Mwanamume wa Somalia anayetoa huduma pekee ya ambilansi ya bure

Abdulkadir Abdirahman Adan akiwa ameegamia basi lake la ambilansi Haki miliki ya picha Abdulkadir Abdirahman Adan

Mji mkuu wa Somalia - ni mji ambao milipuko ya mabomu inayouwa hutokea mara kwa mara -una huduma ya ambilansi moja pekee ya bila malipo , ambayo ilianzishwa na Abdulkadir Abdirahman Adan miaka 13 iliyopita.

Aliporejea nchini humo kutoka Pakistan, alipokuwa akisomea udaktari wa meno , akiwa ndio amemaliza shule alishangazwa na ukosefu wa ambilansi katika mji wenye shughuli nyingi wa Mogadisho - na namna watu walivyokuwa wanatumia mikokoteni kuwapeleka wagonjwa hospitalini.

Ni magari hayo machache tu ya kubebea wagonjwa yaliyokuwepo na kujibu simu kutoka hospitali za kibinafsi ambazo huwa tayari zimelipia huduma hiyo.

kwa hiyo haikuchukua muda mrefu baada ya kurejea, Dkt. Dr Adan aliamua kuanzisha huduma ya ambilansi.

"Nilinunua basi dogo, nikalibadilisha na kulitengeneza kiasi cha kuweza kutumiwa na watumiaji wa viti vya walemavu pia ," aliiambia BBC.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aamin sasa ana ambilansi 20

Alianza kwa kutumia basi dogo, kuwachukua majeruhi na wanawake wajawazito hospitali.

Huduma hiyo ilikuwa kubwa kiasi kwamba alibaini kuwa anahitaji kuipanua na ndipo alipoanza kwenda kwenye masoko ya wazi ya jiji na kona za maduka kutafuta watu wanaoweza kumsaidia.

"Niliweza kulishawishi kundi la wajasiliamali kuingilia kati na kununua basi jingine dogo ," anasema.

Wakati huo Dkt. Adan alikuwa mkufunzi katika vyuo vikuu kadhaa mjini humo.

"Niliwaomba wanafunzi iwapo wanapenda kuokoa maisha na kama wangetaka kufanya hivyo watoe dola 1 kwa mwezi ili kusaidia kuwaokoa makaka na madada zetu ," anasema.

Kokote alikoenda , alianza kuwaomba watu kuchangia dola 1 kwa mwezi ili kusaidia shughuli za Aamin Ambulansi.

'Hakupata ufadhili wa serikali'

"Aamin" inamaanisha "amini" kwa lugha ya kisomali - na wakazi wengi wa mji wa Mogadishu wanahisi kuwa ameishi kama jina lake katika jamii iliyoshindwa kuhudumiwa na wanasiasa wake.

Leo Aamin Ambulance, inayoendeshwa kwa misaada ya ufadhili , inawahudumu 35. Wengi miongoni mwao ni wafanyakazi wa kujitolea na wanafunzi, anasema Dkt. Adan.

Wahudumu wa kujitolea hawalipwimshahara bali wanalipiwa gharama zao , kama vile usafiri.

Huduma hiyo sasa ina mabasi madogo ya ambilansi 20 na dereva wa kila basi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aamin Ambulance ilisaidia wakati wa mashambulio la wanamgambo mwezi Oktoba 2017 ambapo watu zaidi ya watu 580 waliuawa

"Tunaendesha shughuli zetu kwa misaada. Hatupokei msaada wowote kutoka kwa serikali''.

" Zamani kidogo , tuliiomba ofisi ya meya wa Mogadishu kama wanaweza kutusaidia kutupa walau lita 10 tu za mafuta kwa siku, lakini bado tunasubiri kupata jibu ."

'Baadhi ya wasomali ni watu warimu sana'

lakini Dkt. Adan ameweza kupata uungaji mkono kiasi kutoka kwa Umoja wa Mataifa.

"Shirika la Afya Duniani( WHO) walituletea magari mawili . Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) lilitoa msaada wa simu za mawasiliano ," anasema Aden mwenye umri wa miaka 45.

"Tulinunua magari ya ambilance yaliyotumiwa Dubai kutoka Dubai na yakaletwa hadi hapa. Hivi karibuni , ubalozi wa Uingereza mjini Mogadishu uliandaa mbii za nusu marathon kwa ajili ya kuchangisha fedha za huduma yetu.

Kuchangisha pesa inaweza kuwa kazi ngumu, kwasababu inawafanya wakabiliane na maafisa wa jiji ambao hivi karibuni walipiga marufuku magari ya ambilansi ya Aamin Ambulance kufika maeneo ya mashambulio.

Tatizo linaonekana ni kuwa serikali inahofu juu ya kutangazwa kwa idadi ya waathiriwa wa mashambulio ya mabomu yanayofanywa na wanamgambo wa kiislamu - mara kwa mara Aamin Ambulancehuwajulisha waandishi wa habari taarifa za kimatibabu walizoshuhudia kupitia mitandao ya habari ya kijamii kadri kadri wanavyozishuhudia.

Marufuku hiyo iliwakera baadhi wakati iliporitiwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Idhaa ya Kisomali ya BBC kwenye ambapo watu waliilaumu serikali kwa "kusitisha msaada".

Lakini Dkt. Adan alijaribu kutoonyesha athari za marufuku hiyo.

"Nilizungumza na kamishina wa polisi ambaye aliweka marufuku hiyo, lakini alituambia tuwafahamishe ni lini tunafanya shughuli za dharura . Haturuhusiwi kuzungumza na waandishi wa habari au kuzungumzia juu ya idaidi ya miili ya watu.

Huku msemaji wa mamlaka ya kikanda , Salah Hassan Omar, aliiambia BBC kuwa suala zima halijaeleweka na kwamba zaidi kinacholengwa ni kuangalia ni " vipi tunaweza kufanya kazi bora kwa pamoja ".

kwa Dkt Adan, pingamizi za aina hiyo zinaweza kupatiwa suluhu kwasababu ameridhishwa na ukarimu alioushuhudia tangu alipoanza huduma ya ambilansi.

"Kila mtu katika maisha haya ana sababu na maana zaidi kwangu ni maisha ya binadamuna ndicho kinachotia msukumo wa kutoa huduma hii," anasema.

Image caption Muhudumu anayepokea siku saa 18 kwa siku na kutuma magari ya ambilansi kwenye maeneo ya tukio

"Wasomali ni watu wakarimu sana hataka kama hawana kitu. Nchi yetu imekuwa katika mzozo kwa miaka 30 na sasa shughuli zinaendelea kutokana na msaada kutoka nchi za nje.

" Nchi yetu imekuwa ikiendeshwa kutokana na ukarimu na utashi mwema wa Wasomali wanaoishi katika mataifa ya kigeni kwa miongo.

"Aamin ni matokeo ya juhudi za pamoja za jamii - imetubidi tuchukue usukani kwa ajili ya kuboresha maisha ya Wasomali wenzetu."

'Sisi si wanasiasa'

Ingawa mji wa Mogadishu umegonga vichwa vya habari kwa taarifa za mashambulio yanayofanywa na wanamgambu wa kundi la al-Shabab, huduma za Aamin Ambulance hazikuanzishwa kutokana na haja ya kuwasaidia waathiriwa wa mashambulio ya aina hii.

Bwana Adan anasema magari yake ya ambilansi huenda kule ambako yanahitajika, iwe kumsaidia mtoto mdogo, mwanamke mwenye uchungu wa kujifungua au mzee anayehitaji usaidizi.

"Kusema ukweli tunamsaidia yeyote anayehitaji msaada wetu- tuna madaktarina wauguzi wako tayari ," anasema.

kwa siku zijazo, Dkt. Aden anaimani Somalia ambayo hakuna mtu atakayekufa kwa kushindwa kupata msaada wa matibabu anapouhitaji.

Angependa kuona huduma za Aamin Ambilansi zikipanuka kote nchini.

Huenda ikaonekana kuwa ndoto isiyoweza kutimia kwani al Shabab bado wanadhibiti maeneo mengi ya vijijini- lakini Dkt Adan hana chochote zaidi ya lengo la kufanikisha hilo.

Na al-Shabab, wanaofahamika kwa kudai pesa za ulinzi kutoka kwa wafanyabiashara wengi wa kisomali - hata Mjini Mogadishu ambako walifukuzwa mwaka 2011 hawaonekani kusumbua ambilansi za Adan.

"hatufanyi biashara, hatupati faida na sisi si wanasiasa. Sioni chochote ambacho al-Shabab wangetaka kutoka kwetu," anasema Dkt. Adan.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii