Vijana wanavyokabiliana na 'uhaba' wa kondomu Zanzibar

Kondomu Haki miliki ya picha Getty Images

Mashirika ya kijamii yamekuwa mstari wa mbele katika kampeni mbalimbali za kuhamasisha matumizi ya mipira ya kondom ili kuzua maambukiza ya magonjwa ya zinaa.

Lakini katika baadhi ya maeneo visiwani Zanzibar matumizi ya kondomu si jambo la kawaida.

Kondomu haiuzwi katika maduka ya kawaida, jambo ambao limekua likiwaumisha vichwa wanaharakati wa chama cha watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi visiwani humo.

Kwa mujibu wa Wizara ya afya Zanzibar, maambukizi ya virusi vya Ukimwi yapo chini ya 1% lakini kwa upande wa makundi hatarishi kama vile watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na pamoja na wanawake wanaofanya biashara ya ngono bado maambukizi ni makubwa.

BBC imebaini kuwa changamoto kuu ni upatikanaji wa mipira ya kondomu hasa katika maduka ya kawaida.

''Ishawahi kunitokea'' ,anasema mmoja wa wanawake wanaofanya biashara ya ngono.

''Nataka kondomu lakini sehemu ya kupata hamna, inabidi siku kama hiyo ndio sifanyi kazi'' anasema mwanamke huyo.

Aliongeza kuwa visiwani Zanzibar ukienda kuulizia kundomu watu wanakushangaa sana.

Aliwahi kununua kondomu katika duka la kawaida lakini alipata jibu aambalo lilimuacha na maswali mengi

''Eti wataka kondomu? mimi siuuzi kondomu hapa, wewe dada unanivunjia heshima'', alisema mwanamke huyo.

Hata hivyo kuna badhi ya wakaazi ambao wanasema siku hizi mambo yamebadilika sio kama ilivyokuwa zamani.

Image caption Jamii ya Zanzibar ni ya kihafidhina ambapo matumizi ya kondomu hayakubaliki.

''Sasa hivi kondomu zipo kwa hivyo mtu huwezi kufanya mapenzi kiholela bila ya kutumia kondomu'' mwanamake mwingine aliiambia BBC.

Baadhi ya vijana wanofanya kazi na na kujitolea katika chama cha watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi wamewahi kukumbwa na adha ya upatikanaji wa kondomu.

Wanasema jambo hilo ni tatizo kubwa zaidi kwa vijana vijana wa kawaida.

Kwa kiasi kikubwa jamii ya Wazanzibari wanaona matimizi ya kondomu ni sehemu ya uchochezi wa ngono.

Hata hivyo Tume ya Ukimwi visiwani humo inapania kuja na mkakati ambao utasaidia kutatua suala hilo.

''Kondomu kwetu Zanzibar ni suala ambalo kidogo ni nyeti'' anasema afisa wa Tume hiyo, Siaba Saadati.

Anasema kwenye jamii viwango vya maambukizi ni madogo lakini katika makundi maalum ni makubwa.

''Hapa katikati lazima lazima tuje na mbinu ya kuwakinga watu'' aliongeza Bw. Saadati.

Hata hivyo amekiri kuwa ipo haja ya wao kuja na mkakati ambao utalingana na hali halisi ya mila na desturi ya kizanzibari.

Mbali na kuwa maambukizi ya Ukimwi kuwa chini visiwani Zanzibar bado wadau wa masuala ya afya wanasisitiza juu ya upatikanaji wa uhakika wa kondomu katika maduka na sehemu za wazi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii