Afrika kusini: Mashambulio ya ubaguzi yanafanyika kwa kiasi gani?

A man from Malawi injured after an attack on foreign workers Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wafanyakazi wa mataifa ya nje wamekuwa wakilengwa Afrika kusini

Katika kipindi cha wa siku chache zilizopita wazururaji wamesababisha ghasi katika mji wa kibiashara nchini Afrika Kusini wa Johannesburg, huku wakichoma moto majumba na kupora mali za watu , nyingi kati ya mali hizo magari na maduka ya wahamiaji . Hii hi mara ya kwanza kwa matukio yanayowalenga wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika kutokea nchini humo.

Kundi la wanaume ambao hawana ajira waliwashambulia wahamiaji kutoka Malawi wanaoishi katika mji wa Durban Afrika kusini mwishoni mwa mwezi Machi.

Ilifuata visa vingine kadhaa katika mji huo katika kipindi cha mwezi huo, jambo lililochangia viongozi kutoka vyama vitatu vikuu kushutumua mashambulio dhidi ya raia wa kigeni.

Kuongezeka kwa ghasia hizo limekuwa suala lililozusha mjadala mkuu katika kamepni kuelekea katika uchaguzi mkuu mwezi mei.

Lakini je mashambulio haya dhidi ya wahamiaji yanafanyika kwa kiasi gani, na je ni kweli yanaongezeka?

Wageni washambuliwa

Serikali ya Afrika kusini haikusanyi data inayodhihirisha mashambulio au tishio dhidi ya raia wa kigeni.

Hatahivyo, taasisi ya uhamiaji The African Centre for Migration & Society (ACMS) imefuatilia mashambulio hayo kote Afrika kusini tangu 1994. Takiwmu hioz zimetokana na taarifa katika vyombo vya habari , pamoja na taarifa kutoka kwa wanaharakati, waathiriwa na waangalizi.

Threats, attacks and killings against foreigners in South Africa

Source: Xenowatch, African Centre for Migration & Society

Inapendekeza mashambulio yaliongezeka mnamo 2008 na kwa mara nyingine 2015.

Mnamo 2008, kulikuwana wimbi la mashambulio nchini dhidi ya wakimbizi na wahamiaji - zaidi ya wtau 60 inaarifiwa waliuawa na maelfu wengine kuachwa bila ya makaazi.

Mnamo 2015, kulishuhudiwa visa kadhaa vya ghasia dhidi ya wasiokuwa raia wa afrika kusini, zaidi katika miji ya Durban na Johannesburg, hali iliyochangia kutumwa kwa jeshi kuzuia ghasia zaidi.

Mnamo Machi serikali iliidhinisha mpango wa kutoa uhamasisho kwa umma na kuimarisha upatakinanaji huduma kwa waathiriwa wa unyanyasaji huo.

Makundi ya kutetea haki za binaadamu yalikaribisha hatua hiyo, lakini yamesema serikali inahitaji kutambua wazi kwamba mashambulio dhidi ya wageni ni ya ubaguzi.

Katika taarifa iliyochapishwa Oktoba, chama kikuu cha upinzani Afrika kusini Democratic Alliance, ilikishutumu chama tawala ANC kwa ilichotaja "donda sugu la ghasia za kibaguzi".

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Waziri wa mambo ya nje, Lindiwe Sisulu, ameomba polisi ichukuwe hatua dhidi ya watu wanaolenga wageni

Wahamiaji wanatoka mataifa gani?

70% ya wageni nchini Afrika kusini wanatoka nchi jirani za Zimbabwe, Msumbiji na Lesotho.

30% ilioyosalia wanatoka Malawi, Uingiereza, Namibia, eSwatini, iliyokuwa inajulikana kama Swaziland, India na mataifa mengine.

Kuna takriban wahamiaji milioni 3.6 nchini humo, msemaji wa idara ya takwimu za tiafa ameiambia BBC, kati ya idadi jumla ya zaidi ya watu milioni 50 nchini.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mashambulio hayo yamechangia kuidhinishwa kampeni tofauti za kukabiliana na hali hiyo

Maeneo mengine yanalingana vipi?

Jimbo la Gauteng unaojumuisha mji mkubwa nchini Johannesburg na mji mkuu Pretoria, una kiwango kikubwa cha ghasia dhidi ya raia wa kigeni, likifuatwa na jimbo la Western Cape, kw amujibu wa ACMS. KwaZulu-Natal, ambako mji wa Durban unapatikana ni la tatu.

Mashambulio yamefanyika zaidi katika miji mikubwa , lakini visa hivyo vimeripotiwa pia katika miji midogo na maeneo ya mashinani .

Ghasia hizo mara nyingi huchochewa na mizozo ya wakaazi, na wahamiaji wakishutumiwa kuchukua nafasi za kazi za raia wa Afrika kusini.

Maduka yanayomilikiwa na wageni yameporwa na kuharibiwa.

South Africa attacks

Xenophobic violence incidents by Province, 1994-2018
Gauteng212
Western Cape111
KwaZulu-Natal67
Limpopo40
Eastern Cape33
Mpumalanga22
North West20
Free State19
Northern Cape5
Source: Xenowatch, African Centre for Migration & Society

Uchumi wa tiafa hilo haujaimarika katika siku za hivi karibuni na viwango rasmi vya ukosefu wa ajira vikinakiliwa kuwa zaidi ya 27% kufikia mwisho wa mwaka jana.

Na kwa ukubwa zaidi, taifa hilo limeorodheshwa kuwana idadi kubwa ya mauaji duniani.

"Chanzo kikuu ni umaskini na chimbuko la enzi za utawlaa wa ubaguzi wa rangi," anasema Sharon Ekambaram, anayeendesha mpango wa wakimbizi na wahamiaji kwa mawakili wa kupigania haki za binaadamu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii