Je athari ya ponografia kwa wanawake ni ipi?

Onyo: taarifa hii inahusu masuala ya ngono tangu mwanzo

Abstract image composition - woman falling, computer screens, purple and bright pink background Haki miliki ya picha BBC/ISTOCK
Image caption Ni mambo machache yanayofahamika kuhusu namna ponografia inavyowaathiri wanawake.

"Nilikuwa na miaka 12 wakati nilipoanza kutazama picha chafu za ngono," anasema Neelam Tailor mwenye umri wa miaka 24.

Hakuwa peke yake - utafiti uliofanywa mnamo 2016 unaashiria kwamba takriban 53% ya watoto walio na umri wa kati ya miaka 11 hadi 16 walitazama picha chafu za ngono katika mitandao.

Licha ya hao ni machache yanayofahamika kuhusu namna ponografia inavyowaathiri wanawake na hakuna utafiti mwingi kuhusu suala hilo.

Kwake Neelam, lilianza kama udaku wa kutaka kujua kuhusu ngono.

Hadithi ya Neelam

Haki miliki ya picha BBC THREE
Image caption Neelam alianza kutazama picha chafu za ngono akiwana umri wa miaka 11

"Nilishangaa sana. Wajua, unaanza kutazama filamu za mapenzi ukiwa mtoto, ambazo watu wanapendana na nono ni jambo la kawaida na sio sua;la la uchafu kutazama...." analiachaia hapo huku akishusha mabega.

Kati ya umri wa miaka 11 na 16, Neelam alitazama ponografia kwa wingi.

Alikuwa akienda chumbani kwake alikokaa akiwa utotoni- Picha za rafiki zake zimetundikwa ukutano, vitabu na hati za kutwalii zimetapakaa sakafuni - afunga mlango na kukaa "kati ya dakika 10 na saa moja" akipekuwa mitandao ya ponografia.

"Sidhani kwamba wazazi wangu waliwahi kujua," anasema.

Kwa wepesi alikabiliana na mshtuko wa awali: " Nadhani ponografia inakuondoshea hisia. Nilifika wakati kwa hakika ambapo nilikuwa sisishutishwi na chochote - alafu unaona uchafu zaidi alafu ulichokiona awali kinakuwa sio kitu, ni kawaida tu."

"Nadhani nililiona kwenye filamu na nikataka kujua zaidi. Pengine nilikuwa na mshawasha mwingi, au pengine ni kubaleghe tu, sijui, lakini nilianza kutafuta katika mitandao filamu zilizo na visa vingi vya ngono."

Alihitimu hatimaye, na kuanza kutazama picha chafu zaidi.

Wakati Neelam alipoanza kufahamu zaidi kuhusu aina tofuati za video zilizopo, alianza kupenda aina maalum ya video hizo.

"Nilianza kutazama video ambapo mwanamke asiye ridhia, pengine anayebembelezwa au mara nyingine hata kuonekana ni kama analazimishwa kushiriki tendo hilo."

"Au ningetafuta zilizo na wanaume wazee na wasichana wadogo. Sijui kwanini lakini kwa umri niliokuwa nao, miaka 13 sidhani kwamba tayari nilikuwana upendeleo maalum wa tendo la ngono - nadhani ushawishi mkubwa ulitokana na nilichokiona."

Haki miliki ya picha BBC THREE

Ponografia na ubongo wa (mwanamume)

Mambo mengi yameandikwa kuhusu suala la athari ya kutazama ponografia kupita kiasi kwa wanaume - na vyombo vya habari na pia wanasayansi.

Mnamo 2016, Angela Gregory, mtaalamu wa akili kuhusu masuala ya ngono aliambia BBC kwamba ponografia inayotazamwa kwa urahisi imechangia kuongezeka kwa idadi ya wanaume walioshauriwa kupokea matibabu kutokana na matatizo ya kuweza kushiriki tendo la ndoa.

Uchambuzi wa Shirika moja la msaada la elimu umeashiria kwamba wakati ponografia inachangia kati ya 2 hadi 5% ya visa vya wanaume kutoweza kushiriki tendo la ndoa katika miaka ya 2000- sasa inadhaniwa kuchangia takriban 30% ya visa hivyo.

Na sio tu kuhusu ufanyaji kazi wa viungo vya mwili: watafiti Marekani wamedai kwamba wanaume wanaotazama picha hizo chafu za ngono wakiwa na umri mdogo huenda wapo katika nafasi kubwa ya kukubali kauli zinazosifia ukubwa au aujasiri wa mwanamume, mfano "mambo huwa mazuri wanaume wakishikilia usukani".

Kwa mtazamo wa Dkt Thaddeus Birchard mtaalamu wa masuala ya tabia kuhusu masuala ya ngono anasema kwa mtazamo wake, huenda wanaume wakavutiwa zaidi na ponografia kwasababu "wanawake wengi hawavutiwi kwa sehemu za mwili".

Athari ya ponografia kwa ubongo kwa mwanamke - wanachosema wanawake?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption "Ponografia ni kiwango kisicho cha kawaida cha uchechemuaji, ambacho hakuna mpenzi anayeweza kuikata hamu yake.

Neelam aliacha kutazama picha chafu za ngono alipotimiza miaka 16, hususan kutokana na athari ya kimwili aliyokuwa akiipata.

"Nilipata mpenzi na nikagundua kwamba sisimkwi kwa ngono," anasema Neelam.

"Nadhani ponografia ni usisimuaji wa mwili wa kiwango kisicho cha kaiwada, hasa kama umefungua kama kompyuta 10 kwa mara amoja unatazama - ni binaadamu gani anayeweza kuishghulikia hamu hiyo?

"Kwa kutambua tofuati ya hisia wakati nikitazama picha za uchafu na wakati nikishiriki ngono kwa uhalisi… niliogopa sana. Nilijiuliza , 'Kwahivyo itanibidi niende chooni kutazama ponografia ili nisisimkwe kila ninapotaka kushiriki tendo la ndoa?'"

Aliacha kuzitazama picha hizo chafu kuanzia wakati huo. "Sidhani naweza kusema kwamba nilikuwa na uraibu, kwasababu niliamua kuacha na nikaacha tu."

Ponografia, vitendo vya ngono na aibu

Haki miliki ya picha BBC THREE / ISTOCK

Dkt Leila Frodsham ni mshauri wa afya ya akina mama na msemaji wa taasisi ya Psychosexual Medicine.

"Nimekuwa nikiwatibu watu kwa miaka 20 na sijawahi kuona mwanamke ambaye anakiri kwamba nina 'tatizo' na ponografia," anasema.

"Kuna utafiti - mmoja unaowashirikisha watu 48 na uliionyesha hakuna tofuati katika kusisimikwa kwa wanawake.

Wengine uliowashirikisha wanawake 200 kutoka eneo la mashariki ya kati, umeonyesha kuwepo athari kwa hamu yao na kusisimkwa kwao ambao unatajwa kama 'kusinywa na ngono'."

Frodsham anasema ponografia inachangia mabadiliko katika ushiriki wa tendo hilo la ngono.

Anadai kwaba katika eneo analofanya kazi , ameshuhudia ongezeko la watu wanaoogua maambukizi ya magonjwa ya zinaa usoni na katika macho - sio katika sehemu za siri - na hili analitaja kutokana na kutazamna picha chafu.

"Ilikuwa aghlabu kushuhdia visa kama hivi miaka 20 iliyopita, lakini sasa vinaongezeka na ni kutokana na 'money shots' [mwanamume kushusha shahawa usoni mwa mwanamke]," anaeleza.

Ana wasiwasi kuhusu ukosefu wa uelewa wa kitabibu kuhusu hali hii: "Inashangaza kwamba tunashuhudia visa vya watu wenye matatizo ya ingono kwa wanaume na wanawake. Na kwa uhalisi ni kwamba wanaanza kutazana pnografia wakiwa na umri mdogo maishani mwao."

"Je ni kutokana na kwamba kuna aibu katika kulizungumzia suala hili, au ni kutokana na kwamba hakuna matatizo yoyote?"

Ngono pasi majutio

Haki miliki ya picha Getty Images

Neelam amekata shauri: "Nilijaribu kutazama tena picha chafu za ponografia miaka ya nyuma, kuona tu nitahisi vipi, lakini sikufurahia kabisa, nimeachana nalo kabisa kwa sasa."

Lakini kwa kukaa na kuzungumza na wanawake tofuati kuhusu hisia zao na suala hilo la kutazama ponografia ni jambo linalosaidia kupanua mitazamo.

Pengine inayoangazia miili tofuati zaidi, hisia tofuati mfano furaha, inayofanyana kutoa hisia ya kwamba ngono au tendo la ndoa sio jambo ovu bali kitu cha kujiburudisha.


*Majina yamebadilishwa

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii