Wataalamu wanasema kuna haja ya kutafakari upya usalama mtandaoni

Kinyonga na Faru Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Je tunahitaji kutafakari upya kuhusu suala la usalama mtandaoni?

Mabilioni ya fedha hupotea kila mwaka kutokana na uhalifu mtandaoni na tatizo hilo linaonekana kuendelea kuwa baya zaidi.

Watafiti wa masuala ya teknolojia kutoka Israel wamepiga hatua katika harakati ya kupata suluhisho la kudumu.

Lakini je kuna uwezekano wa kuundwa kwa kompyuta ambayo itawashinda maarifa wadukuzi na wapelelezi?

Jambo muhimu litakalowalemaza wadukuzi, ni kuwafanya wasipate faida, anasma Neatsun Ziv, naibu wa raisi wa shirika la Check Point Security Technologies lililopo mjini Tel Aviv,

"Kwa sasa tunafuatilia makundi 150 ya udukuzi mtandaoni kila wiki, na tumebaini kuwa yanatengeneza dola 100,000 kila wiki," aliiambia BBC.

"Tukifanikiwa kuziba pengo hilo huo bila shaka watapoteza hela na kamwe hawataki kufanya hivyo."

Hii inamaanisha watakua na kibarua kigumu kufikia malengo yao na wamekua wakitafuta kila njia ya kujinufaisha kabla hawajaishiwa na maarifa.

Huu ndio mwongozi maalum wa kukabiliana na makundi ya wahalifu wa mtandaoni.

Vizazi sita vya uvamizi wa kimtandao

Haki miliki ya picha Getty Images

1991: Disc tamba au Floppy discs zilitumiwa kushambulia kompyuta iliyounganishwa nayo.

1994: Wavamizi walifikia mtandao wa ndani ya kampuni na kuiba data

1997: Wadukuzi waliwalaghai wahudumu wa mtandao na kufukia kompyuta zilizo hatarini kudukuliwa.

2006: Wavamizi walianza kutafuta adui wa kushambulia programu zote za kompyuta na kutumia mfumo huo kupenya mitandao au kutuma faili zisizo halali.

2016: Wadukuzi walitumia mchanganyiko wa mbinu zote za uvamizi wa kompyuta kwa wakati mmoja.

2019: Wadukuzi wanaanza udukuzi kwa kuvamia mtandao wa intaneti wa vifaa vyote vilivyounganishwa .

Chanzo: Check Point Software Technologies

Watafiti wanasema muda umewadia kwa mashirika kubadili mfumo wa kukabiliana na wadukuzi.

"Tunahitaji kuimarisha juhudi zetu,"anasema Yuval Danieli, naibu mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa shirika la Morphisec nchini Israel

"Ulimwengu umejikita zaidi katika masuala ya kutafuta suluhisho - na kuwinda kitisho - badala ya kuzuia uvamizi kabla haujafanyika."

Morphisec - ilibuniwa kuokana na utafiti wa uliofanywa na chuo kikuu cha Ben-Gurion - na imeunda kitu kinachofahamika kama "kuimarisha usalama unaolenga kitu maalum".

Ni njia moja ya kuhifadhi data katika kompyuta kwa kuzingatia vigezo ambavyo vitafanya iwe vigumu kuifikia.

Teknolojia ya kampuni hiyo imetumiwa kulinda data ya soko la ubadilishaji fedha la London, shirika la roboti la Yaskawa nchini Japan, mabenki na hoteli.

Yuval Elovici, mkuu wa kitengo cha utafiti wa usalama mtandaoni kitika chuo kikuu cha Ben-Gurion, anaonya kuwa mbinu hiyo pia sio salama kwa 100%.

Haki miliki ya picha Ben-Gurion University
Image caption Yuval Elovici mkuu wa kitengo cha utafiti wa usalama mtandaoni katika chuo kikuu cha Ben-Gurion

"Njia pekee kutunza kompyuta haivamiwi ni kuhakikisha ulinzi wake unairishwawakati wa uundaji wake," anasema Bw. Yuva.

Mfumo huo hata hivyo huenda ukatiliwa shaka na baadhi ya wafanyibiashara wengi.

Mfumo mwingine unaofahamika kama "ushirikiano katika usalama wa mtandao" unaonekana kama njia salama ya kukabiliana na wadukuzi mtandaoni.

Hebu tafaka uwezekano wa mashirika manne kufanya kazi pamoja : Barclays, Microsoft, Google na kampuni ya usalama wa mtandaoni.

Kwa mfano, ikiwa kila mmoja atapeana sehemu ya data kwa kampuni nyingine inamaanisha haitafahamika ni data gani zinalindwa lakini watahifadhi katika mtandao wao.

Ili kufikia habari za faragha kutoka kampuni yoyote wavamizi wanahitaji kudukua mitandao yote minne na kufanya kazi na sehemu ya data iliyokosekana, ilikubani yaliyomo katika faili walizoiba

Haki miliki ya picha Check Point
Image caption Neatsun Ziv anaamini hakuna kompyuta isiyoweza kudukuliwa"

"Ikiwa uwezekano wa kufikia mtandao mmoja ni1%, bala shaka uwezo wa kufikia mitandao minne tofauti ni karibu na 0.00000001%," anaeleza Alon Cohen, muanzilishi wa kampuni ya usalama wa mtandaoni ya nsKnox na mkurugenzi mkuu mtendaji wa kitengo cha teknolojia katika jeshi la Israel.

Anauita mfumo huo "crypto-splitting", na inahusisha kuningiza kila data kama maelfu ya nambari na kisha kuigawanya mara nne kati ya kampuni nne zilizoshirikiana kufanya kazi pamoja.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii