Ratiba ya mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika Afcon 2019

Kombe la mataifa ya Africa

Mkufunzi wa timu ya taifa Stars nchini Tanzania Emmanuel Amuneke ametabiri kwamba majina makubwa katika kinyang'anyiro hicho huenda yakayaaga mapema mashindano hayo . Nyota huyo wa zamani wa Nigeria na barcelona anafikiri kwamba timu zisizo za majina makubwa katika mchezo huo huenda zikayashangaza mataifa makubwa.