Omar al-Bashir: Mapinduzi ya kijeshi yamng'oa mtawala baada ya maandamano

Waziri wa ulinzi Awad Mohamad Ahmed ibn Auf.

Baada ya takriban miaka 30 madarakani , rais wa Sudan Omar al-Bashir ameng'atuliwa madarakani na kutiwa mbaroni kulingana na wazilri wa ulinzi.

Akizungumza katika runinga ya kitaifa , Wawd Ibn Ouf alisema kuwa kuwa jeshi liliamua kusimamia serikali ya mpito ya miaka miwili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.

Pia amesema kuwa hali ya tahadhari ya miezi mitatu pia inatarajia kutangazwa.

Maandamano dhidi ya rais Bashir ambaye ameitawala Sudan tangu mwaka 1989 yamekuwepo kwa miezi kadhaa.

Kundi linalosimamia maandaano hayo mara moja lilikataa taarifa hiyo ya jeshi na kuwaomba raia kuendelea na maandamano nje ya makao makuu ya jeshi.

''Waandamanaji wanataka baraza la raia kuongoza kipindi cha mpito badala ya baraza la kijeshi'', alisema mwandishi mmoja.

''Natangaza kama waziri wa ulinzi kung'atuliwa mamlakani kwa utawala uliopo na kumkamata kiongozi wake katika eneo lililo salama'', alisema bwana Ibn Auf katika taarifa yake.

Eneo alilofichwa bwana Bashir halijulikani.

Bwana Ibn Ouf amesema kuwa taifa hilo limekuwa likidorora kutokana na usimamizi mbaya, ufisadi na ukosefu wa haki, na aliomba msamaha kwa mauaji na ghasia zilizotokea.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wengine walisherehekea Khartoum baada ya tangazo hilo

Alisema kuwa katiba ya Sudan ilikuwa inaahirishwa ,mipaka inafungwa hadi itakapotangazwa tena na kwamba anga ya taifa hilo itafungwa saa 24 .

Huku habari hizo zikitolewa kwa mara ya kwanza , makundi ya watu yalisherehekea nje ya makao makuu ya Khartoum , kuwakumbatia wanajeshi na kupanda juu ya magari ya kijeshi.

Idaya ya ujasusi nchini Sudan imesema kuwa inawaachilia huru wafungwa wote wa kisiasa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamanji dhidi ya serikali wamekuwa wakiwaunga mkono wanajeshi

Bwana Bashir anatafutwa na mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC ambayo inamtuhumu kwa kuandaa uhalifu dhidi ya binadaamu katika eneo la magharibi mwa Sudan jimbo la Darfur.

Hatahivyo haijulikani kile kitakachofanyika kufuatia kukamatwa kwake.

Je mapinduzi hayo yalianzaje?

Mapema alfajiri siku ya Alhamisi , magari ya kijeshi yaliingia mjini Khartoum katika eneo lenye jumba la waziri wa ulinzi , makao makuu ya jeshi na makao ya Omar al Bashir.

Kituo cha Runinga na redio baadaye viliingilia kati vipindi na ujumbe kwamba jeshi litatoa taarifa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Omar al-Bashir amekuwa madarakani tangu 1989

Wakati huohuo, makumi ya maelfu ya waandamanaji walitembea katikati ya mji mkuu wa Khartoum ., wengi wakiimba , 'utawala umeanguka tumeshinda'.

Je waandamanji walifanya nini?

Waandamanaji wa maandamano hayo kwa jina Professionals Association (SPA) walisema kuwa jeshi limetangaza mapinduzi ambayo yatatoa watu na taaisi zilizokataliwa na raia.

Waliwaambia watu kuendelea na maandamano hayo nje ya makao makuu ya Khartoum na kusalia barabarani katika miji yote nchini humo.

''Wale walioharibu taifa hili na kuwaua raia ili kuiba kila tone la damu na jesho ambalo lilitolewa na waandamanaji na kumng'oa madarakani Bashir'', taarifa ilisema.

Omar al Bashir ni mmojawapo wa viongozi waliohudumu kwa muda mrefu duniani

Kundi hilo la SPA lilisema kwamba utawala wowote wa mpito haufai kuwashirikisha watu kutoka kwa utawala wa kiimla uliokuwepo.

Mwanamke ambaye alikuwa nembo ya maandamano hayo pia alipinga tangazo hilo la jeshi.

Je Omar al-Bashir ni nani?

Utawala wa rais wa Sudan Omar al-Bashir umegubikwa na mapigano.

Aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 na ameiongoza taifa hilo lililokuwa kubwa zaidi barani Afrika zama hizo hadi mwaka 2011 alipochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.

Alipochukua madaraka, Sudan ilikuwa katika mwaka wa 21 wa mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Kaskazini na Kusini.

Japo serikali yake ilitia saini makubaliano ya kumaliza vita mwaka 2005, vita vingine vilizuk atena - katika eneo la magharibi mwa Darfur.

Bw. Bashir alituhumiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC kwa kupanga uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu katika eneo hilo.

Licha ya ICC kutoa waranti ya kimataifa ya kukamatwa kwake, ameshinda uchaguzi mara mbili mwaka 2010 na 2015, japo vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi uliyopelekea ushindi wake.

Waranti ya kukamatwa kwake kumemfanya awekewe vikwazo vya kimataifa vya usafiri.

Hata hivyo Bw. Bashir amefanya ziara ya kidiplomasia katika mataifa ya Misri Saudi Arabia na Afrika Kusini.

Alilazimika kuondoka ghafla nchini Afrika Kusini mwezi Juni mwaka 2015 baada ya mahakama kuhoji uwepo wake nchini humo na kuamuru akamatwe.

Kabala ya kutwaa uongozi wa Sudan alikua kamanda wa jeshi aliyekua na jukumu la kuongoza oparesheni kusini mwa nchi hiyo dhidi ya kiongozi wa waasi John Garang.

Alipotia saini mkataba wa amani na Garang na kundi lake la Sudan People's Liberation Movement, alilsistiza kuwa makubaliano hayo hayamaanishi kuwa amekubali kushindwa.

"Hatukutia saini mkataba huu baada ya kushindwa, Tumesaini mkataba wakati tukiwa kileleni," alisema.

uhuma dhidi ya Omar al-Bashir

Mauaji ya kimbari

  • Kuwaua watu wa jamii ya Fur, Masalit na Zaghawa
  • Kuwasababishia mafadhaiko makubwa ya kimwili na kiakili
  • Kuwaweka katika hali ngumu kwa kuwaharibia makaazi yao

Uhalifu dhidi ya binadamu

  • Mauaji
  • Kumpoteza mtu
  • Kuwahamisha watu kwa nguvu
  • Ubakaji
  • Mateso

Uhalifu wa kivita

  • Kushambulia raia katika jimbo la Darfur
  • Kuiba mali katika miji na vijiji

Lengo lake lilikuwa la kuunganisha Sudan, lakini kufanyika kwa maoni kuhusu kujitenga kwa Sudan Kusini ilifikiwa kama sehemu ya mkataba wa amani.

Mwezi Januari mwaka 2011, 99% ya wapiga kura wa Sudan Kusini waliunga mkono pendekezo la kujitenga na Sudan.

Taifa huru la Sudan Kusini lilibuniwa rasmi miezi sita baadae.

Haki miliki ya picha AFP

Japo alikubali kujitenga kwa Sudana Kusini, mtazamo wake kuhusu jimbo la Darfur - ambalo lilikumbwa na ghasia kuanzia mwaka 2003 haukubadilika.

Waasi waliyokubali kuweka chini silaha walidai kubaguliwa na serikali.

Hata hivyo alipinga tuhuma ya jamii ya kimataifa kwamba aliunga mkono wanamgambo wa kundi la Janjaweed linalotuhumiwa kwa kutekeleza uhalifu wa kivita dhidi ya jamii ya waafrika weusi katika eneo hilo.

Kwa miaka mingi, Bw. Bashir alipinga hatua ya kupelekwa kwa vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda amani Darfur.

Kuzaliwa kwake

Haki miliki ya picha Reuters

Omar al Bashir alizaliwa mwaka 1944 katika familia ya wakulima kaskazini mwa Sudan, ambayo pia ni sehemu ya ukoo wa ufalme wa Misri.

Ni mwanachama wa Al-Bedairyya Al-Dahmashyya, kutoka kabila la Bedouin.

Alijiunga na jeshi la Misri akiwa kijana mdogo na kupanda ngazi ya uongozi wa jeshi hilo, katika vita dhidi ya Israel mwaka 1973.

Ni mambo machache sana yanajulikana kuhusu maisha ya kibinafsi ya kiongozi huyo wa Sudan.

Hana watoto na alipofikisha miaka ya 50 alioa mke wa pili.

Alimuoa mjane wa Ibrahim Shams al-Din, anayetajwa kuwa shujaa wa wa kaskazini - kama mfano kwa wengine, alisema

Mapigano ya muda mrefu ya wenyewe kwa wenyewe yaliwafanya wengi wa wandani wake wa karibu kuwaoa wajane ambao waume wao waliuawa vitani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii