Ikiwa na wapiga kura milioni 900, uchaguzi ujao wa India utasimamiwa na maafisa takriban milioni 10

Takriban raia milioni 900 wanaweza kupiga kura kwenye uchaguzi huu
Image caption Takriban raia milioni 900 wanaweza kupiga kura kwenye uchaguzi huu

Kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, hakuna kilichobadilika

Wakati wa uchaguzi wa Inda, Maafisa wasimamizi huenda mpaka kwenye hifadhi za msitu wa Gir kwenda kuchukua kura ya mtu mmoja.

Wako takriban watano wakiambatana na Polisi wawili .Hubeba vifaa vya kura, ikiwemo mashine ya kupigia kura ya kielektroniki.

Baada ya safari ndefu, walitengeneza kituo cha muda mfupi kwa ajili ya mwalimu wa dini Bharatdas Darshandas eneo la umbali wa kilometa mbili kutoka nyumbani kwake, kama sheria inavyoeleza

Mpiga kura huyo ambaye ana miaka ya 60, anatunza hekalu ndani ya msitu magharibi mwa jimbo la Gujarat.

''Tulikua watu 45 kwenye hekalu, tukiishi hapa.Tulikua na idadi kubwa ya mahujaji.Baadae mamlaka za misitu zikaanza kuweka mazingira mabaya kwa watu kuishi hapa, hivyo wote wakaondoka, mimi ni mpiga kura pekee niliyebaki,'' aliiambia BBC mwaka 2009.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kampeni za uchaguzi

Ana matumaini ya kuona barabara nzuri katika eneo hio ili mahujaji waweze kutembelea.

''Lakini najisikia vizuri kuwa mamlaka inakuja hapa kuchukua kura yangu.''

India inapiga kura tena mwezi Aprili.Ikiwa na wapiga kura milioni 900 waliojiandikisha, idadi hii itakuwa kubwa kuwahi kushuhudiwa ulimwenguni

Lakini ni kwa namna gani nchi inamudu kuratibu uchaguzi kwa ajili ya watu ambao ni 12% ya idadi ya watu duniani?

Kwa kusimamia kwenye uchaguzi huru na haki, Tume ya uchaguzi inaeleza.

Tume itasimamia uchaguzi kwenye majimbo 29 na mamlaka nyingine za kimaeneo.

Takribani vituo vya kura milioni moja vinaandaliwa, huku vingine vikiwa na mahitaji makubwa

Kwa mfano, kituo katika jimbo la kaskazini mwa India la Himachal Pradesh linaelezwa kuwa halifikiki kwa urahisi likiwa na umbali wa mita 4,440 usawa wa bahari.

Maafisa hulazimika kutembea umbali wa kilommeta 20 kuwafikia wapiga kura, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Migongoni mwao, hubeba mitungi ya oksijeni, mabegi ya kulalia, chakula na kurunzi pia mashine za kupigia kura.

Kwa kutumia Ngamia au helikopta

Namna ambayo wapiga kura hufikiwa ni kinyume cha mategemeo ya wengi.

''Unaweza kuona ni kichekesho lakini njia zote za usafirishaji kutoka za zama za kale kama vile Tembo, Ngamia,Boti,baiskeli,helikopta,treni na ndege hutumika kuwafikia wapiga kura kupitia kwenye majangwa, milima, barabara, misitu, visiwa na maeneo ya pwani.

Image caption Kila mwenye haki ya kupiga kura afikiwe kwa Ngama au hata helkopta

Maafisa karibu milioni 10 watasimamia uchaguzi wa mwaka huu.Kwa taarifa yako tu idadi yao ni karibu sawa na idadi ya watu nchini Sweden!

Inahusisha paredi za vikosi, waangalizi, wapiga picha,wafanyakazi wa serikali na waalimu, pia wasimamizi wauchaguzi.

Hao wote watafanya kazi katika maeneo mbalimbali yaliyochaguliwa kuepuka upendeleo.Lakini wana jambo moja kwa pamoja wamepatiwa mafunzo na wako na ari ya kukabiliana na hali za maeneo mbalimbali.

Udanganyifu wakati wa kura

Maafisa wanaofanya kazi kwenye vituo vya kupigia kura wameandaliwa kuweza kukabiliana na changamoto

Jimbo la Kaskazini la Bihar kwa mfano lina historia ya kuviteka vituo ,hasa pale wafuasi wa chama wanapotumia nguvu kuingia na kupiga kura feki, kwa kutumia majina ya wale waliojiandikisha kupiga kura.

Vitendo hivi huwaogopesha wapiga kura na kuwafanya wasijitokeze, hasa wanawake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tume ya uchaguzi inasema imejizatiti kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika vyema

Tume ya uchaguzi hulishughulikia suala hili kwa kuugawa mchakato huu katika awamu sita au saba. Hatua hii huwawezesha kuvisambaza kvikosi vya usalama kuhakikisha kituo cha kupiga kura kiko salama.

Udanganyifu kwenye mchakato wa kura katika jimbo la Manipur, ulidhibitiwa kwa njia ya kutumia teknolojia ya kutambua sura.

ilipoanza kutumika , mwanamke mmoja alitambulika ''Alikua akipiga kura zaidi ya mara ya sitini,'' Imeelezwa.

Kijiji 'kichafu' kinataka jina jipya

Instagram yaibua mjadala wa ubaguzi

Pamoja na tahadhari kuchukuliwa na matukio ya kuwepo machafuko kwenye uchaguzi wa mwaka 2014, ulioathiri majimbo ya Kashmir, Jharkhand na Assam.

Vikosi vya usalama vinafanya kazi kuhakikisha kuwa hakuna matukio ya namna hiyo kwenye uchaguzi ujao.

Kabla ya wapiga kura kuingia kwenye kituo kuna mambo kadhaa ya kufanyika:

  • Kuzipata na Kukagua mashine za kielektroniki nchi nzima.
  • Kuchagua tarehe muafaka za uchaguzi na kuhakikisha kuwa tarehe hizo haziingiliani na sikukuu ya jamii yoyote, au kipindi cha mitihani au hali mbaya ya hewa.
  • Kuagiza wino wa kutosha wa kuweka kwenye kidole cha mpiga kura kuepuka mtu kupiga kura mara mbili.
  • Alama ya chama cha kila mgombea ambayo wapiga kura wanaweza kuwatambua haraka.
Image caption Alama zinazowakilisha vyama vya siasa

Wazo la kutumia alama lilitolewa kabla ya uchaguzi mkuu wa kwanza(uliofanyika mwezi Oktoba mwaka 1951 mpaka mwezi Februari mwaka 1952) wakati ambapo karibu 84% ya wapiga kura hawakujua kusoma wala kuandika.

Kuhakikisha kuwa uhesabuji wa kura unabaki kuwa wa haki, maafisa hufanya kura za majaribio kabla ya wakati wa kura zenyewe.

Lakini, mara kwa mara, kumekua na mashaka kuhusu mashine za kupiga kura.Upande ambao umekua ukipoteza kwenye uchaguzi, umekua ukidai kuwa mashine zimetumika kuiba kura.

Mamlaka zinazosimamia uchaguzi zimekua zikieleza kuwa mashine za kupigia kura haziwezi kufanyiwa udanganyifu, na iwapo zitafanyiwa udanganyifu ni rahisi kugundua.

Kwa sasa, wanashughulikia mahitaji ya mwisho ya vituo vya kupiga kura, nchi nzima.

Tume ya uchaguzi imeendelea kuamini uwezo wake.

Naibu kamishna wa tume Umesh Sinha anasema ''Mchakato wa uchaguzi utakua mzuri,''

Swali ni je hatua hii italeta watu kujitokeza kwa wingi? au kufanya uchaguzi uwe huru na haki?

Dunia itasubiri mpaka tarehe 23 mwezi Mei.

Mada zinazohusiana