Maandamano Algeria: Raia waandamana licha ya kaimu rais Abdelkader Bensalah kutangazawa

Abdelkader Bensalah, kumrithi rais Abdelaziz Bouteflika Haki miliki ya picha AFP

Bunge la Algeria limemteua spika wa bunge kuu Abdelkader Bensalah, kumrithi rais Abdelaziz Bouteflika ambaye alilazimishwa kustaafu baada ya kuhudumu kwa miaka 20.

Bwana Bensalah atakuwa kaimu rais wakati kipindi cha mpito ambapo uchaguzi mpya utaandaliwa.

Lakini yeye sio maarufu na waandamanaji ambao walikongamana katika maandamano hayo makubwa ambayo yalimngatua mamlakani bwana Bouteflika.

Kwa nini maandamano yamefanyika licha ya tangazo

Wanamchukulia bwana Bensalah kuwa mwandani wa rais huyo aliyeoindolewa madarakani.

Na dakika chache baada ya tangazo la uteuzi wa Bensalah waandamanji walirudi barabarani mjini Algiers.

Abdelaziz Bouteflika alijiuzulu wadhifa wake baada ya miaka 20 kufuatia wiki kadhaa za maandamano nchini mwake.

Tayari alikuwa amefutilia mbali mpango wa kugombea muhula mwingine kutawala kutokana na kukuwa kwa upinzani.

Haki miliki ya picha Getty Images

Bouteflika alitangaza kutowania muhula mwengine

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la nchi hiyo, kiongozi huyo tayari aliondoa mipango yake ya kusaka awamu ya tano madarakani, wakati upinzani dhidi ya serikali yake ukiongezeka.

Jeshi la Algeria ambalo lina nguvu, lilimtaka kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 kutangaza kuwa hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya uongozi.

Abdelaziz Bouteflika alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi, miaka sita iliyopita na tangu hapo mara chache amekuwa akionekana katika sehemu za umma.

Chama tawala na jeshi viliunga kuondolewa kwake madarakani

Chama tawala nchini Algeria FLN kiliunga mkono kuondolewa madarakani kwa rais Abdelaziz Bouteflika, ambaye ametajwa kuwa mgonjwa na hivyobasi kutoweza kuongoza.

Uamuzi huo wa FLN ulijiri siku moja baada ya mkuu wa jeshi nchini humo Luteni Ahmed Gaed Salah kusema kuwa uamuzi wa kikatiba unafaa kufanywa kumuondoa afisini rais huyo.

Bouteflika ambaye yuko chini ya shinikizo kali baadaye alikubali kujiuzulu baada ya marekebisho ya kikatiba kupitishwa.

Awali Abdelaziz Bouteflika, amepeleka mbele uchaguzi wa urais uliotakiwa kufanyika tarehe 8,april na kusema kuwa hatagombea tena,

Nia ya kugombea kwake ilizuia maandamano ya nchi nzima kwa wiki kadhaa sasa.

Ameongoza Algeria kwa miaka 20 sasa, lakini hajaonekana muda mrefu katika maeneo ya wazi , kutokana na ugonjwa wa kiharusi alioupata mwaka 2013.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii