Gukuna: Utamaduni wa kurefusha sehemu za siri za wanawake nchini Rwanda

Mwanamke na mwanawe nchini Senegal

Huku nchi nyingi za Afrika zinapofanya mila ya ukeketaji wa wanawake,nchini Rwanda hali ni tofauti,sehemu nyeti haikatwi badala yake hurefushwa hadi kufikia urefu wa kidole cha katikati.

Mila hiyo inafahamika kama 'gukuna' hufanywa na shangazi wa mtoto wa kike au mamake mwenyewe.

Lengo hasa ni kuongeza ashki wakati wa tendo la ndoa.

Mila hii imeanza kutoweka kwa vijana wa kizazi kipya hasa sehemu za mijini,

Lakini inaonekana kushamiri kwa wanawake ambao hawakuitekeleza wakiwa watoto

Shangazi ambaye anaishi katika mji wa Rubavu na ambaye hakutaka jina lake kamili litajwe anasema kuwa yeye huwasaidia wanawake na wasichana wanaotaka kurefusha sehemu zao za siri.

Anasema kuwa yeye hutumia dawa ya mimea inayochanganywa na mafuta ya ngombe ambayo hutumiwa na wasichana wa kati ya miaka12 hadi 20.

''Anasema hii ni kazi aliyofanya kwa miaka mingi nchini Rwanda na sasa amepanua soko lake hadi nchi jirani ya Congo ambako anaweza kulipwa hata dolla 100 kwa mtu anayetaka huduma hiyo.

Anasema kwamba kwa wale wanaotekeleza mila hii ya Kinyarwanda makusudio yao ni kuongeza ashki wakati wa tendo la ndoa.

Hatahivyo baadhi ya raia wasiopendelea utamaduni huo wanasema kuwa ndoa nyingi huporomoka kutokana na kutekeleza utamaduni huo.

Wanasema kuwa utamaduni huo una madhara hususan wakati wa kujifungua.

Lakini kulingana na Bwana Mutabazi Leon ambaye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, utamaduni huo hauathiri kivyovyote njia ya uzazi wakati wa kujifungua.

''wakati mwanamke anapojhifungua sisi huangalia njia ya ndani ya uzazi kwa hivyo utamaduni huo hauna athari zozote kwa wanawake wajawazito''.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii