Wailimanyang hawana matundu ya kutoa jasho katika ngozi yao

Wailimanyang hawana matundu ya kutoa jasho katika ngozi yao

Ilimanyang ni jamii ndogo ya wakenya wanaopatikana katika kijiji cha Kapua jimbo la Turkana nchini Kenya.

Tofauti na wanadamu wengine, wa’Ilimanyang hawana matundu ya kutoa jasho katika ngozi yao, na wanaishi kwa kutembea na mikebe ya maji ili kujimwagia kwenye miili yao kila mara ili kupooza makali ya joto.

Kwa watoto wa shule, hali ni mbaya hata zaidi, kwani wanalazimika kutoka nje ya madarasa yao mara kwa mara ili kujimwagilia maji.

BBC ilizuru kijiji cha Kapua kuzungumza nao.