Kwa nini wanawake ni silaha ya siri ya ugaidi?

Chanzo cha picha, Met Police
Shamima Begum (kulia) akiwa pamoja na marafiki zake wawili wa shule , Amira Abase na Kadiza Sultana, katika uwanja wa ndege wa at Gatwick mwaka 2015
Wakati taarifa za wanawake wanapogonga vichwa vya habari kwasabu ya ugaidi, mara nyingi kinachozungumziwa zaidi ni mchango wao kama wahanga au kama watu wanaoweza kuwa washirika katika kukabiliana na tisho la ugaidi
Kinyiume chake, wanawake wanaoshiriki na kuunga mkono itikadi kali wamekuwa wakati mwingine wanapuuzwa.
Mtizamo huu ulibadilika wakati msichana mtoro wa miaka 15 Shamima Begum alipoelezewa kama "msichana wa maana "kwa Islamic State baada ya kupatikana katika kambi ya wakimbizi wa Syria.
Miaka minne iliyopita , aliondoka nchini Uingereza na marafiki zake wawili kujiunga na IS, lakini akadai kuwa alikuwa "mke tu ".
Hata hivyo , Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza alimnyang'anya uraia wa Uingereza, akisema : "kama unaunga mkono ugaidi, lazima utapata matokeo ".
Anatarajiwa kuupewa masaada wa kisheria kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
wanawake katika itikadi kali
Kisa cha Begumkimeibua maswali mengi kuhusu uhusika wa wanawake ana utashi wao wa kushiriki ghasia zinazosababishwa na itikadi kali katika kundi la IS na makundi mengine.
Uchambuzi wa Rusi analysis unasema kuwa 17% waliopokea mafunzo ya ya itikadi kali katika bara la Afrika ni wanawake , huku utafiti mwingine ukionyesha kuwa 13% ya waliopokea mafunzo ya itikadi kali katika kundi la IS kutoka mataifa ya kigeni waliopo katika mataifa ya Iraq na Syria ni wanawake.
Idadi kamili si ya kuaminika na inaweza kuwa kubwa zaidi ya ile inayotajwa.
Chanzo cha picha, PA
Shamima Begum alikuwa na umri wa miaka 15 akiishi katika eneo Bethnal Green, London,wakati alipoondoka Uingereza mwaka 2015
Tafiti kadhaa zilizoungwa mkono na Rusi na tafiti nyingine zimechunguza nafasi ya wanawakekatika makundi ya ugaidi ya kimataifa kama vile IS na al-Shabab,moja kati ya makundi hatari ya kijeshi yanayosababisha mauaji barani Afrika.
Watafiti waliwahoji wanawake ambao walihusika moja kwa moja au kwa njia nyingine katika shughuli za al-Shabab , kubaini ni vipi waliweza kupata mafunzo, na athari walizopata wanawake hao kutokana na kushiriki katika ghasia za itikadi kali.
Kazi hiyo ya utafiti ilifanywa na wasomi wa Kenya, ambao waliweza kutumia uzoefu wao wa muda mrefu namawasiliano ya jamii zilizobainika kuwa katika hatari ya kupewa mafunzo itikadi kali.
IS na al-Shabab
Majukumu waliyopewa wanawake yalikuwa tofauti baina ya makundi hayo.
Wakawake katika al-Shabab mara nyingi wamekuwa wakifungiwa katika maeneo fulani jambo ambalo linaweza kuwa linatokana na majumu yao ya kitamaduni, kama wake wa wapiganaji na wasaidizi wa shughuli za nyumbani.Wakati mwingine wamekuwa wakifanywa kuwa watumwa wa ngono.
Wanaweza pia kusaidia katika kuwavutia wajumbe wapya. Utafiti mmoja nchini Kenya ulibaini kuwa wanawake walikuwa wanalaghaiwa na wengine ambao waliwaahidi kuwapatia kazi, msaada wa kifedha na kupewa ushauri nasaha.
kwa mfano, Hidaya ( sio jina lake halisi), mmiliki wa saluni, alipewa mafunzo na mteja ambaye alimuahidi kuwa atawekeza na kupanua biashara yake . Alishawishiwa kusafiri katika jimbo la mpakani ambako alitekwa nyara na kupelekwa ndani ya Somalia.
Chanzo cha picha, Getty Images
Katika kundi la IS, wanawake huingizwa kwenye kundi hilo hasa kupitia mtandao -na huchangia sana katika kuonyesha imani za kundi hilo.
Katika kisa cha Shamima Begum mwalimu wake alionekana katika propaganda za ushindi wa IS, licha ya madai yake kwamba alipokuwa Syria hakufanya jambo lolote isipokuwa kumtunza mumewe na watoto wake.
Wanawake katika kundi la IS pia wanaruhusiwa kuhudumu kama madaktari na wahudumu wa afya, kwa masharti fulani, ambapo kundi hilo linakikosi kinacholinda maadili ya wanawake.
Hivi karibuni zaidi baada ya kundi hilo lilipopoteza maeneo yake katika nchi za Iraq na Syria, kundi hilo limekuwa tayari kuwaweka wanawake katika maeneo ya nafasi za mapigano, likitumia gazeti la Al-Naba kuwaita wanawake kujiunga na jihad na kutoa ukanda wa video mwaka jana uliowaonyesha wanawake kadhaa wakiwa wamevalia magwanda ya jeshi nchini Syria.
Sally-Anne Jones alikuwa akitoa mafunzo kwa ajili ya IS na kusafiri hadi Syria, ambako anadhaniwa kuwa aliuawa katika shambulio la ndege zisizokuwa na rubani mwaka 2017
Hata hivyo , tofauti baina ya makundi hayo zimekuwa zikififia kutokana na kila kundi kujifunza kwa kundi jingine.
Nchini Somalia, ambako al-Shabab linajaribu kuanzisha kuanzisha taifa la kiisalamu linaloongozwa na sheria ya kiislamu(sharia), matukio ya wanawake kushiriki katika vita na kulipua mabomu ya kujitolea muhanga yamekuwa yakishuhudiwa.
Uchunguzi wa mashambulio ya mabomu ya kujitolea muhanga ya al-Shabab kati ya mwaka 2007 2016 ulibaini kuwa 5% yalitekelezwa na wanawake.
Hali ndivyo ilivyo katika maeneo mengine ya Afrika, kama vile Nigeria ambako kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limekuwa likiwatumia wanawake katika mashambulio ya mabomu ya kujitolea muhanga
Ni kwanini wanawakehujiunga na makundi ya jihad
Kuna sababu mbali mbali zijnazowapeleka wanawake katika mafunzo ya itikadi kali.
Kwa kiasi fulani, inaonekana kilichowatia hamasa wanaume pia ndicho kinachowavutia wanawake kujiunga na makundi ya itikadi kali, kama vile mvuto wa fikra na faida za kifedha.
Hata hivyo, mbinu zinazotumiwa kuwalenga wanawake tpia zilijitokeza, kama vile wito wa kuwataka wanawake warejee katika majumu yao ya kitamaduni
Kwa mfano, moja ya utafiti ulibaini kuwa wanaowaingiza watu katika kundi la al-Shabab walicheza na hisia za wasichana wa Kiislam wanaohofia kuwa kuendelea na masomo kutawafanya wachelewe kuolewa ili kuwavutia kujiunga na kundi hilo
"Kama nikipata mwanaume ambaye atanioa na kunilinda, kwanini nihangaike kusoma au kupata elimu ?", mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi aliwauliza watafiti.
Wengine walionekana kuvutiwa na matumaini ya kupata fedha na mafanikio mengine.
hata hivyo kufahamu kilichowafanya wajiunge na limekuwa ni jambo gumu . Wengi miongoni mwa wanawake tuliowahoji walidai kuwa waliingizwa bila utashi wao
kama Shamima Begum, baadhi wanadai kuwa hawakuhusika katika shughuli za kundi, au walishiriki kinyume na utashi wao na baadhi wanasema walikuwa ni waathiriwa.
Japo baadhi huenda walihusika kwa namna fulani katika shughuli za kundi hilo, kukana kuwa waliwajibika ni njia inayowafaa katika kujaribu kurejea katika jamii zao wanaporudi.
Kuhusu taarifa hii
Tathmini iliagizwa na BBC kutoka kwa wataalamu wanaofanyia kazi mashirika ya nje.
Martine Zeuthen ni mtaalamu wa maisha ya binadamu na tamaduni zao ambaye anaongoza mpango unaodhaminiwa na Muungano wa Ulaya Rusi ambao lengo lake ni kupunguza utoaji wa mafunzo ya itikadi kali na ugaidi katika mataifa ya upembe wa Afrika.
Gayatri Sahgal ni meneja wa utafiti katika taasisi ya Rusi. Huduma ya Royal United ( Royal United Services Institute (Rusi) ni taasisi huru iliyobobea katika utafiti wa ulinzi na usalama.

Wapiganaji 36 wa Islamic State wanyongwa Iraq
Iraq imewanyonga wapiganaji 36 wa kundi la Islamic State wanaohusishwa na mauaji ya makurutu 1,700 katika kambi moja iliokuwa ya Marekani mwaka 2014.