Mshukiwa anadaiwa kuwachoma visu jiraji zake waliokuwa wakijinasua na moto aliouwasha nchini Korea

Makazi

Chanzo cha picha, Gyeongsangnam-do Fire Department/News1

Maelezo ya picha,

Mwanaume huyo alichoma moto makazi yake kabla ya kuwashambulia majirani

Mwanaume mmoja nchini Korea Kusini ameichoma moto nyumba yake na kuwaua kwa kuwachoma kisu wakazi walipokua wakikimbia. Watu watano wamuawa, Polisi wameeleza.

Watu wengine 13 wamejeruhiwa katika tukio lililotokea katika mji Jinju kusini mwa nchi hiyo.

Mtu huyo mwenye miaka 42 ambaye hajabainika kwa jina alishikiliwa na kukiri kufanya uhalifu, polisi walisema.

Sababu ya kutekeleza uhalifu huo hazijajulikana, hata hivyo polisi walisema sababu ni malipo yake yaliyocheleweshwa, kwa mujibu wa shirika la habari la Yonhap.

Chanzo cha picha, News1

Maelezo ya picha,

Makazi mjini Jinju sehemu ambayo uhalifu ulitokea

Mshukiwa huyo alichoma moto makazi yake yaliyokuwa kwenye ghorofa ya nne ya jengo la makazi. Mkuu wa polisi mjini Jinju amewaambia wana habari kwenye mkutano.

Kisha akashuka mpaka ghorofa ya pili ambapo aliwashambulia kwa kisu wakazi waliokuwa wakikimbia kwenye ukumbi .

Waathirika wa tukio hilo miongoni mwao ni binti wa miaka 12, mwanaume mmoja mwenye miaka 70, wanawake wawili wenye miaka ya 60 na mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka ya 30, liliripoti Yonhap.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Polisi waliwasili eneo la tukio

Alishikiliwa kwenye eneo hilo baada ya mkazi mwingine kutoa taarifa kwa polisi. Kikosi cha zima moto walizima moto kwenye makazi ya mshukiwa dakika 20 baadae.

Mshukiwa huyo alikua akiishi peke yake tangu mwaka 2015, polisi wamesema.