Tetesi za soka Ulaya Jumapili 14.04.2019:Willian, Alderweireld, Wan-Bissaka, Eriksen, Koulibaly, Joao Felix

Ole Gunnar Solksjaer
Image caption Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solksjaer

Klabu ya Manchester United kumpatia kocha wao Ole Gunnar Solksjaer pauni milioni 200 za usajili. Hiko ndiyo kiwango kikubwa zaidi United kuwahi kutoa. (Sunday Express)

Kiungo Paul Pogba, 26, anatarajiwa kupewa unahodha katika klabu yake ya Manchester United ili kuzima mipango ya kuhamia Real Madrid. (Sunday Mirror)

Manchester United watachuana na mahasimu wao Manchester City katika mbio za kumsajili beki kinda wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England Aaron Wan-Bissaka, 21, mwenye thamani ya pauni milioni 40. (Mail on Sunday)

Miamba hiyo ya Old Trafford club pia ipo tayari kumlipa mshahara mara tatu ya anaopokea sasa kiungo Christian Eriksen, 27, wa Tottenham endapo atakubali kujiunga nao mwishoni mwa msimu.

Image caption Christian Eriksen

Man united pia wanaendelea kumnyemelea beki wa Napoli Kalidou Koulibaly. Beki huyo raia wa Senegal mwenye miaka 27 ana thamani ya pauni milioni 110. (Sunday Express)

Solskjaer: Tutaifunga Barcelona nyumbani kwao

Je Manchester United wataweza kuwazuia Suarez na Messi?

Kiungo wa Arsenal na Uswizi Granit Xhaka, 26, ananyemelewa na miamba ya soka nchini Italia klabu ya Inter Milan.(Sunday Express)

Barcelona wanatazamiwa kujaribu kumsajili tena winga wa Chelsea Willian, 30. Barca waliwahi kupeleka dau la pauni milioni 55 ili kimsajili Mbrazili huyo lakini wakakataliwa. (Sunday Telegraph)

Tottenham wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Celta Vigo na Uruguay Maxi Gomez. Gomez 22- mkataba wake una thamani ya pauni milioni 43. (Mail on Sunday)

Image caption Paulo Dybala wa Juventus

Juventus watalazimika kumuuza mshambuliaji wao Paulo Dybala, 25, ili kuwezesha kupata pauni milioni 86.4 ili wamsajili mshambuliaji wa Benfica Joao Felix, 19. (Tuttosport via Football Italia)

Rais wa Benfica Luis Filipe Vieira wiki iliyopita alikataa dau la pauni milioni 65 kutoka kwa miamba hao wa Italia. (O Jogo - in Portuguese)

Mada zinazohusiana