Je unafahamu madhara ya hewa chafu kwa mwili wako?

moshi takataka Haki miliki ya picha CRISTINA ALDEHUELA

Uzinduzi pengine wa kupigiwa upatu unawadia katika mojawapo ya jitihada zenye ujasiri duniani kukabiliana na uchafuzi wa hewa.

Maelfu ya madereva wataanza kutozwa malipo kuingia katikati ya mji mkuu wa Uingereza London katika kujaribu kuzuia magari machafu kuingia katika eneo hilo na kuchangia kupunguza magonjwa na vifo vya mapema.

Hatua hiyo imeidhinishwa wakati wanasayansi wanasema athari ya hewa chafuina hatari zaidi ya ilivyodhaniwa awali.

Lakini katika miongo kadhaa ya nyuma, utafiti umefichua namna gesi kama vile nitrogen dioxide na chembe chembe ndogo, zinazojulikana kama particulate matter au PM, zinaweza kupenya ndani ya mwili zikiwa na hatari ya kusababisha athari ya kudumu.

Image caption picha ya Thermal

Pumu

Athari ya wazi ni kwa namna tunavyopumua - yeyte anayeugua pumu, kwa mfano huenda yumo katika hatari kubwa kwasababu hewa chafu inaweza kusababisha madhara makubwa na pia kuchangia mtu kubanwa na pumu.

"Ilinibidi nikeshe usiku kucha kwasaabu kifua kilinibana vibaya kutokana na kupumua hewa chafu ," anasema Alfie mwenye umri wa miaka 10. " sikuweza kulala na ilimbidi mamangu akae macho na mimi usiku mzima."

"Hewa yote chafu inaweza kuumiza mapafu, ubongo na inaweza kuathiri kila kiungo ndani ya mwili wako," amesema.

Alfie ni mojawapo ya watoto 300 katika mji mkuu wa Uingereza wanaoshiriki katika utafiti maalum.

Utafiti umebaini kwamba watoto wanaozaliwa katika miji inayoshuhudiwa uchafuzi mkubwa wa hewa, mapafu yao hufanya kazi kwa kiasi cha chini kuliko waliozaliwa katika mazingira masafi yasioshuhudia uchafuzi wa hewa katika mazingira.

Haki miliki ya picha SEYLLOU

Changamoto kubwa

Na hewa chafu inaweza kuchochea maatizo mengine ya mfumo wa kupumua kwa binaadamu , ikiwemo hali inayofahamika kama emphysema na bronchitis kali, na inadhaniwa saratani ya mapafu inatokana na hilo pia.

Dkt Ben Barrett wa King's College London, anayeendesha utafiti huo anasema watoto wanaozaliwa katika maeneo yanayoshuhudia uchafuzi mkubwa wa mazingira wanakabiliwa na changamoto kubwa maishani.

Fursa nyengine ya kuwepo madhara inatokea wakati chemchembe ndogo zinapoingia mwilini hdai ndaniya mapafu kufika katika inachojulikana kama alveoli, enoe ambako hewa ya oxygen inasambazwa ndani ya mfumo wa damu.

Imebainishwa kwamba chembechembe hizo za PM2.5 ni ndogo sana kiasa cha kuruhusu kuingia mwilini kwa urahisi na kuingia katika mfumo wa damu na kusambaa katika mwili mzima.

Hatari inayotokana na hili ni pamoja na kuziba mishipa ya damu, kuongeza hatari ya kupatwa na kiharusi, pamoja na magonjwa mengine ya moyo na pia kupata mshtuko wa moyo.

Zaidi ya hayo, kuna uhshidi kwaba chembe chembe hizo zinaweza kufika katika ubongo kwa hiyo watafti wanachunguza athari zinazoweza kuwepo kwa hali kama vile ugonjwa wa kusahau dementia.

Haki miliki ya picha Getty Images

Ushahidi mwilini

Kwa mujibu wa Profesa Jonathan Grigg wa chuo kikuu cha Queen Mary mjini London, mtafiti mkuu katika masuala ya athari za hewa chafu kwa watoto, ushahidi wa madhara tofuati unaongezeka.

"Tuna uhakika mkubwa kwamba hewa chafu inahusika na magonjwa ya kupumua kama pumu, kisukari na na maatizo ya moyo na katika miaka mitano tutakuwa na uhakika zaidi kuhusu hali zaidi kama dementiana kunenepa kupita kiasi."

Eneo jipya la utafiti wetu ni kusaka jibu la kwanini watoto katika maenoe yenye mazingira machafu mara nyingi huzaliwa kabla ya kutimiza muda wao tumboni na huwana uzito mdogo wakilinganishwa na waliozaliwa kwingine.

Utafiti mdogo unaendelea unaochunguza mji wa mtoto au kwa maneno mingine kondo la nyuma ambayo huonekana kuwa na alama nyeusi zinzoonekana kuwa sawa na chembechembe za uchafu zinazopatikana katika seli za mapafu.

Mojawapo ya watafiti waliohusika katika hilo, Norrice Liu, pia wa kutoka chuo kikuu cha Queen Mary mjini London anasema kondo hilo la nyuma linatarajiwa kutoa mazingira salama kwahivyo alama hizo nyeusi zinashangaza kuwepo.

Uwepo wake hatahivyo hauthibitishi uhusiano kati ya watoto kuzaliwa mapema au watoto kuzaliwa na uzani mdogo lakini inaashiria kinachowezekana kuwa ni mfumo fulani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii