeko la watuna mizigo kutoka eneo moja hadi jingine kati ya mataifa tofauti ili sote tuweze kufaidika.hatutakubali kuwawacha wahalifu kurudisha nyuma hatua zilizopigwa''.

Kulingana na Edgebert Mkoko ambaye ni raia wa Tanzania anayeishi katika jimbo la kwazulu natal hali sio shwari hususan miongoni mwa raia wa Zimbabwe, Malawi na Ethiopia ambao ndio wengi wanaotafuta maisha katika eneo hilo. Mkono anasema kuwa kuna baadhi ya watu wanaodaiwa kuuawa katika eneo hilo.

''Vurugu zilizotokea hapo awali zimeibuka tena na chanzo ni kwamba raia wa kigeni wanaoishi nchini humo wanachukua kazi za raia wa taifa hilo'''.

Anasema kuwa bado hakuna suluhu yoyote iliotolewa na serikali hatua ambayo imewafanya raia wengi wa kigeni kuamua kusalia majumbani.

Anaongezea kuwa hali ngumu kwa raia wengi wa kigeni kwa kuwa wanaishi pamoja na raia wa kipato cha chini.

Mkoko anasema kuwa siku mbili zilizopita raia wengi wa kigeni walijaa katika vituo vingi vya polisi katika mji wa Durban

Waathiriwa

Takriban watu 100 walishambulia maduka ya vyakula siku ya Jumapili usiku na Jumatau alfajiri , wakiiba na kuchoma majumba.

Mwanamke mmoja alifariki wakati alipoanguka kutoka kwa paa la nyumba wakati alipokuwa akiwatoroka waandamanaji hao.

Watu wengine wawili waliuawa kutokana na majeraha ya risasi , baada ya mwenye duka moja kudaiwa kuwapiga risasi.

Siku ya Jumanne wageni walianza kutafuta hifadhi katika misikiti na kituo cha polisi.

Waziri wa mahusiano ya kigeni na ushirikiano Lindiwe Sisulu aliwaagiza maafisa wa polisi kuwakabili watu wanaowashambulia wageni.

''Vitendo vyovyote vya kihuni pamoja na wizi wa mali ya raia wa kigeni hautakubalika na maafisa wa polisi na taasisi za kiusalama zinafaa kuchukua hatua za dharura bila kupendelea upande wowote'', alisema katika taarifa.

Haki miliki ya picha Getty Images

Ameandaa mkutano na wanadiplomasia wa Afrika.

Baadhi ya watu hulalamika kuhusu wageni wanaofanya kazi nchini Afrika Kusini ambapo ukosefu wa ajira uko juu ukiwa asilimia 72 mwisho wa mwaka uliopita.

Mashambulizi dhidi ya wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Afrika sio jambo geni nchini Afrika kusini.

Mwaka 2015, ghasia katika miji ya Johannesburg na Durban zilisababisha mauaji ya watu saba baada ya wahamiaji kuwindwa na kushambuliawa na magenge.

Afrika kusini ilikumbwa na ghasia mbaya zaidi dhidi ya wageni mwaka 2008 wakati ambapo zaidi ya watu 60 waliuawa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii