Orodha ya Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda bora wa kike 2019 yatangazwa - mpigie kura umpendaye

Lucy Bronze
Maelezo ya picha,

Lucy Bronze wa England ndiye anayeshikilia taji hilo kwa sasa

Orodha ya Tuzo ya BBC ya mwanamke bora katika soka 2019 imetangazwa - na sasa unaweza kumpigia kura mshindi wako.

Wachezaji watano wa tuzo hiyo ya BBC World Service walichaguliwa na jopo la wataalamu, wakiwemo makocha, wachezaji, wasimamizi na waandishi habari.

Walioteuliwa ni :

  • Pernille Harder - Vfl Wolfsburg mchezaji wa kiungo cha mbele
  • Ada Hegerberg - Olympique Lyonnais mshambuliaji
  • Lindsey Horan - Portland Thorns mchezaji wa kiungo cha kati
  • Sam Kerr - Chicago Red Stars na Perth Glory mshambuliaji
  • Saki Kumagai - Olympique Lyonnais mlinzi

Mwisho wa kupiga kura ni Alhamisi Mei 2 saa 09:00 BST (08:00 GMT) na mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa Jumatano Mei 22 kupitia BBC World Service na mtandao wa michezo wa BBC.

Haya ndiyo unayostahili kuyajua kuhusu wateuliwa wanaowania tuzo hiyo, inayotolewa kwa mwaka wa tano sasa

Pernille Harder

Chanzo cha picha, Reuters

Umri: 26 Nchi: Denmark Mataji: 110

Klabu: VFL Wolfsburg Kiungo: Mbele

Harder alimaliza msimu wa 2017-18 kama mfungaij mkuu katika ligi ya Ujerumani BUndesliga kwa wanawake kwa kutinga mabao 17, na kuisaidia Wolfsburg kupata ushindi mara mbili nyumbani.

Alicheza na kufunga katika mechi yake ya kwanza kwenye fainali ya ligi ya mabingwa mwaka jana dhidi ya Olympique Lyonnais, lakini aliondoka bila ya taji lolote baada ya timu yake kufungwa 4-1.

Hatahivyo, Harder alifanikiwa kunyanyua mataji binafsi baada ya kupigiwa kura kuwa mchezaji bora wa Uefa 2018. Alikuwa mshindi wa pili katika tuzo ya Ballon d'Or kwa wanawake.

Ada Hegerberg

Chanzo cha picha, RONNY HARTMANN

Umri: 23 Nchi: Norway Mataji: 66

Klabu: Olympique Lyonnais Kiungo: Mbele

Hegerberg alishnda taji lake la tatu mtawalia katika ligi ya mabingwa akiwa na Olympique Lyonnais mwaka jana na kumliza kwa rekodi ya magoli 15 katika mahsindnao wakati timu yake ilipomaliza katika ligi ya Ufaransa na ya Ulaya.

Hegerberg amefunga mabao 193 kwa klabu hiyo tangu ajiunge mnamo 2014, huku 19 cyakitoka kaika mechi 18 za ligi msimu huu. Amesaini mkataba mpya wa muda mrefu msimu uliopita wa joto.

Raia huyo wa Norway ambaye haichezei tena timu ya taifa alikuwa wa kwanza kupokea tuzo ya Ballon d'Or kwa wanawake mnamo 2018.

Lindsey Horan

Chanzo cha picha, MARK RALSTON

Umri: 24 Nchi: Marekani Mataji: 62

Klabu: Portland Thorns Kiungo: Kati

Mnamo Septemba 2018, Horan alitajwa kuwa mchezaji mwenye thamani katika ligi ya taifa ya soka ya wanawake (NWSL).

Alikuwa mchezaji wa kwanza wa Portland Thorns kupewa heshima hiyo baada ya kufunga magoli 13 na kutoa pasi mara mbili zilizochangia ushindi katika mechi 22 katika msimu wa kawaida.

Horan aliisaidia klabu yake kufika katika fainali ya ubingwa wa NWSL kwa kumaliza katika nafasi ya pili kwenye orodha ya ligi lakini walishindwa na timu ya North Carolina Courage.

Sam Kerr

Chanzo cha picha, DANIEL POCKETT

Umri: 25 Nchi: Australia Mataji: 67

Klabu: Perth Glory na Chicago Red Stars Kiungo: Mbele

Kwa sasa anazichezea timu za Perth Glory na Chicago Red Stars, Kerr ndiyo mfungaji mkuu katika NWSL, na mnamo Januari mwaka huu alijishindia rekodi kama hiyo katika ligi ya wanawake Australia.

Alishinda tuzo ya pili mtawalia ya golden boot katika NWSL mnamo 2018, akikamilisha kwa magoli 16 na usaidizi mara nne katika mechi 19 kwa timu ya Red Stars.

Kerr alipewa wadhifa wa kapteni wa timu ya taifa ya Australia mnamo Februari na kuiongoza timu hiyo katika taji la mataifa .

Saki Kumagai

Chanzo cha picha, FRANCK FIFE

Umri: 28 Nchi: Japan Mataji: 102

Klabu: Olympique Lyonnais Kiungo: mlinzi/mlinzi wa kiungo cha kati

Mshindi wa kombe la dunia katika timu ya taifa ya Japan, Kumagai alikuwa kapteni wa timu hiyo ya taifa katika mashindano ya taji la bara Asia mnamo 2018 - ushndi wao wa kwanza katika mashindano hayo katika muda wa miaka minne.

Alikuwa mojawapo ya wachezaji wa Olympique Lyonnais waliochangia ushindi katika msimu wa 2017-18 na ana mataji matatu ya ligi ya mabingwa yaliotokana na jitihada zake.

Kumagai amekuwa na jukumu kubwa katika umahiri wa rekodi ya ulinzi ua klabu hiyo ya Ufaransa katika kutafuta ushindi kwenye ligi; timu hiyo imefungwa mabao 6 katika mechi 20.