Nafasi ya wanawake katika maandamano ya Sudan
Huwezi kusikiliza tena

Maandamano Sudan: Picha hii inaashiria nafasi ya wanawake katika maandamano dhidi ya serikali

Picha hii inayomuonesha mwanamke akiongoza maandamano ya kupinga serikali mjini Khartoum, Sudan imepata umaarufu mkubwa mitandaoni.

Umati wa watu unaonekana ukimshangilia kwa kutumia maneno 'thawra' kumaanisha mageuzi.

Baadhi ya watu wanamuita Kandaka-Jina lililopewa malikia katika Sudan ya kale.

Inakadiriwa kuwa, zaidi ya nusu ya waandamanaji wanaomtaka rais Omar al-Bashir, ang'atuke madarakani ni wanawake.