Kanisa la Notre-Dame: Mamilioni ya Euro yaahidiwa kulijenga kanisa kongwe Ufaransa

Flames on the roof of the Notre-Dame cathedral in Paris, France, 15 April 2019 Haki miliki ya picha EPA

Picha za mwanzo za ndani ya kanisa kongwe la Notre-Dame baada ya moto zimepatikana na kuonesha kuna baadhi ya maeneo ya kanisa hilo hayajaungua.

Baadhi ya maeneo muhimu ambayo hayajaunguzwa katika mkasa huo ni madhabahu na msalaba, mimbari pamoja na baadhi ya mabenchi.

Maafisa wa zima moto walifanikiwa kuliokoa jengo hilo la historia lenye miaka 850 lakini paa na mnara wa jengo hilo yameanguka.

Moto huo ulidhibitiwa saa tisa baada ya kuanza, na kuzimwa kabisa baada ya saa 16.

Chanzo chake hakijajulikana lakini maafisa wanasema huenda ukahusishwa na ukarabati mkubwa unaoendelea.

Ofisi ya mwendesha mashtaka imesema inachunguza mkasa huo kama ajli kwa sasa. Afisa mmoja wa zima moto alijeruhiwa kiasi wakati akikabiliana na moto huo, kamanda Jean-Claude Gallet ameiambia televisheni ya BFM.

Rais wa Ufaransa ameahidi usaidizi wa kimataifa katika kulijenga upya kanisa kongwe.

Tayari mamilioni ya Dola yameahidiwa na watu mbali mbali duniani ili kusaidia ukarabati wa kanisa hilo.

Bilionea François-Henri Pinault, ambaye ni mwenyekiti wa wa kundi la makampuni ya Kering ambayo inamiliki chapa za fasheni maarufu za Gucci na Yves Saint Laurent ameahidi kutoa dola milioni 113 ili kudhamini ujenzi wa kanisa hilo, shirika la habari la AFP linaripoti.

Bilionea Bernard Arnault na familia yake wanaomiliki kampuni ya LVMH - inayotambulika kwa chapa za Louis Vuitton na Sephora - wameahidi kutoa Euro milioni 200, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Shirika la kubwa la mafuta la Ufaransa, Total, pioa limeahidi kutoa Euro milioni 100.

Nini kilichofanyika?

Moto mkubwa ulizuka katika kanisa hilo kongwe la Notre-Dame mjini Paris Ufaransa mwendo wa saa kumi na mbili na nusu kwa saa ya huko - jengo ambalo ni moja ya makanisa maarufu na linalotembelewa na idadi kubwa ya watalii kutoka pande mbali mbali duniani kila mwaka.

Sehemu kubwa ya paa la majengo ya kanisa hilo yameteketezwa na moto huku mwingine ukifanikiwa kuzimwa katika minara miwili ya kengele.

Wazima moto wanafanya kila juhudi kuokoa vito vya thamani vilivyoko ndani kanisa hilo na pia kuzuia mnara wa upande wa kaskazini kutoporomoka.

Maelfu ya watu wamekusanyika katika barabara zilizo karibu na kanisa hilo kushuhudia mkasa huo wakiwa kimya.

Baadhi yao walionekana wakidondokwa na machozi, huku wengine wakiimba nyimbo za sifa na kuomomba Mungu.

Haki miliki ya picha Reuters

Makanisa kadha nchini Ufarasa yamekua yakipiga kengele kuashiria uharibifu wa moto huo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron,ambaye alifika katika eneo la tukio amesema mawazo yake yako na "waumini wote wa kanisa katoliki na wafaransa wote kwa ujumla."

"Sawa na watu wengine nchini , nimesikitika sana kuona sehemu ya maisha yetu ya kila siku ikiteketea."

Bw. Macron awali alifutilia mbali hutuba mmuhimu kwa taifa kufuatia moto huo, alisema afisa wa Élysée Palace.

Msemaji wa kanisa hilo pia amekiri kuwa sehemu kubwa imeteketea na bado inaendelea "kuteketea".

Interactive Notre-Dame cathedral fire

After

Image of Notre Dame with the tower missing

Before

Image of Notre Dame with the tower on fire

Mwanhistoria Camille Pascalameliambia shirika la habari lla Ufaransa BFMTV kwamba moto umeharibu ''turathi ya kitaifa"

"Kanisa hili limedumu Paris kwa takribani miaka 800 ", alisema.

"Matukio ya furaha na ya kusikitisha kwa karne kadhaa yamekua yakiadhimishwa kupitia mlio wa kengele za Notre Dame.

"Tunasikitishwa na kile kilichotokea na kile tunachojionea".

Meya wa jiji la Paris, Anne Hidalgo ametoa wito kwa wakaazi kuheshimu mipaka iliyowekwa na maafisa wa zima motoili kuwahakikishia usalam wao.

"Kuna kazi nyingi inayoendelea ndani ...hili ni janga kubwa," aliwaambia wanahabari.

Nembo ya Taifa

Uchambuzi wa Henri Astier, wa BBC

Hakuna eneo lingine linalowakilisha Ufaransa kama Notre-Dame, likifuatiwa na nembo nyingine ya kitafa ambayo ni , mnara wa Eiffel Tower

Notre-Dame limesimama wima juu ya mji wa Paris tangu miaka ya 1200.

Mara ya mwisho kanisa hilo liliharibiwa ni wakati wa mageuzi ya Ufaransa

Limeponea vita kuu viwili vya dunia bila kupata hata alama ya kukwaruzwa.

Kwa wafaransa wliyoshuhudia jengo hilo likiteketea ilikua sawa na kuona taifa likichomeka na kuanguka kwa baaa lake ilikua majonzi makubwa kwao

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kanisa hilo hutembelewa na mamilioni ya watu kila mwaka

"Nina marafiki wengi wanaoishi ng'ambo na kila wakati wanapokuja hapa nawaambia watembeleeNotre-Dame,"mmoja wa walioshuhudia mkasa huo Samantha Silva aliliambia shirika la habari la Reuters.

"Nimezuru kanisa hili maranyingi sana, lakini jengo hili halitakua sawa tena. Lilikua nembo halisi ya mji wa Paris."

Rais wa Marekani Donald Trump amependekeza"magari maalum ya kuzima moto" yatumiwe kuuzima moto huo.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amejitolea kuwsaidia watu wa Ufaransa, na kulitaja Notre-Dame kama "nembo ya Ufaransa na utamaduni wa Ulaya".

"Najumuika na wananchi wa Ufaransa pamoja na maafisa wa kutoa huduma za dharura katika harakati ya kuuzima moto huo mkumba kanisa kongwe la Notre-Dame", aliandika katika mtandao wake wa Twitter Waziri mkuu wa Uingereza Bi Theresa May

Makao makuu ya Vatican imesema kuwa taarifa ya mkasa huo wa moto imewashutia na kuwaacha na majonzi makubwa," na kuongeza kuwa inawaombea Mungu huduma ya zima Moto ya Ufaransaa

The Notre-Dame cathedral, ambalo umaarufu wake huwavuvia maelfu ya watalii kila mwaka, lilikua likifanyiwa ukarabati baada ya nyufa zake kupasuka na kuzua hofu huenda jengo hilo likawa dhaifu.

Mwak jana, kanisa katoliki liliomba msaada Ufaransa kufanyia ukarabati jengo la kanisa hilo la zamani.


Maelezo kuhusu Notre-Dame

  • Kanisa hilo hupokea karibu wageni milioni 13 kila mwaka, idadi ambao ni kubwa kuliko watalii wanaozuru Eiffel Tower
  • Lilijengwa katika karne ya 12 na 13 na limekuwa likifanyiwa ukarabati mkubwa.
  • Sanamu kadhaa ziliondolewa kanisani hapo ili kuruhusu ukarabati wake.
  • Palaa la lanisa hilo lililoteketezwa na moto lilikua limetengenezwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mbao

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii