Afrika kwa picha wiki hii : Tarehe 5-11 Aprili 2019

Baadhi ya picha bora zlizopigwa wiki hii kutoka maeneo mbali mbali ya Afrika na nje ya bara hili:

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Muandamanaji wa Sudan akimbusu mwanajeshi siku ya Alhamisi kabla ya kutangazwa kwamba rais Omar al-Bashir amepinduliwa
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Siku moja kabla muandamanaji maarufu , Alaa Salah, ambaye amepewa jina bandia "Nubian queen", akiongea na umati wa watu mjini Khartoum.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Katika siku hiyo hiyo kaskazini zaidi mwa Afrika, nchini Algeria, muwandamanaji huyu alidai watawala waachie madaraka
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanataka wale walioongoza pamoja na Abdelaziz Bouteflika, aliyejiuzulu wiki iliyopita , waandae uchaguzi ujao.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jumapili, wanariadha wakipita kwenye shamba la maua wakati wa mbio za Rotterdam Marathon nchini Uholanzi Netherlands. Mkenya Marius Kiperem (akiwa nyuma kulia) alishinda mbio hizo, na kuweka rekodi mpya ya mbio hizo
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Katika siku hiyo hiyo nchini Italia, Muethiopia Tebalu Zawude Heyi alishinda mbio za Rome marathon. Waethiopian , walipata medali za fedha na shaba katika mbio za wanaume na wanawake.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Makabiliano ya mieleka wakati wa tamasha la kitamaduni la mieleka Jumapili katika mji mkuu wa Mali ,Bamako.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jumanne mwanamume mmoja wa Morocco akiwa amebarizi kwenye kivuli cha mti, huku mkiambiaji aliyeshiriki mbio za kilomita 250 za Marathon de Sables akipita karibu yake
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tukio la siku sita linalofanana na mbio za Marathon, linalinganishwa na karibu kiwango cha sita cha marathon . Wanariadha hawa wanaoshindana,walipigwa picha Jumatano huku wakikikabiliana na joto ambalo linaweza kufikia kiwango cha nyuzi joto 50
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanamke amevalia sanamu mfano wa simbaalipokuwa akishangilia mechi siku ya Jumamosi katika mji wa Afrika Kusini wa Cape Town kama ishara ya kuhamasisha watu wazuwie kutokomezwa kwa tembo na ngili
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Katika siku hiyo hiyo mjini Cape Town, mashindano ya kusokota bangi yalifanyika kusherehekea kukuakwa sekta ya bangi kwenye tamasha la mmea huo . Matumizi ya bangi miongoni mwa watu wazima katika maeneo maalumu yalihalalishwa mwaka jana nchini Afrika Kusini
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Msanii Muingereza mwenye asili ya Nigeria Yinka Shonibare akiwa katika duka la London la Tate Modern Jumatatu na kitambaa chake katika makaba ya vitabu vya London vilivyofunikwa kwa vitenge vinavyohusishwa na fasheni za Afrika
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel akitoa heshma zake mjini Kigali kwa askari wa Ubelgiji 10 wa kulinda amani walikufa katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alikuwa anashiriki matukio ya maadhinisho ya miaka 25 baada ya mauaji ya kimbari . Katika siku hiyo hiyo katika makumbusho ya mauaji hayo mjini Kigali mwanamke huyu alikuwa akisoma orodha ya majina ya baadhi ya watu zaidi ya 800,000 waliouawa 1994...
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jumapili , ulikuwa usiku wa kuwakumbuka na kuwaombea wanyarwanda waliouawa wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, katika uwanja wa kitaifa wa a night vigil and prayers Amahoro Stadium mjini Kigali...
Haki miliki ya picha AFP
Image caption hata wale ambao walikuwa hawajazaliwa wakati huo waliwakumbuka waliouawa na wakaapa kuwa mauaji hayo yaliyodumu kwa miaka 100 hayatawahi kutokea tena

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii