Kasisi ahamishwa kituo cha kazi baada ya mke wake kutenda 'dhambi' ya kushiriki 'Umiss'

Oskana Zotova akishiriki michuano ya ulimbwende Haki miliki ya picha Yana Terekhova
Image caption Picha za Oksana Zotova zimesababisha hasira kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii

Kasisi wa madhehebu ya Orthodox katika mji wa Urals amebadilishwa kituo cha kazi na kupelekwa kijijini kama adhabu baada ya mke wake kushiriki maonesho ya ulimbwende wakati wa Kwaresima.

Oksana Zotova, anayemiliki saluni ya urembo katika mji wa Magnitogorsk, alishinda kuwa mlimwende aliyevutia zaidi, na kusababisha kukosolewa baada ya habari za mitandaoni kubainisha kuwa ni mume wa Kasisi.

Viongozi wa kanisa walipopata taarifa hizo, Sergei Zotov papo hapo alihamishwa kutoka Magnitogorsk na kupelekwa kwenue kijiji cha Fershampenuaz,umbali wa kilometa 65 kutoka mji aliokua akifanyia kazi, wenye idadi ya watu 4000.

Dayosisi ya Magnitogorsk haikufurahishwa na vitendo vya mke wa Sergei.

Kiongozi wa makasisi Feodor Saprykin, aliyekua mwenyekiti wa mahakama ya dayosisi, alisema kuwa ''Ni dhambi kubwa pale mke wa Kasisi anapojionyesha mbele za watu kwenye maonyesho.''

Alitoa hukumu kuwa Sergei Zotov hatatoka huko mpaka mkewe atakapotubu''.

Ni aina gani ya Kasisi kama hawezi kuidhibiti familia yake mwenyewe? aliuliza. ''Atawezaje kuongoza waumini?''

'Tabia isiyokubalika'

Haki miliki ya picha PoChel.ru
Image caption Kituo cha kazi cha Sergei Zotov

Mtandao wa kijamii uliotoa taarifa hizo pia ulidai kuwa hii si mara ya kwanza kwa mke wa kasisi ''kufanya vitendo hivyo vya kuchukiza''.

Mchungaji Lev Baklitsky wa Dayosisi ya Magnitogorsk amethibitisha kuwa Bibi Zotova aliweka picha zake akiwa na mavazi ya kuogolea na kuwa alifuta picha hizo baada ya kuambiwa hivyo.

Amesema tabia hii ''Bila shaka haikubaliki'' na kuthibitisha kuwa uhamisho wa Kasisi Zotov ni hatua ya muda mfupi,ili ajirekebishe''.

Kwa upande wake Sergei amekiri kufanya makosa na kueleza kuwa kuhamishwa kwake ni ''adhabu kali''.

Lakini alilalamika kuwa mke wake alipokea ujumbe wa kudhalilisha kwenye mitandao ya kijamii.

Tutalijenga upya kanisa la Notre-Dame, asema Macron

Wafunguka kuhusu unyanyasaji wa kingoni katika kanisa katoliki

'Ni watu wa kawaida'

Taarifa hiyo ilisambaa nchini Urusi, ikisambaa kwenye vyombo mbalimbali na majukwaa mbalimbali ya mitandaoni.

Baadhi ya watumiaji hawakufurahishwa na vitendo vya kasisi na mkewe. ''Haya ndio yale unayopaswa kujua kuhusu wake wa makasisi.Na makasisi wenyewe pia.Wanahubiri jambo moja na kufanya jambo jingine,'' Alisema mtu mmoja.

Lakini watu wengine wengi walikosoa uamuzi wa Kanisa na kuwaunga mkono wenza hao.

''Kwa nini asifurahie maisha yake? Kuna watu bado wanaamini kuwa makasisi ni watu safi? Ni watu wa kawaida wenye kazi nzuri,'' mtu mmoja aliuliza kwenye taarifa hiyo ya mtandaoni.

''Nimekosa nini, shida iko wapi? '' mtu mwingine akauliza. ''Biblia inasema wapi kuwa makasisi hawawezi kuwa na wake warembo?''

Mada zinazohusiana