Grrrrrr! Kwa nini ni jambo jema kuwa na hasira

Chanzo cha picha, Getty Images
Paka mwenye hasira
Data zilizokusanywa na Umoja wa mataifa, Shirika la biashara duniani, WTO na serikali mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa katika nchi nyigi, kiwango cha umasikini kinashuka na muda wa mwanadamu kuishi unaongezeka.
Wengi wa wale wanaoishi kwenye nchi zilizoendelea wako salama zaidi, na wenye uwezo mkubwa kwenye historia ya maisha ya mwanadamu.
Sasa kwanini watu wengi wanaonekana na hasira wakati wote?
Madereva wenye hasira za barabarani, kutoa kauli mbaya za hasira mitandaoni, wakati mwingine .
Oliver Burkeman-Mwandishi wa habari na vitabu aliyeandika jinsi ya kupata furaha
Je, kwa nini tunapata hasira? mambo gani yanasababisha na muhimu zaidi, je ni jambo baya?
Kwa nini tunapata hasira?
Chanzo cha picha, Getty Images
Dereva mwenye hasira
Ni vitu gani vilikua vikimfanya mtu awe na hasira dhidi ya mwingine?
Hasira ni mfumo uliochangamana,'' anasema Aaron Sell, Profesa wa Saikolojia na mtaalamu wa masuala ya makosa ya jinai katika Chuo cha Heidelberg mjini Ohio Marekani.
''Hasira ni kitu kinachodhibitiwa akilini. Ni namna ya kuingia kwenye mawazo ya mwingine na kuyafanya yakuthamini wewe zaidi. Ni njia ya kushinda kwenye mizozo kwa kuwafanya wabadilishe akili zao.''
Profesa Sell anaeleza,wanasayansi wameweza kubainisha kuwa ''sura yenye hasira'' inarithishwa -si suala la kujifunza-kwa sababu ''Watoto wasioona wanaweza kuonyesha hasira usoni.''
Chanzo cha picha, Getty Images
Unaweza kuwachezea hawa?
Unaweza kufikiri kuwa wazee wetu wa zamani hawakua na hasira wala kuwa katika ugomvi waliishi maisha marefu kuliko waliokuwa na hasira na wenye kugombana, lakini si kweli.
''Kilichokua kinatokea,'' Profesa Sell anasema ''walikua wakiyazungumza kwa namna nzuri ili kupata ufumbuzi na kwa njia hiyo waliweza kushinda''.
''Hapo zamani, watu ambao hawakua na hasira walikua wakionewa,'' anasema Profesa Sell-watu waliwaibia, waliwatishia ''matokeo yake walipoteza uvumilivu''.
Kinachotokea kwenye miili yetu tunapokua na hasira
Chanzo cha picha, Getty Images
Hasira hazibadili tu sura isipokua pia saikolojia yako
Kuelewa suala hili la hasira tunapaswa kufikiria namna linavyoathiri kisaikolojia, namna gani linavyotufanya tutende na kufikiri au kutofikiri.
Profesa Ryan Martin, mwenyekiti wa programu katika Chuo kikuu cha Wisconsin nchini Marekani, ni mtafiti wa tabia za hasira.
Anasema ''Unapokua na hasira mfumo wako mzima hubadilika, Profesa Martin anasema, ''kasi ya mapigo ya moyo huongezeka, kasi ya kuhema huongezeka, unaanza kutoka jasho na mfumo wa umeng'enyaji chakula hupunguza kasi yake ya kufanya kazi.''
Mabadiliko haya ya kimwili yana nia ya kukupa nguvu kukabili hali yoyote ya uonevu unaohisi kufanyiwa.
Na ubongo wako unafanya kazi hiyo pia.
''Tunafahamu pia kuwa wakati watu wakiwa katika hali hiyo watu hufikiri zaidi kujinasua wakiwa washindi au kulipa kisasi.'' Anaeleza Profesa Martin.
Hutaki kuwaza vitu vingine ikiwa unajaribu kufanyia kazi uonevu uliotendewa.
Kwa nini maisha ya kisasa yanachochea hasira?
Chanzo cha picha, Getty Images
Unamaanisha nini ''mimi wa 15 kwenye foleni''?!
Watu wengi katika nchi zilizoendelea hawana mambo mengi ya kuwafanya wawe na wasiwasi kama wazee wao wa zamani, sasa kwa nini maisha ya kisasa yana utofauti?
Ni rahisi, Profesa Martin anasema: ''Watu wako na pilika nyingi, na mahitaji yameongezeka kwenye maisha yao, hivyo madhara yake yanakua makubwa kwa sasa.''
Ikiwa tutapanga mstari kupata huduma kwenye duka na kuachwa hapo muda mrefu, tunapatwa na hasira kwa urahisi-Kwa sababu hatuna muda wa kupoteza.
''Ni vitu ambavyo tungeweza kuvikwepa, vitu vyenye kutufanya tuwe na hasira, anasema Profesa Martin.
Namna tunavyotenda tunapokua na hasira ''Si mara zote kunakua na matokeo mazuri katika ulimwengu wa leo.''
Je, tunaweza kudhibiti hasira kuliko tunavyofikiria?
Chanzo cha picha, Getty Images
Unapokua na hasira fikiri kabla ya kutenda
Ni wazi kumdhuru mtu uliye na hasira naye haisaidii wala haizai matunda- hivyo tunapaswa kutafuta namna nyingine ya kuelekeza hasira zako.
Tunaweza kudhibiti hali hii kuliko tunavyofikiria anasema Maya Tamir, Profesa wa Saikolojia, Chuo cha kiebrania mjini Yerusalemu.
Utafiti wake unaonyesha kuwa hasira si mara zote zinahitaji kuonyesha ukaidi.
Tumia hasira kwa kutenda jambo jema
Chanzo cha picha, Getty Images
Umeshawahi kutendewa isivyo haki? usipate hasira, badala yake tumia hasira yako kufanya ambo jema ili kupata matokeo chanya
Hivyo hasira inaweza kuleta hasara: zinaweza kutufanya viburi kwa matendo, maneno na hata kwenye mitandao ya kijamii.
Kama wale wanaotaka kulinda mamlaka zao na nafasi zao hupata hasira, inaweza kusababisha madhara makubwa sana-hata vita.
Lakini wana saikolojia pia wanasema hasira zinaweza kutupa nguvu kuchukua hatua pale tunapokosewa.
Lakini Mark Vernon mwanafilosofia, anaeleza namna ambavyo hasira zinaweza kukufanya kuchukua hatua chanya.
''Hasira inaweza kumfanya mtu kufanya jambo akiwa na moyo na kuwashawishi wengine kujenga hoja nzuri ili kuchukua maamuzi mazuri.
Hivyo hasira si jambo baya wakati wote, tunachotakiwa kufanya ni kuzidhibiti kwa busara.