Ugonjwa wa Bubble boy: HIV yatumika kuimarisha kinga ya watoto wanane

Chanzo cha picha, Courtesy of St Jude Children's Research hospital
Gael, ni mgonja katika hospitali ya utafiti wa watoto ya St Jude na mamake
Wanasayansi wa Marekani wanasema kuwa wametumia HIV kutengeza matibabu ya jeni ambayo yaliwaponya watoto wanane waliokuwa na ukosefu wa kinga imara mwilini kwa jina ''Bubble boy''.
Matokeo ya utafiti huo uliofanyika katika hospitali ya Tennesee yalichapishwa katika jarida la matibabu la Uingereza.
Watoto hao waliozaliwa bila kinga sasa wana kinga imara mwilini.
Watoto walio na tatizo hilo na ambao hawajapatiwa matibabu huishi katika hali mbaya na mara nyingi hufariki wakiwa wachanga.
Matibabu hayo ya jeni hushirikisha kukusanya uboho wa watoto hao na kusahihisha tatizo lililopo katika jeni muda mfupi baada ya kuzaliwa.

Chanzo cha picha, SPL
David Vetter, aliyejulikana kama Bubble Boy miaka ya sabuini
Jeni sawa iliotumika kusahihisha tatizo hilo iliingizwa katika toleo la mabadiliko ya moja ya VVU, virusi vinavyosababisha UKIMWI.
Watafiti wanasema kuwa watoto hao walitoka na kwenda nyumbani baada ya mwezi mmoja.
Dkt. Ewelina Mamcarz wa hopsitali ya St Jude , mwanzilishi wa utafiti huo, alisema katika taarifa ya hospitali hiyo: Hawa wagonjwa ni watoto ambao wanaitikia chanjo na wana mifumo ya kinga ya kufanya seli zote za kinga ambazo zinahitajika kuimarika ili kuulinda mwili kutokana na maambukizi kwa lengo la kuishi maisha ya kawaida.
"Mafanikio haya ni ya kwanza kwa wagonjwa walio na SCID-X'', aliongezea akitaja aina ya kawaida ya SCID.
Wagonjwa hao walitibiwa katika hospitali ya utafiti wa watoto ya St Jude mjini Memphis na Hopsitali ya watoto ya UCSF Benioff mjini San Francisco.
Je huu ni ugonjwa gani?
Kisa cha David Vetter pengine ndio kilichochulikana sana cha ugonjwa huo wa ukosefu wa kinga mwilini (SCID), ugonjwa ambao ulimzuia kushirikiana na ulimwengu
Ukipewa jina la utani la "Bubble Boy", Vetter alizaliwa mwaka 1971 akiwa na ugonjwa huo na kufariki akiwa na umri wa miaka 12 baada ya kufeli kwa upandikizaji wa uboho

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika sekunde 20 za kwanza za kuzaliwa kwake katika hospitali ya watoto ya Texas mjini Houston alitengwa na kuwekwa ndani ya plastiki ambapo aliishi hadi kufikisha umri wa miaka sita ambapo alipewa nguo maalum ya plastiki iliotengezwa na Nasa , shirika la anga za juu la Marekani.
Wazazi wake tayari walikuwa wamempoteza mtoto mmoja kutokana na ugonjwa huo kabla ya yeye kuzaliwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Je kuna tiba mbadala?
Kwa sasa tiba bora ya ugonjwa wa SCID-XI ni upandikizaji wa uboho na mfadhili wa tishu aliye na uhusiano wa karibu nawe.
Lakini kulingana na hospitali ya watoto ya St Jude , zaidi ya asilimia 80 ya wagonjwa hukosa wafadhili hao hivyobasi hulazimika kutegemea seli za damu kutoka kwa wafadhili wengine.
Mchakato huo huponya ugonjwa wa Bubble boy na husababisha madhara makubwa baada ya tiba hiyo.
Tafiti nyengine za matibabu ya jeni zilitoa tiba mbadala ya upandikizaji wa oboho , lakini tiba hizo mara nyengine hushirikisha tiba ya kemikali na huwa na matokeo ya magonjwa mengine mengi, ikiwa ni pamoja na matatizo ya damu na seli mundu.


Jaribio la dawa ya HIV lawapatia matumaini wanaoshiriki tendo la ngono lisilo salama
Jaribio la dawa ya HIV ambayo inapunguza viwango vya maambukizi limekuwa likileta matumaini nchini Wales kulingana na takwimu mpya.