Waliozaliwa na jinsia mbili 'kutambuliwa' Kenya

Apostle Darlan Rukih is one of just a handful of Kenyans who publicly identifies as intersex
Image caption Mhubiri Darlan Rukih ni moja wa Wakenya wachache waliyojitokeza hadharani kusema kuwa alizaliwa na jinsia mbili

Watu waliozaliwa na jinsia mbili nchini Kenya wana kila sababu ya kusherehekea.

Hii ni baada ya Jopokazi lililobuniwa na serikali ya Kenya kuchunguza sera na sheria zilizopo kuhusu watu wenye maumbile hayo kupendekeza watambuliwe kama "jinsia ya tatu".

Jopo hilo pia linapendekeza jinsia ya watu hao ijumuishwe katika stakabadhi rasmi na vile vile washirikishwe katika sensa ya kuhesabu watu.

Mahuntha huwa na hisia ya jinsia ya kiume na ya kike, hali ambayo hujitokeza wakati wa kuzaliwa au baadae maishani.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu waliozaliwa na jinsia mbili ni kati ya 0.05-1.7% duniani.

Ikizingatiwa kuwa idadi ya watu nchini Kenya ni karibu milioni 48, hii inamaanisha kati ya watu 24,000 na 800,000 huenda wamezaliwa na jinsia mbili nchini humo.

Kwa muda mrefu wanaharakati wa kutetea haki wamekua wakilalamikia kubaguliwa kwa watu hao kwasababu hawajatambuliwa rasmi na kwamba ipo haja ya wao kupewa utunzi maalum wa kimatibabu.

Ripoti iliyotolewa mapema jumatatu inakuja baada ya mashauriano ya karibu miaka miwili.

Jopo hilo pia limependekeza sheria ifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kimsingi ya watu wenye uhuntha inalindwa na kuheshimiwa.

Huwezi kusikiliza tena
Darlan Rukih: Nilibaguliwa kwa kuwa na jinsia mbili

Ripoti ya Jopokazi hilo la Kenya inasema kuwa mataifa ya Afrika Kusini, Zimbabwe na Uganda ndio mataifa pekee ya Afrika ambayo yamejaribu kuwatambua watu waliozaliwa na jinsia mbili.

Mapendekezo ya Jopokazi hilo yakiidhinishwa kuwa sheria, Kenya itakua taifa la kwanza la Afrika kuwatambua mahuntha kisheria.

Ujerumani, Austria, Australia, New Zealand, Malta, India na Canada zote zimeidhinisha hatua zitakazoangaia masuala yanayowakabili wanainchi wao waliozaliwa na jinsia mbili.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii