Saluni inayotembea: ''Ni kama Uber'', lakini ni ya kuzunguka

Darren Haki miliki ya picha Other

Kwa Waingerezeza wengi weusi , saluni za kinyozi ni mahala pa kubarizi , kupiga porojo na kukutana na marafiki. Lakini kwa wengine hupoteza sana muda wao mwingi, jambo ambalo lilimfanya vijana wawili kuanzisha mtindo mpya - saluni ya kinyozi inayoendeshwa ambayo unaomba hudumu mapema kwa kutumia programu ya mtandao.

Basi dogo lililochorwa kwa rangi za kuvutia linaendeshwa taratibu kwenye bara bara yenye makazi ya watu eneo la Norwood, kusini mwa London. Kijana mmoja akatoka nje ya bustani akitizama simu yake ya mkononi , akampungia mkono dereva , ambaye aliegesha gari lake kabisa.

Walisalimiana, halafu akasukuma mlango wa basi dogo. Mara kikaonekana kiti cha kinyozi cha rangi ya chuma kinachong'ara, kioo kipana na kifaa cha kukausha nywele( hair dryer) na kikapu kilichojaamikasi ya aina mbali mbali.

Kijana mmoja alikuyekuwa amevalia vazi la kuzuwia uchafu au aproni, akachomeka simu yake kwenye kipaza sauti ili kupata muziki . Dereva ambaye kwa sasa ndiye kinyozi wake anafanyakazi yake katika eneo dogo . Mlango bado umefunguliwa wazi ili kuwezesha mwanga wa jua kuwamulikia.

Mwanamke anayemtembeza mbwa kwenye njia ya wapita njia haachi kugeuka mara kwa mara kuangalia gari hilo kwa kutoamini kile anachokishuhudia.

"Huduma yangu ni kama huduma ya kuwasilisha bidhaa kwa wateja au Uber ya kupeleka chakula kwa wateja, lakini badala yake kuwasilisha chakula , tunawasilisha huduma ya kunyoa nywele ," alieleza Darren Tenkorang, mwenye umri wa miaka 24, mmoja wa waanzilishi wa saluni hiyo kwa jina-Trim-It.

Kwa sasa ana mabasi madogo ya aina hiyo mawili yanayofanya kazi maeneo ya kusini mwa jiji la London .

Darren anaamini kuwa anafanya kitu cha maana.

"Usafi wa mwanamume ni sehemu muhimu sana ya utamaduni wangu," anasema.

Lakini katika basi dogo? Ndio , anasema.

" Watu wa rika yangu kwa ujumla wanathamini mambo yanayofanyika kwa wakati na haraka zaidi ya kila kitu unaona."

Darren amekulia Brixton, kusini mwa London, ambako mama yakealifanya kazi za usafi na baba yake kama mlinda usalama; walikuja kutoka Ghana katika miaka ya 1980 na walikuwa na ndoto yake kuwa mfanyakazi wa benki, wakili au muhasibu.

Chuo kikuu kilikuwa wati wote ni sehemu yake, lakini muda ulipowadia , hakuwa na uhakika ni taaluma ipi ingemfaa.

Ni saluni ya kunyoa nywele iliyomsaidia kuamua.

"Inasikika kama kitu cha ujinga, lakini ukweli kwamba kulikuwa na saluni ya Waafrika na Wacaribean niliyoiona mara moja nilipokuwa nikishuka kwenye kituo cha treni cha Brighton, kutembelea Chuo kikuu cha Sussex, ilinifanya nifikiria mara moja, 'Ninaweza kuwa SAWA hapa , Ninaweza kujihisi kama niko nyumbani,'" Alisema Darren.

Nywele za Waafrika na Wacaribean ni tofauti na nywele za wazungu wa Ulaya na inahitaji utaalamu fulani kuzikata vizuri. Darren hupata matokeo mazuri ya kazi yake kwa kuwa na vinyozi ambao wamebobea kwa kazi hiyo.

"Ninapenda pale vinyozi wa kawaida wanapokiri kuwa hawajui namna kutengeneza nywele zangu ," anasema.

Alisomea Uongozi wa biashara katika Chuo Kikuu cha Sussex, akapata mkataba kazi wa mwaka mmoja katika kampuni ya bima jijini London - kazi ambayo wazazi wake walitaka waifanye.

Lakini alipokuwa pale akagundua kitu fulani kilichomfanya afikirie sana kuhusu maisha yake ya baadae . Anatatizo la ubongo linalosababisha mtu kushindwa kuandika.

Mwanzoni lilikua ni tatizo dogo, lakini Darren akaomba ushauri wa kitaalamu na ugonjwa ukathibitishwa. Alipowaambia wazazi wake, mama yake akazema alifahamu tatizo hilo tangu alipokuwa shule ya msingi lakini hakutaka kusema.

" Alidhani kuwa ningejua ingenirudisha nyuma kimasomo " anasema Darren.

Image caption Alipokuwa kijana mdogo Darren alikuwa ananyolewa nywele kwenye saluni ya kawaida kama hii

Saluni za kinyozi za Waafrika na Wacaribea zinafahamika kuwa mahali panapotupa mazingira ya kijamii na ya kufurahisha - mahali pa kukutana na marafiki.

"Baba yangu alikuwa ananipeleka saluni ya kinyozi asubuhi na tulikua tunakaa huko kwa masaa ," anasema Darren. "Tulikuwa tunatizama soka na mara nyingi alikuwa anakunywa pombe aina Guinness, akiwa ametulia na vijana wake."

Wafariki kwa kupiga 'Selfie'

Darren alifurahia sana nyaka hizo . Lakini alipokuwa mtu mzima alikerwa sana na jinsi walivyokuwa wakifanya kazi taratibu.

"Nilichoka sana kusubiri kwa saa nzima kwa kinyozi hasa katika siku za Ijumaa na Jumamosi," alisema.

Kwa hiyo wazo likamjia la kutumia programu ya mtandao ambayo itawawezesha watu kuomba huduma hiyo mapema katika saluni ya kinyozi kwa muda uliopangwa na katika saluni ya kipekee.

Alifikiri kuwa jambo hili litamvutia kila mmoja si kwa wale wanaotumia saluni za vinyozi wa Waafrika na Wacaribea pekee . Na kweli baadhi ya programu zilikuwa tayari zinatoa huduma sawa na hiyo.

Aliongeza katika muswada wake wazo ambalo kwake lilionekana kuwa ni gumu kutekelezwa. Hatimae aliamua kuwaajiri vinyozi moja kwa moja ambao waliwaendesha wateja katika basi dogo: saluni za kunyoa nywele zinazoendeshwa kwenye magurudumu.

Image caption Darren alikutana na mshirika wa kibiashara Nana Darko alipokuwa katika Chuo kikuu cha Sussex

Darren Trim-It app ilishinda shindano, na akatajwa kama mwanafunzi mjasiliamalimali wa mwaka wa Chuo Kikuu cha Sussex.

Zawadi ilikuwa ni £10,000. Ili kuiwezesha kapuni yake kufanya kazi vema alimuajiri mshindani wake katika shindano , mwanafunzi mwenzake anayeitwa Nana Darko, ambaye kujiamini kwake kulimvutia.

Darren aliahidi kumfanya Nana tajiri. Alikuwa sawa na yeye, kijana mweusi kutoka kusini mwa London aliyekuwa na ndoto za mafanikio.

Ni wakati huo ambapo Darren na Nana walipoamua kujaribu kuanzisha biashara.

Image caption Kris ni kinyozi mwenye ajira ya kudumu akifanya kazi ndani ya basi dogo

Kupitia familia na marafiki waliweza kuchangisha msaada wa pesa za kuanzisha biashara yao na mwezi Februari 2018 basi dogo la kwanza lilikuwa tayari -Basi la kwanza aina ya Ford liliegeshwa nje ya nyumba ya wazazi wake. Eneo la nyuma la basi hiyo lilikuwa limetolewa, ili kulibadilisha kuwa saluni ndogo ya kinyozi , likiwa na genereta ya umeme.

Waliwaajiri vinyozi waliofanya kazi muda wote, wakatengeneza upya app na wakasubiri watu wa kutaka huduma yao.

Haraka sana watu wakaanza kuomba huduma mapema . Kufikia Julai 2018 kulikuwa hakuna nafasi ya wateja wa kunyoa zilikuwa zimejaa.

Taarifa ya huduma zao ilisambaa kwa upande mmoja kutokana na kupata baadhi ya wateja maarufu kama wanamuziki Charlie Sloth na Sneakbo, ambao kwa pamoja wana maelfu ya wafuasi kwenye Instagram na Twitter.

Kama Darren na Nana walivyoazimia , aina ya watu waliotuma maombi ya kunyolewa walikuwa wengi wao ni vijana weusi - watu kama Lewis, kutoka West Norwood.

"Ningekuwa na umri wa miaka 15 au 16, ningefanya kazi ya kinyozi," anasema Lewis. "lakini nina miaka 23, ninafanya kazi ya usimamizi wa mali na nianafanya kibarua , kwa hiyo sina muda wa kwenda saluni na kusubiri muda wangu ufike ."

Anaweza kukosa gumzo kidogo lakini katika saluni ya kawaida ya Waafrika na Wacaribea , lakini kama anahisi anataka kuwa na watu anaweza kuwaalika marafiki wakae ndani ya basi dogo ambakoko kuna benchi dogo la kukaa, alisema

Hadi wiki hii , kuna mabasi madogo matatu ya saluni yanayoendesha shughuli ya kunyoa nywele . Kuongezeka kwa idadi ya watu weusi waliosomea kazi hiyo inamaanisha kuwa bei ya juu kiasi ya pauni 25 ya Trim-It sio kikwazo cha ukuaji wao kibiashara. Lakini kuna wengine.

Haki miliki ya picha Trim-It
Image caption Huduma yake pia imewavutia baadhi ya wateja Wazungu na Waasia

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii