Shinikizo ya kuwa mrembo nchini Bangladesh

Mwanamke wa Bangladesh mwenye uso uliofinikwa na mchoro wa ngozi ya chui. Haki miliki ya picha Habiba Nowrose
Presentational white space

"Kama wanawake sisi hushinikizwa kuonyesha urembo wetu'', kulingana na Habiba Nowrose, mpiga picha mwenye umri wa miaka 29 akiandika makala ya shinikizo ya wanawake wanaotaka kuwa warembo nchini Bangladesh.

''Katika mchakato huo wa kutaka kuwa warembo tunalazimishwa kujivua ,hali ambayo ni ya uchungu mno. Tunajificha hali ya kutoweza kujitambua sisi wenyewe''.

Wanawake hawa katika picha hizi za Habiba wanavutia lakini sura zao hufichwa , wakiwakilisha hasara ya nafsi zao licha ya kwamba wamefanya juhudi za kila aina ili kuwa warembo.

Habiba anataka kuvutia hisia jinsi wanawake wa Bangladesh wanavyotumia kila njia ili kuwafurahisha wengine.

Haki miliki ya picha Habiba Nowrose

Akizungumza na BBC Bengali, Habiba amesema kuwa wazo hilo la msururu wa makala hayo unatokana na yale aliopitia yeye mwenyewe.

Haki miliki ya picha Shams Jerin
Image caption Bi Nowrose anasema kuwa alilazimika kukabiliana na matarajio ya watu wengine.

"Nilipofuzu kutoka chuo kikuu nilpata watu wengi wanatarajia mengi kutoka kwangu . Nilitakiwa kuolewa na kupata mtoto , kupata kazi na mshahara mzuri. Nimeona ikitokea kwa wasichana wengi -wanalazimka kusahau kile wanachotaka maishani''.

Haki miliki ya picha Habiba Nowrose

Katika mwaka wake wa kwanza kama mpiga picha , Habiba alihisi kwamba licha ya kufanya bidii haikutosha.

Iwapo wewe ni mwanamke na unataka kuonyesha kwamba unaweza lazima ufanye bidii mara mbili zaidi ya vile wanavyofanya wanaume.

Hatimaye Habiba alijiona amenaswa: Nilihisi kana kwamba nilikuwa najisahau . Baadaye nilianza kufanya kazi ili kujifurahisha.

Haki miliki ya picha Habiba Nowrose

Takriban miaka sita katika kazi yake kama mpiga picha , Habiba alianzisha makala yake ya 'yaliojificha'.

''Nilianza msururu wa makala haya kama njia ya kukataa niliopitia na kuwanyima watu wengine matarajio yao'', anasema.

Haki miliki ya picha Habiba Nowrose

Wakati Habiba alipoanzisha maonyesho ya picha hizo 2016 mjini Dhaka, anasema kuwa zilipokewa na maswali mengi.

Wanawake wengi walielewa ujumbe wake lakini wanaume walihitaji kulezewa zaidi.

''Wanawake walielewa kazi niliofanya kutokana na uzoefu waliokuwa nao katika shughuli hiyo ya urembo lakini kwa wanaume haikuweza kuwa rahisi kuelewa''.

Haki miliki ya picha Habiba Nowrose

Habiba anasema kwamba hakuna wanawake wengi wapiga picha nchini Bangladesh na hizo ndio miongoni mwa sababu . Lakini mambo yameanza kubadilika .

Haki miliki ya picha Habiba Nowrose

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii