Namna ya kuwazuwia watoto kuangalia ujumbe wenye madhara mtandaoni?

Watoto wadogo wakitizama kompyuta aina ya tableti huku wakiwa wamejifunika blanketi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Je elimu na majadiliano ndio yanayofaa zaidi kuliko udhibiti wa teknolojia katika kuwalinda watoto na hatari za 'matumizi ya digitali'?

Wakati hali ya wasi wasi ikiendelea kuongezeka juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii yenye madhara kwa watoto wetu, tunaangalia ni mbinu gani zilizopo zinazoweza kutumiwa na wazazi kudhibiti taarifa wanazotizama watoto wetu na ni kwa muda gani wanaweza kuutumia kwenye mtandao.

Kazi ya kuwazuwia wasiwe kutumia muda wao mwingi wa maisha yao kwenye mtandao ni jmbo wazazi wengi anaifahamu.

Watoto wetu hutumia saa nyingi kwenye Instagram wakitaka "likes" - na mara nyingi hukabiliana na unyanyasaji wa mitandao - au kucheza michezo, kufuatilia watu maarufu kwenye YouTube na kutafuta urafiki ''kwenye ''makundi mbali mbali ya urafiki' kwenye WhatsApp.

Je ni vipi tunaweza kuwasaidi kupata ujumbe wenye madhara?

Programu ya inayochuja ujumbe imekuwepo kwa miaka mingi, lakini mara kwa mara wazazi wamekuwa na aibu ya kutumia teknolojia- jambo ambalo linaweza kuwa chanzo cha mizozo ya familia.

Lakini kwa sasa imeanzishwa programu ya udhibiti wa malezi ya kizazi kipya cha digitali na tayari imeingia sokoni, na wabunifu wake wanaahidi kuwaitawasaidia wazazi kuwadhibiti watoto wao kwa urahisi zaidi.

Kwa mfano mzunguko wenye picha ya Disney, Koala Safe na Ikydz, ni mifumo ambayo inadaiwa kuwa na uwezo wa kudhibiti kila kifaa cha digitali katika nyumba yako kwa kubofya kwenye programu ya smartphone.

Chanzo cha picha, Circle with Disney

Maelezo ya picha,

Mzunguko wenye mraba wa Disney ulitengenezwa kwa njia ya matumizi rahisi , lakini una maana yoyote muhimu?

Kazi ya kutengeneza programu hizi mpya zaidi ni kuziunganisha kwenye mfumo uliopo nyumbani kwako wa wi-fi. Unaingiza mzunguko huo kwenye boksi jeupe - ni kazi iliyoandaliwa na shule ya mitindo ya programu ya Apple school -na mara moja huorodhesha kila simu, kipatakalishi, ablet, na vifaa vingine vya nyumbani vya kielekkroniki na kutkuonyesha njia tofauti za kuvidhibiti.

Inaweza kuwa vigumu kutambua ni nani mmiliki wa kifaa. Mwanzoni nilifunga simu ya mumewangu kimakosa . Lakini baada ya kutambua kila anwani ya MAC ya kila kifaa - namba na herufi za utambulisho wa kila kifaa -imekuwa rahisi kutambua kila kifaa ni cha mtumiaji gani.

Halafu unaweza pia kuchuja matumizi ya vifaa hivyo kulinga na umri- watoto wa shule za chekechea, wa shule za awali , walio katika umri wa kubarehe , watu wazima au hata kuzuwia kurasa mitandaoi mingine kama ileya kutafuta wapenzi, uchezaji kamali, kulingana na ktaarifa ulizochagua kuzichuja.

Unaweza pia kufunga programu fulani au tovuti kama Fortnite na Instagram ya mtu yeyote? Na unaweza kuweka ukomo wa matumizi, kusitisha interneti kwa muda fulani , na kupanga muda wa kulala kwa watoto wako.

Lakini usingeweza kufanya hivi kwa kutumia programu ya zamani ya software ya kuchuja taarifa , na siku hizi watoaji wa huduma za interneti , makampuni ya huduma za usalama wa mtandao na watumiaji wa tovuti kwa sasa wanatoa huduma bora zaidi zinazosaidia familia kudhibiti zaidi matumizi ya huduma zao.

kilichojitokeza ni masuala yanayofanana. Wasichana wangu wenye umri wa miaka 11 na 13, wanapinga sana "ukiukaji wa haki ya taarifa za kibinafsi " walipogundua kuwa ninaweza kuona kila kurasa za mtandao walizozitembelea.

Wakati nilipowahakikishia kuwa si kwa nia ya kuchungulia wanachokifanya , bali nikuwasaidia kuwa na ukomo na kuhakikisha wanakuwa salama, walionekana kukubali kwa shingo upande matumizi ya vifaa vya udhibiti.

Utafiti wa mwaka 2018 wasichana na wavulana wenye umri wa miaka kati ya 11 na 16 kuhusu maswala ya Interneti, uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali ulionyesha kuwa 65% ya watoto hao walipendelea kuwepo na udhibiti wa wazazi.

Chanzo cha picha, Phil Coomes

Maelezo ya picha,

Laurel na mabinti zake . teknolojia ya kuchuja taarifa za mtandao inasaidia, lakini pia elimu na majadiliano yanafaa inapokuja katika swala la matumizi ya tovuti, anasema

Anne Longfield, kamishina wa maswala ya watoto nchini Uingereza , anahisi ni vizuri kwa wazazi kuweka vikomo vya matumizi ya mitandao miongoni mwa watoto.

"Intaneti inaweza kuwa chanzo kizuri, lakini pia inaweza kuwa kama msitu wa wanyama kwa watoto. hatuwezi kusema kuwa ni sawa kuwaacha watoto wetu kwenye mbuga ya wanyama usiku wakati wakiwa bado ni wadogo ," alisema.

"Kwa namna hiyo hiyo hatupaswi kufikiria kuwa ni sawa kwao kuzurura kwenye intaneti bila muongozo au masharti yoyote ."

Kuna hasara ya matumizi ya vifaa hivi vipya vya kuchuja matumizi ya mtandao , hata hivyo. Baadhi haifanyi kazi mara mwanao anapondoka nyumbani na kuwa mbali la wi-fi ya nyumbani . Na havitafanya kazi iwapo wi-fi imezimwa au kama huduma ya intaneti haipatikani kupitia data za simu ya mkononi.

Kwa hiyo ni njia nyingine zipi zilizopo?

" Kwa watoto wadogo simu ya Monqi (Simu iliyotengenezwa kwa ajili ya watoto) inaweza kuwa kifaa bora zaidi kutumiwa kwanza na mtoto ,"anashauri Ghislaine Bombusa, Mkuu wa masuala ya digitali katika kampuni ya Internet Matters.

"Au kama unahofu juu ya tovuti fulani unaweza kuweka programu ya rambazo salama kwenye masafa ya mtandao ya familia; hiyo inaweza kufaa na ni huduma ya bure . Pia unaweza kuweka programu salama ya kurambaza ya Google (Google Safe Search) au mfumo wenye udhibiti kwenye You Tube ( restricted mode on YouTube)

Njia nyingine ni kununua moja ya huduma za mtandao za mpya za kasi zaidi na ambazo baadhi yake hutoa huduma bora zaidi pamoja na huduma ya udhibiti wa wazazi inayoweza kuwekwa mapema.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Unajua ni nini watoto wako wanatazama kwenye mtandao?

Lakini Ben Halpert, ambaye alianzisha kampuni yenye makao yake nchini Marekani ya mtandao wa watoto Savvy Cyber Kids, anaonya kuwa kuna ukomo wa kile teknolojia inachoweza kufanikisha.

"pale mtoto anapofikia umri fulan, ushawishi wa watoto wenye umri sawa na wake au wanaweza hata kugundua njia ambazo zitawasaidia kupenya udhibiti wa wazai wao ," alinasema.

"Hata uweke teknolojia ya aina gani , haiwezi kamwe kumzuwia mtoto kupata taarifa ambazo ungependa wasizipate . Hi ndio maana kujenga uaminifu na watoto wako na kuendelea kuzungumzia juu ya matumizi ya teknolojia ni muhimu."

Wataalamu wengi wanasisitiza majadiliano, na elimu ni muhimu sawa na kutumia teknolojia inapokuja katika swala la kukulinda usalama wao watumiapo mtandao