Solksjaer: Bahati haitatusaidia dhidi ya Barcelona, kivumbi hii leo Camp Nou

Alexis Sanchez Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Alexis Sanchez amefunga magoli 47 kwenye michezo 141 games akiwa na Barcelona

Alexis Sanchez na Nemanja Matic wamesafiri wakiwa sehemu ya kikosi cha Manchester United kwa ajili ya mchezo wa marudiano leo usiku wa ligi ya mabingwa hatua ya robo fainali dhidi ya Barcelona

Mshambuliaji Sanchez amekua nje kwa majuma sita kwa sababu ya jeraha la mguu na kiungo wa kati Matic alikosa michezo mitatu iliyopita.

Wachezaji wote wawili walikosa mechi ya kwanza iliyochezwa Jumatano iliyopita ambayo Barcelona iliibuka na ushindi wa 1-0.

Matteo Darmian pia amewekwa kwenye kikosi cha wachezaji 22 baada ya kupona lakini Ander Herrera na Eric Bailly wako nje ya kikosi hicho.

Lionel Messi yuko tayari kucheza, baada ya kujeruhiwa usoni kwenye mechi ya kwanza alipogongana na Chris Smalling.Mshambualiaji huyo alipumzika kucheza mechi ya Jumamosi iliyopita ya La liga, waliotoka bila kufungana na timu inayoburuza mkia ya Huesca.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nemanja Matic na Alexis Sanchez

Sare yoyoye itawafanya Barcelona kuingia kwa mara ya kwanza kwenye hatua ya nusu fainali tangu mwaka 2015, lakini Kocha Ernesto Valverde amesema atakipeleka kikosi chake kushinda mchezo huo.

Aubameyang airudisha Arsenal nafasi ya 4 EPL

Solskjaer: Tutaifunga Barcelona nyumbani kwao

Mechi walizocheza

  • Barcelona haijawahi kupoteza mechi ya kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya Manchester United, huku walipokutana mara ya mwisho mwaka 2008 mwezi Aprili wakitoka sare ya kutofungana.
  • Katika mechi yao ya kwanza , Manchester United ilishindwa kupata mkwaju mmoja kuelekea golini kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya ligi ya mabingwa tangu mwezi March mwaka 2005 (0-1 dhidi ya AC Milan).
  • 90% ya magoli ya Manchester United kwenye ligi ya mabingwa msimu huu yamepatikana walipocheza ugenini sawa na (tisa kati ya kumi).Hata hivyo walishinda moja ya ugenini kati ya tano walizocheza katika hatua ya mtoano.

Mada zinazohusiana