Sadaf Khadem: Mwanandondi wa Iran anayeogopa kukamatwa kwa kukiuka maadili

Iranian boxer Sadaf Khadem (R) beats the French boxer Anne Chauvin (L) in an amateur bout on 13 April 2019

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Sadaf Khadem (Kulia) na mwanabondia wa Ufaransa Anne Chauvin (Kushoto)

Mwanamke aliyejizolea sifa ya kuwa raia wa kwanza wa Iran kushiriki mashindano ya ndondi, anaogopa kurudi nyumbani kutoka Ufaransa baada ya kuarifiwa kuwa kibali cha kukamatwa kwake kimetolewa.

Sadaf Khadem alimpiga mwanbondia wa Ufaransa Anne Chauvin katika shindano la wanagenzi siku ya Jumamosi.

Alikua amepanga kurudi mjini Tehran na mkufunzi wiki hii.

Khadem alinukuliwa na magazeti ya spoti akisema kuwa anaamini huenda akamatwa kwa kukiuka sheria ya nchi hiyo ya mavazi ya mchezo huo.

Maafisa nchini Iran hawajatoa tamko lolote kuhusiana na madai haya, lakini mkuu wa shirikisho la ndondi nchini humo amekanusha madai hayo.

"Bi Khadem sio mwanachama wa mchezo wa ndondi nchini Iran kile anachofanya ni cha kibinafsil," Hossein Soori aliliambia shirika la habari Iran.

Khadem alipigana akiwa amevalia fulana ya kijani kibichi na suruali ya miguu fupi nyekundu iliyo na mkanda mweupe kiunoni- kuashiria rangi ya bendera ya Iran.

Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 24 aliamua kujaribu bahati yake katika mchezo huo nje ya nchi kutokana na mashrati magumu ya mavazi ya mchezo huo kwa wanawake.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Khadem alipewa mafunzo na Mahyar Monshipour, bingwa wa zamani wa masumbwi Mfaransa mwenye asili ya Iran

Lakini wakati alipokua safarini kuelekea mjini Paras akiwa na mkufunzi wakeMahyar Monshipour, mzaliwa wa Iran na bingwa wa zamani wa dunia wa mchezo huo mshauri wa waziri wa Ufaransa wa michezo, anasema kuwa waliambiwa waranti ya kukamatwa kwao imetolewa.

"Sikuvalia hijab , alafu mkufunzi wangu ni mwanamume, baadhi ya watu wana mtazamo mkali dhidi ya hatua hiyo."

Msemaji wa Ubalozi wa Iran mjini Paris ameliambia shirika la habari kwamba hawezi kuthibitisha madai ya kukamatwa kwa Khadem atakaporidi nyumbani.

Chanzo cha picha, Reuters

Kwa mujibu wa sheria za Iran, wanawake na wasichana walio chini ya miaka tisa hawaruhusiwi kuonekana hadharani bila kuvalia hijab na wale wanaokiuka sheria hiyo wanakabiliwa na tishio la kufungwa jela kwa siku kumi hadi miezi miwili au kutozwa faini.

Wachezaji wanawake nchini humo wanatakiwa kufunika nywele zao , shingo mikono na miguu wakiwa kwenye mashindano.

Hadi hivi karibuni, Khadem hangeli ruhusiwa kushiriki mashindano hayo bila kuzingatia masharti ya mavazi kya Kiislam.

Lakini chama cha kimataifa cha mchezo huo kilibadili masharti ya sare za wachezaji mwisho wa mwezi Februari mwaka huu.