Iko wapi nguvu ya muziki uliopendwa mjini Morogoro?

Iko wapi nguvu ya muziki uliopendwa mjini Morogoro?

Mara baada tu ya Uhuru wa Tanzania mnamo mwaka 1962 Tanzania ilijipambanua kama nguli wa burudani Afrika Mashariki kutokana na harakati za kisiasa na mageuzi ya kitamaduni, kuzungumzia hayo Morogoro ndiyo mji uliokuwa kitovu cha burudani, wanamuziki nguli walikita kambi hapo na watu walikuwa wakitoka miji mikuu ijumaa kwenda kufuata burudani na kurejea kazini jumatatu.