Kiongozi wa baraza la kijeshi la mpito nchini Sudan ameapa ''kuung'oa utawala

Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman pia ametangaza mwisho wa kipindi cha tahadhari ya kutotoka nje na kufunguliwa kwa waandamanaji of jailed protesters

Kiongozi wa baraza la kijeshi la mpito nchini Sudan ameapa ''kuung'oa utawala'' siku mbili baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini humo.

Luteni Generali Fattah Abdelrahman ametangaza "kufanya mageuzi katika taasisi za taifa ", katika hotuba yake kwa taifa.

Tangazo lake limekua wakati maandamano ya upinzani dhidi ya maafisa yakiendelea, licha ya kupinduliwa kwa kiongozi wa muda mrefu, Omar al-Bashir.

Waandamanaji wamedai utawala ukabidhiwe kwa kiongozi wa kiraia na wameapa kuendelea kubakia kwenye mitaa ya mji wa Khartoum.

Katika hotuba yake, Jenerali Burhan alitangaza mwisho wa amri ya kutotoka nje usiku , akithibitisha kuachiliwa huru kwa waandamanaji waliokuwa wamefungwana kuvunja serikali za majimbo.

Jeshi li taimarisha "amani, utulivu na usalama" kote Sudan katika kipindi chote cha mpito kilichokwisha tangazwa.

Kitadumu kwa muda wa miaka miwili, alisema hadi uchaguzi utakapoweza kufanyikana kuanzishwa kwa utawala wa kiraia.

Ametoa wito kwa upinzani "kutusaidia kurejesha maisha ya kawaida ", na akaahidi kuwashtaki wale waliowauwa waandamanaji.

Hotuba hiyo inakuja baada ya kujiuzulu kwa mkuu wa majeshi aliyeogopwa Jenerali Salah Goshsaa kadhaa baada ya kiongozi wa mapinduzi mwenyewe -Waziri wa Ulinzi Awad Ibn Auf kujiuzulu

Maelezo ya picha,

Waandamanaji wamekusanyika tena mjini khartoum Jumamosi

Mapema leo Viongozi wa waandamanaji katika mji mkuu wa Sudan Khartoum amewatolea wito wanaowaunga mkono kuendela kuandamana mitaani siku moja baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Wanadai utawala uhamishiwe mikononi mwa raia baada ya jeshi kumg'oa mamlakani kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir, na kumuweka mahabusu

Maelezo ya picha,

Bwana Ibn Auf ameondoka madarakani siku moja baada ya kuwa mkuu wa baraza la jesi

Mkuu wa baraza la Jeshi la Sudani amejiuzulu siku moja baada ya kuongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir yaliyosababishwa na wimbi la maandamano makubwa ya kupinga utawala wake.

Waziri wa ulinzi Awad Ibn Auf alitangaza uamuzi huo kwenye TV, na kumtaja mrithi wake Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan.

Viongozi wa maandamano wanasema hawataondoka mitaani hadi jeshi litakapokabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia.

Kuanguka kwa Bwana Bashir kulifuatia maandamano na vurugu zilizoanza mwezi Disemba mwaka jana ambapo waandamanaji walilalamikia kupanda kwa bei za bidhaa muhimu.

Bwana Ibn Auf alikuw amkuu wa ujasusi katika jeshi wakati wa mzozo wa jimbo la Darfur ulioibuka mwaka 2000. Marekani ilimuwekea vikwazo mwaka 2007.

Kiongozi wa kijeshi ambaye amechukua mamlaka kwa sasa ana cheo cha juu pia kijeshi, lakini kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press rekodi yake ni safi kuliko majenerali wengine wa Sudan .Amesemekana pia kukutana na waandamanaji kusikiliza maoni yao.

Maelezo ya picha,

Luteni Jenerali Burhan anaonekana akizungumza na waandamanaji Ijumaa

Bwana Bashir anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu juu ya mzozo wa Darfur.

hata hivyo baraza la jeshi limekwoishasema kuwa halitampeleka bwana bashir kwenye mahakama hiyo, ambaye anakana mashtaka yote dhidi yake , ingawa anaweza kushtakiwa katika mahakama za Sudan.

Jinsi sakata la hivi karibuni lilivypotokea

Licha ya kung'olewa mamlakani kwa Bwana Bashir siku ya Alhamisi, waandamanaji wamegoma kuondoka mitaani, huku wakiendelea kukita kambi kweny makao makuu ya jeshi mjini Khartoum, wakikaidi amri ya kutoitoka nje iliyowekwa na jeshi.

Maelezo ya picha,

Waandamanaji wameendelea kuwepo kwenye mitaa ya Khartoum usiku kucha

Katika hatua yao ya mwanzo kufuatia maandamano hayo, baraza la kijeshi lilijitokeza na kukanusha kwamba halitaki mamlaka , likiwaambia waandamnaji kuwa wataamua hali ya baadae ya nchi yao, huku jeshi likiiimarisha usalama wa umma.

Saa chache baadae, bwana Ibn Auf akatangaza kuwa anajiuzulu na nafasi yake itachukuliwa na Luteni Jenerali Burhan.

"Ili kuhakikisha kunakuwepo na maelewano ya mfumo wa usalama, na hususani kwa majeshi na kwa kumtegemea Mungu ngoja tuanze njia ya mabadiliko ," alisema.

Waandamanaji walisherehekea kuondoka kwake ghafla lakini Chama cha wasomi wa Sudan , ambacho kimekuwa kikiongoza maandmano, baadae kilitangaza kuwa mgomo wa kuketi mbele ya makao makuu ya jeshi utaendelea.

"Tunaowatolea wito wanajeshi wote kuhakikisha kwamba wanakabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia ," walisema kwenye ukurasa wao wa Facebook.

Aidha walitoa wito wa kuondolewa kwa "maamuzi dhalimu ya viongozi ambao hawawakilishi watu " na kuondolewa kwa "nembo zote za utawala ulioondolewa mamlakani ambao ulihusika katika uhalifu dhidi ya watu".

"Hadi madai haya yatakapotimizwa tuhtaendelea na maandamano yetu ya kuketi chini kwenye makao makuu ya jeshi ," ilisema ripoti ya chama hicho cha wasomi wa Sudan.

Wakati huo huo polisi wamesema kuwa watu wapatao 16 waliuawa kwa risasi katika maandamano ya Alhamisi na Ijumaa.