Utawala wa miaka 30 wa Omar al-Bashir Sudan

Rais Bashir aliingia madarakani mwaka 1989 kupitia mapinduzi ya kijeshi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Bashir aliingia madarakani mwaka 1989 kupitia mapinduzi ya kijeshi

Utawala wa rais wa Sudan Omar al-Bashir umegubikwa na mapigano.

Aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 na ameiongoza taifa hilo lililokuwa kubwa zaidi barani Afrika zama hizo hadi mwaka 2011 alipochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.

Alipochukua madaraka, Sudan ilikuwa katika mwaka wa 21 wa mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Kaskazini na Kusini.

Japo serikali yake ilitia saini makubaliano ya kumaliza vita mwaka 2005, vita vingine vilizuk atena - katika eneo la magharibi mwa Darfur.

Bw. Bashir alituhumiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC kwa kupanga uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu katika eneo hilo.

Licha ya ICC kutoa waranti ya kimataifa ya kukamatwa kwake, ameshinda uchaguzi mara mbili mwaka 2010 na 2015, japo vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi uliyopelekea ushindi wake.

Haki miliki ya picha Reuters

Waranti ya kukamatwa kwake kumemfanya awekewe vikwazo vya kimataifa vya usafiri.

Hata hivyo Bw. Bashir amefanya ziara ya kidiplomasia katika mataifa ya Misri Saudi Arabia na Afrika Kusini.

Alilazimika kuondoka ghafla nchini Afrika Kusini mwezi Juni mwaka 2015 baada ya mahakama kuhoji uwepo wake nchini humo na kuamuru akamatwe.

Kabala ya kutwaa uongozi wa Sudan alikua kamanda wa jeshi aliyekua na jukumu la kuongoza oparesheni kusini mwa nchi hiyo dhidi ya kiongozi wa waasi John Garang.

Alipotia saini mkataba wa amani na Garang na kundi lake la Sudan People's Liberation Movement, alilsistiza kuwa makubaliano hayo hayamaanishi kuwa amekubali kushindwa.

"Hatukutia saini mkataba huu baada ya kushindwa, Tumesaini mkataba wakati tukiwa kileleni," alisema.


Tuhuma dhidi ya Omar al-Bashir

Mauaji ya kimbari

  • Kuwaua watu wa jamii ya Fur, Masalit na Zaghawa
  • Kuwasababishia mafadhaiko makubwa ya kimwili na kiakili
  • Kuwaweka katika hali ngumu kwa kuwaharibia makaazi yao

Uhalifu dhidi ya binadamu

  • Mauaji
  • Kumpoteza mtu
  • Kuwahamisha watu kwa nguvu
  • Ubakaji
  • Mateso

Uhalifu wa kivita

  • Kushambulia raia katika jimbo la Darfur
  • Kuiba mali katika miji na vijiji

Lengo lake lilikuwa la kuunganisha Sudan, lakini kufanyika kwa maoni kuhusu kujitenga kwa Sudan Kusini ilifikiwa kama sehemu ya mkataba wa amani.

Mwezi Januari mwaka 2011, 99% ya wapiga kura wa Sudan Kusini waliunga mkono pendekezo la kujitenga na Sudan.

Taifa huru la Sudan Kusini lilibuniwa rasmi miezi sita baadae.

Japo alikubali kujitenga kwa Sudana Kusini, mtazamo wake kuhusu jimbo la Darfur - ambalo lilikumbwa na ghasia kuanzia mwaka 2003 haukubadilika.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ni mambo machache sana yanajulikana kuhusu maisha ya kibinafsi ya kiongozi huyo

Waasi waliyokubali kuweka chini silaha walidai kubaguliwa na serikali.

Hata hivyo alipinga tuhuma ya jamii ya kimataifa kwamba aliunga mkono wanamgambo wa kundi la Janjaweed linalotuhumiwa kwa kutekeleza uhalifu wa kivita dhidi ya jamii ya waafrika weusi katika eneo hilo.

Kwa miaka mingi, Bw. Bashir alipinga hatua ya kupelekwa kwa vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda amani Darfur.

Kuzaliwa kwake

Omar al Bashir alizaliwa mwaka 1944 katika familia ya wakulima kaskazini mwa Sudan, ambayo pia ni sehemu ya ukoo wa ufalme wa Misri.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rasi Bashir alipendelea kuhutubia mikutano ya hadhara badala ya kufanyiwa mahojiano ya moja kwa moja

Ni mwanachama wa Al-Bedairyya Al-Dahmashyya, kutoka kabila la Bedouin.

Alijiunga na jeshi la Misri akiwa kijana mdogo na kupanda ngazi ya uongozi wa jeshi hilo, katika vita dhidi ya Israel mwaka 1973.

Ni mambo machache sana yanajulikana kuhusu maisha ya kibinafsi ya kiongozi huyo wa Sudan.

Hana watoto na alipofikisha miaka ya 50 alioa mke wa pili.

Alimuoa mjane wa Ibrahim Shams al-Din, anayetajwa kuwa shujaa wa wa kaskazini - kama mfano kwa wengine, alisema

Mapigano ya muda mrefu ya wenyewe kwa wenyewe yaliwafanya wengi wa wandani wake wa karibu kuwaoa wajane ambao waume wao waliuawa vitani.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii