Ulimwengu wenye wazee wengi kuliko watoto, kuna madhara gani?

Wazee wakufanya mazoezi Japan Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu duniani wanazeeka upesi

Kwa mara ya kwanza katika Historia,kuna wazee wengi duniani kuliko watoto, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Takwimu zinaonyesha kuwa watu wenye umri wa miaka 65 ni wengi ukilinganisha na wale walio chini ya miaka mitano mwishoni mwa mwaka 2018

Kwa sasa kuna watu takriban milioni 705 wenye miaka zaidi ya 65 duniani, wakati wae wenye umri kati ya miaka 0-4 ni takriban milioni 680.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Idadi ya watoto wanaozaliwa imepungua hasa kwa nchi zilizoendelea

Watoto wachache

Christopher Murray,Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti na tathimini ya masuala ya afya ya Chuo Kikuu cha Washington ameiambia BBC : ''Kutakua na watoto wachache sana na watu wengi sana walio na umri wa miaka zaidi ya 65,hali itakayowia vigumu dunia kuendelea.

''Fikiria kuhusu athari za kisosholojia na kiuchumi kwa jamii yenye watu wenye umri mkubwa wengi kuliko watoto,'' anaeleza.

Mwaka 1960, uwiano wa uzao ulikua karibu watoto watano kwa mwanamke mmoja, kwa mujibu wa Benki ya dunia

Karibu miaka 60 baadae uwiano huo umeongezeka kwa 2.4 tu

Idadi ya wazee

Tatizo la uwepo wa wazee wengi ni kubwa katika nchi zilizoendelea.Kuna kasi ndogo ya kuzaliwa watoto kwa sababu kadhaa ikiwemo sababu za kiuchumi, Idadi vifo vya watoto ni ndogo, njia za kupanga uzazi zinapatikana kwa urahisi na kulea watoto ni gharama.

Katika nchi hizo, wanawake hupata watoto wakiwa na umri mkubwa , hivyo huwafanya kuwa na watoto wachache.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption zaidi ya watu wenye umri wa miaka 65 ni theluthi ya raia wa Japan, wakati huo huo idadi ya watoto wanaozaliwa imepungua

Mazingira mazuri ya maisha yao inamaanisha kuwa watu ''huishi maisha marefu'' kwenye nchi zilizoendelea.Mfano Japan, watu huishi mpaka karibu miaka 84 (umri mkubwa zaidi duniani).

Hali hii imeiogopesha Japan kwa miongo kadhaa, na mwaka jana serikali ilitangaza ongezeko la umri wa kustaafu kutoka miaka 65 mpaka 70.

Ikiwa itapitishwa, wafanyakazi nchini Japan watastaafu mapema kuliko sehemu nyingine yeyote duniani.

Unaweza kutimua mbio kiwa na umri wa miaka 80?

Kwa nini wazee hawa wanapenda kuishi jela?

Hali hii pia inatishia nchi zinazoendelea.Nchini China watoto wa umri wa chini ya miaka mitano ni chini ya asilimia 6 ya watu wote.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jamii za kiafrika huzaa sana lakini zina vifo vingi vya watoto.

Idadi kubwa ya watoto kulinganisha na ubora wa maisha

Nchi za kiafrika ni miongoni mwa nchi ambazo ziko kwenye njia panda kuhusu masuala ya uzazi:Viwango vya uzazi viko juu mno na hakuna uwino kati ya idadi ya watu na ubora, Niger ikiwa moja ya nchi hizo.

Hata hivyo nch hizo hizo zina idadi kubwa ya vifo vya watoto, Niger ikiwa na vifo 85 vya watoto katika kila watoto 1000, idadi kubwa duniani.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanamke mjamzito

Athari za kiuchumi

Kuwa na idadi kubwa ya wazee kuna maana kuwa kuna nguvu kazi ndogo, ambapo kunaweza kusababisha kushuka kwa uchumi wa nchi.

Mwezi Novemba mwaka jana, shirika la fedha duniani (IMF) Iliitahadharisha kuwa uchumi wa Japan unaweza kushuka kiasi cha zaidi ya 25% katika kipindi cha miaka 40 ijayo kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya wazee.

Je,teknolojia inasaidia kupunguza madhara ya kiuchumi ya watu wenye umri mkubwa?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Teknolojia inasaidia kupunguza athari zitokanazo na gharama za wazee

Sera na Siasa

Kuna makubaliano, kuwa serikali zinapaswa kuchukua hatua kupambana na hali hii, na wamekuwa wakijaribu kufanya hivyo.

China ilipitia tena sera yake ya ''mtoto mmoja''mwaka 2015 na mwaka 2018 ilitangaza kuachana na sera hiyo ifikapo mwakani.

Nchini China walizaliwa watoto milioni 15.2 mwaka 2018, idadi ndogo katika kipindi cha zaidi ya miaka 60.

Wasomi nchini China wameeleza kupungua kwa wanawake wenye umri wa kuzaa, na familia kuacha mipango ya kuwa na watoto kwa sababu za kifedha, haswa katika familia zenye wanawake wengi walio wasomi ambao hukataa kuwa walezi wakuu.

Wataalamu wa masuala ya idadi ya watu wanasema kuwa sera ambazo zinazozingatia afya za wazee zinapaswa kutumika kupunguza madhara

Hoja ni kuwa watu walio na afya njema wana uwezo zaidi wa kufanya kazi kwa muda mrefu na nguvu zaidi, hali ambayo itapunguza gharama za matibabu.

''Nchi zenye ushirikishaji wa nguvu kazi kubwa kwa wanawake uchumi wake huwa hauporomoki mara kwa mara kwa sababu nguvu kazi yenye wanawake wengi huwakilisha chombo chenye nguvu cha kupambana na umasikini.

Mada zinazohusiana