Mwalimu bora duniani apania kuwawezesha wasichana kupenda masomo ya sayansi

Mwalimu wa sayansi Peter Tabichi kutoka eneo la kijijini nchini Kenya , ambaye hutoa sehemu kubwa ya mshahara wake kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi maskini zaidi , ameshinda tuzo la dola milioni moja ($1m ) kwa kuwa mwalimu bora zaidi duniani.