Elizabeth Tioko: Ulemavu wa kusikia haumzuii kuwafunza watoto darasani

Elizabeth Tioko: Ulemavu wa kusikia haumzuii kuwafunza watoto darasani

Unapomkuta darasani akifundisha, utadhani ni mawasiliano ya kawaida darasani kati ya mwalimu na wanafunzi wake lakini mwalimu Elizabeth Tioko wa shule ya msingi ya Wasichana ya Lokichar, Turkana Kaskazini mwa Kenya ana ulemavu wa kusikia. Mwalimu huyu huweza kuelewa wanayosema wanafunzi wake kwa kutazama jinsi midomo yao inavyotamka maneno. Bi Elizabeth anaeleza kwamba alipata ulemavu huo baada ya kudungwa sindano ya Quinine mwaka wa 2007 alipougua ugonjwa wa Malaria kwa muda mrefu.

Kama anavyosema, hali hii haikumzuia kufunza kwani ni kazi ambayo yeye hufurahia kufanya ndiposa ikambidi yeye kujifunza namna ya kusoma matamshi kwenye midomo ya wanafunzi wake.

Mpiga Picha: Faith Sudi